Kwanini kitabu cha Enoch kinapingwa vikali na Wanathiolojia?

Hivi unaweza nipa ushahidi kwenye biblia inapokiri kuwa wanefili walikuwa ni uzao wa malaika maana 90% humu mnasema tu WANA WA MUNGU ni wale walioasi sijui kina semyaza azazel na zamuzammim..... Ila hamsemi je wapi imeandikwa kuwa walikuwa ni malaika hicho ndio nataka mniambie

Kingine biblia iko wazi kabisa petro wa pili sura 2:5 kwamba alikuwa ni MJUMBE WA BWANA sasa kma alikuwa anawapa ujumbe wa maneno ya Bwana ili gharika likija wapone kivp awahubirie watoto wa MALAIKA???

Agano jipya zima linamtambua Nuhu kma mhubiri na aliokolewa sababu ya utakatifu wake na sio kwa sababu hakuchanganya na malaika!!!! Kivp agano jipya (hata vilivyotolewa) zima sijaona mtu hta mmoja akisema gharika lilikuja sababu ya malaika kuchangamana na wanadamu!!!!

Mie napenda kujifunza hivyo basi kma mnaamini malaika ndio walioongelewa hapo kama WANA WA MUNGU je unaweza niambia kwanini Nuhu ahubirie watoto wa malaika ilihali nyie ndio mnaona sababu ya gharika alafu je akiokoka na kumfuata Nuhu ina maana kizazi cha watoto wa malaika kingeendelea???

Mnazidi kutuchanganya!!!
 
Swali lako linachanganya!Unaruka ruka sana toka mada moja mpaka nyingine, sio kuwa najua kila kitu hapa tunajaribu kueleweshana na itakuwa ngumu kama hatukai kwenye mstari mmoja ili tufikie malengompaka nahisi inaonekana jibu unalo tayari ila una-argue kutaka ku-discredit.

Swali ulilouliza mwanzo lilihusu wana wa Mungu....sas umeruka kwenye wanefili mara uhubiri wa Nuhu utaelewaje kama hutakimkujifunza hatua kwa hatua......................
 
Binafsi kuhusu kitabu cha Henoko kuondolewa kwake sababu kuu ni mtiririko (Sequence) kwa sababu ukikisoma ni kama kinabidi kiwe katikazi ya Maelezo ya kitabu cha mwanzo ilhali Mwanzo yenyewe inajitosheleza!
Sababu kuu kinakinzana na biblia......


“And for all of you sinners there shall be no salvation". Enoch Chapter 5:6i

Hivi wapi kwenye biblia wanakataza mtu mwenye dhambi asiokoke???

Enoch 7:2 inadai wanefili walikuwa futi 450!! Yaani walikuwa wanaurefu kuliko safina ya Nuhu..... Sasa biblia inasema Nuhu aliskia sauti kuwa wanaomba awafungulie kivp mtu mkubwa kuliko chombo anachoomba aingie yaani ni sawa na wwe uombe uingie kwenye shimo la panya inawezekana kweli

Kuna mistari kibao nikiishusha hapa mtakichanachana hicho kitabu
 
Ndio nasema kama ni wana wa Mungu kivp Nuhu awahubiri? Maana tumeshaambiwa na petro kuwa Nuhu aliwahubiri sasa ndio swali langu linakuja kama hao wana wa Mungu walizaa na wanadamu ina maana wangemsikiliza wangeingia kwenye safina?

Je wangeingia kwenye safina si ina maana kizazi cha malaika na wanadamu kingeendelea?

Sijaruka swali mkuu nachotaka tuendelee sababu umeshasema ni wana wa Mungu well and good ndio linazaa swali lingine kwanini wahubiriwe?
 
Waprotestant wamepunguza kutoka kwenye Biblia ya kikatoliki, ila hata Biblia ya kikatoliki wakati ikiundwa kwa kuunganisha vitabu vipo vitabu vingi tu vilivyoachwa kwasababu mbalimbali.

