zitto junior
JF-Expert Member
- Oct 7, 2013
- 20,537
- 31,729
Hivi unaweza nipa ushahidi kwenye biblia inapokiri kuwa wanefili walikuwa ni uzao wa malaika maana 90% humu mnasema tu WANA WA MUNGU ni wale walioasi sijui kina semyaza azazel na zamuzammim..... Ila hamsemi je wapi imeandikwa kuwa walikuwa ni malaika hicho ndio nataka mniambieWana wa Mungu limetokea kama mara 61 kweny Biblia likiwa kama Wana wa Mungu au Mwana wa Mungu: Mwanzo 6;2,Mwanzo 6;4,Ayubu 1;6,Ayubu 2:1, Zaburi 29:1, Hosea 1:10, Mathayo 4:3, Mathayo 4:6, Mathayo 5:9, Mathayo 8:29, Mathayo 14:33, Mathayo 16:16, Mathayo 26:63, Mathayo 27:40, Mathayo 27:43, Mathayo 27:54, Marko 1:1,Marko 3:11, Marko 5:7, Marko 15:39, Luka 1:35,Luka 4:3,Luka 4:9, Luka 4:41, Luka 8:28, Luka 20:36, Luka 22:70,Yohana 1:34, Yohana 1:49, Yohana 5:25, Yohana 9:35, Yohana 10:36, Yohana 11:4, Yohana 11:27, Yohana 19:7, Yohan 20:31, Matendo ya Mitume 8:37, Matendo ya Mitume 9:20, Warumi 1:$, Warumi 8:14, Warumi 8:19, Warumi 9:26, Wakorintho 1:19, Wagalatia 2:20 Wagalatia 3:26, Waefeso 4:13, Wafilipi 2:15, Waebrania4:14, Waebrania 6:6, Waebrania 7:3,Waebrania 10:29, 1 Yohana 3:1, 1 Yohana 3:2, 1 Yohana 3:8, 1 Yohana 4:15, 1 Yohana 5:5, 1 Yohana5:10, 1 Yohana 5:13, 1Yohana 5:20, na Ufunuo wa Yohana 2:18.
Ukisommistari hiyo yote katika Muktadha wake utagundua kuwa hakuna contradiction ila contradiction inaonekana kuwapo/kuwepo katika kuelewa.Muktadha wa wana wa Mungu unajengeka katika Makundi matatu/vifungu vitatu.Fungu la kwanza uko katika Agano la kale na Ufunuo wa Yohana,fungu la pili katika injili (yaani Mathayo Luka Marko na Yohana) na fungu la tatu linajitokeza katika Matendo ya mitume Warumi naNyaraka za paulo.
Ukisoma maelezo yaliyoko katika Agano utagundua Mandhari(Setting ya hawa wana wa Mungu ni Mbinguni-Yaani wana hawa wa Mungu asili yao ni Uungu tunaweza kusema hawa ndio wana wa Mungu halisi kwa kuwa Tangu kuumbwa kwa ulimwengu walikuwepo ukisoma kitabu cha Henoko yaani hawa ndio kina Gabriel upande mmoja na kina Shemyatsa na kundi lake upande wa pili.Kwa hiyo wana wa Mungu asili yao ni mbinguni.
Ukija kwenye Injili Tunaona hapa anazungumziwa Yesu kama -mwana wa Mungu -huyu naye asili yake ni mbinguni kwa hiyo naye ni mwana wa Mungu.
Sasa swali linakuja inakuwaje
Kwa hiyo Mwanzoni wana wa Mungu asili yao ilikuwa mbinguni,baadhi wakaasi kwa kujichafua na binadamu,original plan ya Mungu ikawa imeharibika mpaka ikabidi Yesu/Yahusha(Ben of Adam) aje duniani (You know the story)kuja kurekebisha ku-salvage kwa(sacrifice) kumwaga damu yake msalabani .Kwa hiyo Baada ya kifo cha yesu Watu wote wanaojiunganisha na Yeye yule aliyekubali kufa Msalabani wanapata uwezo kuwa wana wa Mungu ndio maana neno linasema Wale wote wanaofanya mapenzi ya Mungu which means sio kila mtu.Yohana 1:12,Warumi 1:4,Wagalatia 2:20 etc etc
Kingine biblia iko wazi kabisa petro wa pili sura 2:5 kwamba alikuwa ni MJUMBE WA BWANA sasa kma alikuwa anawapa ujumbe wa maneno ya Bwana ili gharika likija wapone kivp awahubirie watoto wa MALAIKA???
Agano jipya zima linamtambua Nuhu kma mhubiri na aliokolewa sababu ya utakatifu wake na sio kwa sababu hakuchanganya na malaika!!!! Kivp agano jipya (hata vilivyotolewa) zima sijaona mtu hta mmoja akisema gharika lilikuja sababu ya malaika kuchangamana na wanadamu!!!!
Mie napenda kujifunza hivyo basi kma mnaamini malaika ndio walioongelewa hapo kama WANA WA MUNGU je unaweza niambia kwanini Nuhu ahubirie watoto wa malaika ilihali nyie ndio mnaona sababu ya gharika alafu je akiokoka na kumfuata Nuhu ina maana kizazi cha watoto wa malaika kingeendelea???
Mnazidi kutuchanganya!!!