Kwanini kitabu cha Enoch kinapingwa vikali na Wanathiolojia?

Kuna bonge la kitabu lilitolewa pia lilikuwa linaitwa gospel of Thomas!....... Nafikiri hiki ndo kilikuwa kitabu bora kabisa katika bibilia!.....Sisi wanadamu hasa wa dini ya kikatoliki ni wabaya sana![emoji22]
Katoliki linausikaje hapo, umeshajiuliza kwanini madhehebu yote ya kikristo isipokuwa wakatoliki wanaitwa wa protestant? Hao ndiyo wamevikataa hivyovitabu ,biblia inayotumiwa na wakatolki ina vitabu 72 pamoja na hicho cha Ester ila biblia inayotumiwa na waprotestant inavitabu 66.

Mfano kunakitabu kisuri sana kina mafundisho ya Hekima kinaitwa Yoshua bin Sira kwenye biblia zakiprotestant hakipo.
 
Mkuu Tlg ubarikiwe kwa darasa zuri unalowapa hiki kizazi kinachojifanya kinajua sana kila kitu kuliko watangulizi wao kiimani
 
Reactions: Tlg
Ndugu Yangu Umechambua Vzr Sana Mpaka Nimefarijika Kiukweri Yani Respect
 
Ndugu Yangu Umechambua Vzr Sana Mpaka Nimefarijika Kiukweri Yani Respect
Mkuu hicho kitabu kimewekwa humu ni vzuri ukisome chote kabla hujafanya conclusion.... Ukisubiri wakuchambulie utalishwa matango pori

Mfano hiyo Atlantis wanasema imezama ila ukiwauliza mabaki hata ya miamba ya huo mji yakwapi hawajui ilihali bara lililozama likazaa kisiwa cha borneo na sumatra mpaka leo lipo huko asia ya kusini hadi australia

Kwa ufupi Atlantis ilitumika kwenye hadithi za plato na kitabu chake cha republic kma mfano wa nchi PERFECT ambayo inatakiwa viongozi wote wa dunia wafuate mfano wa nchi ile zaidi ya hapo watu wanatunga mambo kuwa hilo bara lilikuwepo ila ushahidi haupo
 
Chief Umeongea Kwa Hisia Mpaka Moyo wangu umepata Tetemeko La Mwili

Inaonekana Una Mengi Sana Moyo Mwako Ambayo Binadam wengine Unaweza Kushare Nao Hayo Mambo Mazur uliyo Nayo
 
Naammm Hapo Nimekuelewa Sana
 
Chief Ninakufatilika Kwa Umakin Mkubwa Sana Tafadhari Mwaga Data Za Kutosha Mungu Atakulinda Na Kukupa Afya Njema
 
Mchango tu:

Kosa la kwanza ni 'kumtafuta mungu wa kweli' wakati ni suala la imani.

Kosa la pili ni kudhani unaweza kuja kupata jibu hilo.

Unajua kwa nini?
Kwa sababu mungu wa kweli yukoje?
Yaan utajuaje mungu ni nani... Yupo katika form ipi... Kama huamini unadhani 'utamwona'?

Binafsi, Mungu ni Mungu.
Sina namna ya kum-describe kwa sababu yeye ni Mungu na sijawahi kumuona Mungu kabla...

Hata kama umeambiwa umeumbwa kwa mfano wake, haimaanishi moja kwa moja ni muonekano... Hiyo ni just lost in translation. Mfano wake inaweza kuwa katika intelligence, au reasoning au ethics, etc. Kwa sababu those things are what makes us unique.

Nashauri tusome vitabu vyote hata vilivyokuwa removed, maana hekima inakuja baada ya 'kujua yote'.
 
Una uhakika gani kiliandikwa na Enoch yule yule bwana? Hata akina sauli tu walikuwa wawili zama tofauti una uhakika gani enoch ni mmoja tu? Kuna uwezekano kuna maandiko yaliyopotoka maana pia kuna vitabu vinaitwa vya musa na vinatumiwa na wachawi na secret societies.

Tumeambiwa tuchunguze roho hizo iwapo zinatoka kwa Mungu, na tunawatambuaje wasiotoka kwa Mungu au visivyo toka kwa Mungu ... NI KWA MATUNDA YAO kama andiko linaleta uchonganishi na kuchanganyikiwa mjiulize mara mbili iwapo kweli ni andiko lililoletwa kwa roho mtakatifu.