Ndio nikasema upo uwezekano wa kitabu kutowekwa kwenye Biblia kwasababu binafsi ( self interest) hasa Kama kinawasemea vibaya japo sababu watakazotoa ni nyingne.
 
Kwa faida ya wanajukwaa wote unaweza toa mfano wa kitabu kimoja unachohisi kimetolewa kwa self interest???
 
Kwa faida ya wanajukwaa wote unaweza toa mfano wa kitabu kimoja unachohisi kimetolewa kwa self interest???
Tusiseme kimetolewa, tuseme hakikujumuishwa. Mfano ni hicho kitabu Cha Enock na sababu yake kubwa mtoa post ameiweka mwenyewe. Kitabu kinawapamba watu weusi Kama ndio wa kwanza kuumbwa na kuwaponda wazungu. Hili wazungu wasingeweza kulikubali lienee duniani kote.
 
Lengo kuu la kumhubiria mtu ni nini Tuanzie hapa? Lengo kuu ni kujaribu kumshawishi yule aliyepotoka aziache njia zake na auendee unyofu! Kama atauendea unyoofu basi ile dhana ambayo ingeleta gharika isingekuwepo tena au wewe unaonaje? Au unadhani alikuwa anawahubiria waingie kwenye safina?

Safina ilikuwa kwa ajili ya kumponya Nuhu vinginevyo ingetengenezwa safina kwenye say public square na kumwambia kila mmoja anaetaka aingie asiyetaka aache.
 
Brother! Brother ! Brother! Kuna kitu kimoja unatakiwa u-note - context ya Biblia kabla ya Kifo cha Yesu na Context ya Biblia baada ya kifo cha Yesu . Baada ya kifo cha Yesu kuna kitu kilibadilika kuhusu wokovu wa mwenye dhambi.

Kuhusu urefu wa wanefili -unataka kusema kuwa walikuwa warefu kuliko kina cha maji na safina kwa pamoja? Na swali jingine Wanadamu enzi za nuhu walikuwa kimo gani????
 
Nmeuliza mwenye ushahidi hapa kuwa kimeandikwa na henoko mwenyewe auweke naona wote mnasupport kitabu ingawa mwandishi hamumjui

Kimeandikwa miaka 300 kabla ya kristo hivi kipindi hicho Henoko alikuwa hai???

Henoko anadai ukiwa na dhambi huwezi samehewa ilihali biblia nzima ilishatabiri kuwa Yesu atakuja kutukomboa kutoka mikono ya dhambi na shetani??

Haya basi mnisaidie ipi ina uzito kuhusu watu weusi au HAKUNA KUSAMEHEWA DHAMBI
 
Agano la kale mbona walitabiri kuwa Yesu atakuja na ataokoa ulimwengu manabii Yeremia na isaiah walitabiri kuwa MESSIAH atakuja kutukomboa...... Pia zaburi, malaki na zakaria walitabiri kuwa MKOMBOZI atakuja hivyo walitoa tumaini kwa wenye dhambi kuwa MKOMBOZI atakuja ila kitabu cha HENOKO kinasema kuwa ukiwa na dhambi imekula kwako hakuna Neema ya KUKOMBOLEWA huko mbele sasa ndio biblia gani iweke kitabu kama hicho???

2. Wanefili kwenye biblia yaani hakuna aliyemzidi mfalme Ogu wa Bashani aliyekuwa na urefu wa futi 13 anatajwa kwenye kitabu cha kumbukumbu la torati 3 sasa anaposema watu walikuwa warefu futi 450 huoni angepingana na mwandishi wa kumbukumbu la torati???

Pia kingine hata kma maji yaliwazidi kimo ila jiulize unaombaje kuingia kwenye boti ambayo umeizidi urefu na upana ??? Yaani hata kma amezidiwa kiasi gani unawezaje kuwa na mwili kama wa THE BIG SHOW alafu unaomba kuingia kwenye starlet inawezekana kweli????

3.Naomba unitajie mwandishi wa Henoko ni nani?? Maana kimeandikwa miaka 300 kabla ya kristo na kiliandikwa na watu wengi akiwemo methuselah sasa mnakipaje credibility kitumike kwenye biblia??