Inasemekana baadhi ya maandiko ya hicho kitabu cha Enoch yanasuggest wazungu ni uzao wa malaika wabaya na binadamu, ili iweje labda kwa wakati huu ambao we have more pressing matters like the second coming of Jesus Christ[emoji53].
Tusipotezewe muda na vitabu vilivyoondolewa maana kuna hekima pia iliyotumika na inawezekana ndio mbinu za kuleta kutoamini miongoni mwa waumini na mara paap Yesu huyu hapa, KUMBUKA MAANDIKO "ASIYEAMINI AMEKWISHA KUHUKUMIWA..."
 
Iyo Paragraph Ya Mwisho Nimeielewa Zaid Chief
 

Kuna Vitu huwa tunajipa vichwa ngumu sana kama mtu unaweza kuchanganyikiwa basi utachanganyikiwa tu
na kama umeona kuna mkanganyiko nakuomba usije jaribu kitu hiki cha kusoma biblia iliyoandikwa kwa kiingereza na ukaufuata msitari huo huo katika kiswahili.

Kwa kufanya uchunguzi kama huo imenisaidia kuelewa sana neno tofauti na nilivyokuwa mwanzo

Kuna mahali ukisoma katika kiswahili unakuta kabisa maana imepotea ama inapungua ukisoma katika kiingereza unakuta kile kitu kipo full kabisa.

Mfano mzuri chukua bible yako soma isaya 60 then anza kulinganisha na bible ya kiingereza hapo sasa ndio utajua Neno La Mungu linakaa moyoni wala sio kitabuni.

Kusoma vitabu vilivyoondolewa katika biblia na kujua sababu inatukomaza kiroho pia.

nakumbuka hapa kunawengine wanasomakwasababu wanahitaji wakafundishe wengine, wengine wanasoma kama burudani,wengine wanasoma kwasababu mtumishi anawashauri wasome neno la Mungu.
Hata biblia yenyewe inamikanganyiko usipokuwa makini kwahiyo suala la kuzuia mtu kusoma sio tatizo.

Ndio maana hata ukisoma Biblia haisemi uwe unasoma Biblia inasema Usome Neno.

Neno halikai katika maandishi neno Linakaa Moyoni mwako ndio maana Biblia anaweza kuibeba hata mchawi ama mtenda dhambi na asidhurike lakini mtenda dhambi na ama mchawi hawezi kumgusa mtu aliye na neno la Mungu.

Ndio Maana wakristo waleo mnapata shida sana mtu akikwambia thibitisha kwa Mungu yupo mnakuwa mnatoa mirejeo isiyokuwa na mantiki kwasababu hamtaki kujifunza na mnawazuia watu kujifunza.

Usidhani kwa kumkir Mungu tu unaokoka hata ukikosa maarifa na Ukawa na Mungu unaaangamia tu.
Ndioa Maana anasema watu wangu mnaangamia kwa kukosa maarifa.
Ukiona hujanielewa replya hapa nakuja kuwaeleza tena.
 

Na Unaposema asiyeamini amekwisha kuhukumiwa nikwamba mtu hawezi kuamini kile unachoamini wewe bali anapaswa kuamini kile anachoamini yeye.

ndio maana hata Yesu hakuwalazimisha watu wamuamini bali aliwafundisha mambo mema aliwahubiria habari njema watu walipoona huyu mambo anayotufundisha yanauzito ndio wakaanza kumwamini.

na hicho ndicho kilifanya wakristo wengi wazamani wokovu wao kuwa na nguvu sana sababu waliamini kwa kuelewa sio kwakuaminishwa.

Sasa wewe hutaki watu waelewe unataka waaminishwe wapi na wapi?
Mungu mwenyewe anataka uelewe ndipo uamini kwa ridhaa yako sembuse wewe?

kumjua Mungu na Kumuamini Ni Hiari sio Lazima. Ila Ukisha Kumuamini basi tambua kutembea Katika wokovu ndio Lazima usipofanya hivyo unatupwa nje.
Msiongee kwa kukariri mnataka watu wawaambie mwandishi ni nani hakuna jambo kama hilo, ndio maana ninyi wakristo mnakaalia hata kuwaabudu watu walioko israel mkujua yakuwa mnabarikiwa.

]ila Huku Nyuma mnashindwa kutambua nini biblia inasema juu ya Mzaituni Mwitu.

Mnashindwa kutambua Israeli kimaandiko yuko wapi sasa.
bali Mnakaririshwa tu point zisizo na maana na kisha unataka nasisi tukalili kama wewe.

Tutajifunza na Tutaamini kile tulichoelewa pasipo kusukumwa na mtu maana hata siku ya hukumu ni mtu peke yake atajibia wala hatakuwa na wakili.

Jifunze kuongelea imani kwa nafsi yako bali kwa watu wote wanaokuzunguka.
Na kajifunze upya hiyo hukumu ni ipi usije ukaendelea kuzungumza jambo ambalo halipo
 
Sidhani kama umeelewa nilichoandika, nilichoongelea ni kuchunguza iwapo vinatokana na Mungu na iwapo vilishachunguzwa vikaonekana si sawa basi visiwe kipaumbele wakati kuna masuala ya muhimu zaidi.

Nimeona watu wamekuwa posessed na roho za ajabu wakianzia kwenye vitabu vya hivyo wanavyodai vilitolewa kwenye biblia. Sio kila maarifa yatakujenga au yanajenga kiimani, chuja.
 
Hicho kipengele cha Asiyeamini amekwishahukumiwa sijakitunga mimi, kipo ktk biblia.

Yohana 3:18 Amwaminiye yeye hahukumiwi asiyeamini amekwisha kuhukumiwa;kwa sababu hakuliamini jina la mwana pekee wa Mungu.
Anza kusoma yoh 3:16 mpk hapo 18
 
Hicho kipengele cha Asiyeamini amekwishahukumiwa sijakitunga mimi, kipo ktk biblia.
Yohana 3:18 Amwaminiye yeye hahukumiwi asiyeamini amekwisha kuhukumiwa;kwa sababu hakuliamini jina la mwana pekee wa Mungu.
Anza kusoma yoh 3:16 mpk hapo 18
Ndio Maana nasema tunaishi kwa kukariri maandiko andiko likiwa tunajiwekea mipaka ambayo hata Mungu mwenyewe hajaiweka.
Soma yohana Hiyo Hiyo Msaitari wa 36 Unasema Hivi ""Amwaminiye Mwana yuna uzima wamilele; asiyemwamini mwana hataona uzima, bali ghadhabu ya Mungu inamkalia""
Baada ya hapo soma Yohana Hiyo Hiyo 5:24 Unasema hivi ""Amin Amin Nawaambia yeye alisikiaye neno langu na kumwamini yeye aliyenipeleka yuna uzima wamilele; wala haingii hukumuni, bali amepita kutoka mautini kuingia uzimani"

Hilo Neno ulilosema hapa sio mahala pake wala halihusiani kabisa
Kwanini halihusiani nikwasababu Mungu hamkumu mwanadamu kwasasa bali humfundisha na kumuonya na kumtaka arejee kwake hukumuni baada ya kifo tu.

Wanadamu walikuwa wanahukumiwa na Mungu moja kwamoja nikipindi kabla Yesu hajaja kutukomboa yaani unafanya kosa asubuhi jioni unachapwa adhabu zilikuwa ni kupelekwa utumwani, kupigwa mawe hata kufa, kutengwa ama anawaletea maadui mnauliwa vibaya mno.

Sasa jifunze Mungu hawezikukuhukumu kwasasa kwasababu bado neema ipo laiti angekuwa anahukumu basi hii dunia ingejaa watakatifu tu, maana wasiomwamini Yesu wote wangekuwa wapotezwa kiitambo sana.

Sasa ninaposema acha watu wajifunze nina maana hiii hata usiposoma vitabu vya enoch na ukasoma biblia tu napo unaweza ukapotea kiroho vile vile maana neno lina upana na uzito wake vile vile.

Kwahiyo nikumpa tahadhari msomaji tu kuwa anaposoma atumie sana hekima na maarifa ya Mungu kuliko ya kibinaadamu.

maana kadri unavyoidi kukosa maarifa ndivyo unaangamia. Ndio maana tunawalaumu watumishi hawatufundishi vitu vingine lakini kumbe nisisi wavivu wakutafuta maarifa.

Wau wangu wanaangamia kwa kukosa Maarifa.
 
Unapenda kubishana, sioni hoja yako. I agree to disagree tuishie hapo
 
Unapenda kubishana, sioni hoja yako. I agree to disagree tuishie hapo
Ha ha ha ha
Hizo Ni Kauli Za Wajuaji wanaposhindwa kutetea hoja Hakuna Kubishana Hapa tunaeleweshana tu.

Napingana sana na kauli kama hizo zinaonnyesha uchanga wakimawazo maana jambo la kujadiliana halafu mtu unaseama anapenda kubishana ni kauli za ujuaji maana yake lolote utakaloongea likubalike.
hakuna maisha kama hayo face the challenge and be more wisely
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…