4. Henoko anakataa kwenye kitabu chake kuwa Yesu ni mwana wa Mungu yeye anamuita malaika tu..... Sasa mtu kama hatambui Uungu wa Yesu na kumuona kama malaika tu kivp mkiweke hicho kitabu kwenye biblia

Anyway najua utasema tunakitafsiri vibaya ila jua tu kwamba kilikataliwa sababu hakijulikani mwandishi ni nani hasa maana kimeandikwa kipindi Henoko ameshakufa na kuna utata kuwa kuna mistari ilipandikizwa !!!
 
Kwahiyo ina maana Hao NUSU malaika NUSU wanadamu wangepona kwenye gharika hivyo basi wangeendelea kuishi mpaka leo???

Embu nitoe tongotongo kidogo
 
mkuu kwan kitabu cha ayub aliandika nani na lin? vitabu vingi vya agano la kale vina utata wa nani aliandika na aliandika lin. Hiyo ni kwasababu hapo mwanzo watu hawakupay antetion kuhusu mwandishi kikubwa ni ujumbe ulioandikwa.
 
Kwahiyo ina maana Hao NUSU malaika NUSU wanadamu wangepona kwenye gharika hivyo basi wangeendelea kuishi mpaka leo???

Embu nitoe tongotongo kidogo
Unauliza maswali mazuri sana, naomba ungekuwa unatafakari kwanz kabla ya kuuliza haya maswali kwa sababu ninapoyasoma naona wazi kwamba ukweli unaujua na kuelewa umeelewa nnachojiuliza sijaelewa ulikisoma vipi kitabu cha henoko,kwa sababu kuu ya Mungu kuleta gharika ni kuwa Wale nusu malaika nusu wanadamu licha ya uovu binadamu walishindwa kutekeleza matakwa yao hatimaye wakaanza kuwaua na kuwala na madhila mengi yaliyokuwa kinyume cha wanaadamu kiasi kwamba kilio cha wanadamu kikafika Mbinguni ndiposa swala la gharika likawa.

Kwa hiyo endapo wangekuwa wanatenda mambo ya kawaida wangelikuwa wanaishi tu kama binadamu huku wakisubiri siku ya hukumu kwa maana ukisoma hicho kitabu hasa the first book utaona kwamba judgement yao ilishafanyika tayari na ndio maana walikuwa banned kurudi Shamayim.

Na kuonyesha kuwa wangelikuwepo ni kwamba hata kina Shemyatsa (let me call the original 200 bado wapo ndio hawa kina shetani na pepo wachafu tulioambiwa ole wetu maana wametupwa duniani.
 
Kwa hiyo jibu unalo ,unabishana sababu ya ubishani! Halafu ndugu yangu Maswala mengine ni ya kiimani Zaidi(Rejelea Maana ya Imani) ukiyachukulia kama historical events ukataka date of publisher of the book of Hanok seriously!

Pili, Kutumika au kutotumika kwa kitabu The original compilers and translators ndio wanajua sababu na vigezo vilivyotumika mimi na wewe sanasana tuta-speculate tu.

Tatu jambo la msingi ni kujifunza yale mazuri yaliyomo na kuyatumia kwa matokeo chanya na yale mabaya kuyaacha yawe funzo ya jinsi ipasavyo kufanya. Na mwisho imani yetu ikapate kuzidi katika kile tunachokisimamia kwa sababu itatufaa nini kuupata ulimwengu huu na kuukosa uzima wa milele.

I am neither a pastor nor a good christian so dont get me wrong!
 


Sababu mimi na wewe hatuzijui??? Tutaspeculate??? Labda wewe ila kwa wengine iko wazi kabisa kikao kilichokaa constantinople mwaka 380+ AD kiliamua kuweka vigezo ili wachuje vya kuwekwa na vyakutolewa na vigezo viko wazi kwenye vitabu vya wasomi wa kipindi hicho kina St Jerome na Papa Damasus waliainisha vigezo vilivyotumiwa hata ukigoogle majina yao utapata hivo vigezo so sio speculation vipo wazi na vitabu vyote vilivoachwa viko wazi kabisa vinapatikana so ukiona kiliachwa kimakosa unaweza andaa andiko lako la kitafiti kupinga tafiti za wale wasomi wa kale na kitawekwa kwani kigumu ni kipi?? So hakuna speculation hilo moja

2 Hoja haikusema mazuri alafu mabaya tuache ila swali je kiwekwe kwenye biblia ngoja nkupe contradiction mojawapo alafu upime mwenyewe....

Enoko anatuhadaa kwamba waliotengeneza safina walikuwa malaika

Enock 67:2
"Nawaona malaika wakitengeneza safina"

Ilihali biblia inaweka wazi kabisa kuwa alitengeneza ni mwanadamu sio malaika tufuatane

Mwanzo 6:14
14 Ujifanyie safina ya mti wa mvinje; fanya na vyumba ndani ya safina, ukaifunike ndani na nje kwa lami.

Sasa ulitaka biblia iweke kitabu kinachokinzana na kingine???

3. Unasema tujifunze mambo mazuri!! Je mtu atajuaje kipi kizuri kipu kibaya ngoja nkupe mfano

Jude 1:14-15: "...Behold, the Lord cometh with ten thousands of his saints, to execute judgment upon all, and to convince all that are ungodly..." KJV

Book of Enoch 1:9: "And behold! He cometh with ten thousands
of His holy ones to execute judgment upon all, and to destroy all the ungodly..."

Hivi mstari kama huu utajifunza mazuri gani wakati inaongea tofauti kabisa na biblia?? Ukishaamini kitu unatakiwa ukiamini nje ndani sio nusu nusu maana ni ngumu kujua ukweli ni upi na uongo ni upi ..... Kwa mfano wewe nikikuhoji mstari huo je nani mkweli YUDA au HENOKO???? Kma kamnukuu Henoko kwanini watofautiane maneno mazito kuhusu kuja kwa YESU KRISTO

Tuanzie hapo
 
mkuu kwan kitabu cha ayub aliandika nani na lin? vitabu vingi vya agano la kale vina utata wa nani aliandika na aliandika lin. Hiyo ni kwasababu hapo mwanzo watu hawakupay antetion kuhusu mwandishi kikubwa ni ujumbe ulioandikwa.
Nmeweka sababu nyingi sio moja tu

1. Biblia inasema Nuhu alijenga safina ila Henoko anasema Malaika ndio walijenga safina

2. Henoko anamtambua Yesu kma malaika tu wa kawaida ila Biblia nzima inamtambua Yesu kama Mwana wa Mungu

3. Henoko anasema ukifanya dhambi unahukumiwa yaani hakuna neema ya kuokoka ila Biblia inatupa tumaini kwamba Mungu anasamehe dhambi zetu

4. Henoko anasema wana wa Mungu ni malaika ilihali Biblia inasema Wana wa Mungu ni wale wanaotenda mapenzi ya Bwana yaani wanaomcha Mungu

5. Henoko anasema wanefili walifika futi 450 ilihali Biblia inatueleza mtu mrefu zaidi kurekodiwa alikuwa Futi 13.5 Yaani mfalme ogu wa bashani

6. Henoko anasema Yesu atakuja kuhukumu na kuangamiza wenye dhambi ila Biblia inasema Yesu atakuja kuhukumu na kuokoa wenye dhambi

Anyway tofauti zipo nyingi so ukilazimisha kitabu cha Henoko kisikilizwe basi amini pia kuwa HAKUNA MSAMAHA na sisi wengine wenye dhambi hatutaonja mbingu!!!!
 
Kwahiyo kama wanefili wangekuwa watu wazuri tu wangekuwepo mpaka leo yaani Mungu angekuwa tayari kuona kizazi cha malaika na wanadamu?

Maana naona unaongelea malaika tu ila huelezi hatma ya vizazi vya watoto wa malaika?? Je huoni vingechafua uzao wa Hawa na mwisho wa siku kubaki na viumbe hao wa ajabu pekee kwenye uso wa dunia??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…