Kwanini kitabu cha Enoch kinapingwa vikali na Wanathiolojia?

Kwanini kitabu cha Enoch kinapingwa vikali na Wanathiolojia?

Kuna bonge la kitabu lilitolewa pia lilikuwa linaitwa gospel of Thomas!....... Nafikiri hiki ndo kilikuwa kitabu bora kabisa katika bibilia!.....Sisi wanadamu hasa wa dini ya kikatoliki ni wabaya sana![emoji22]
Katoliki linausikaje hapo, umeshajiuliza kwanini madhehebu yote ya kikristo isipokuwa wakatoliki wanaitwa wa protestant? Hao ndiyo wamevikataa hivyovitabu ,biblia inayotumiwa na wakatolki ina vitabu 72 pamoja na hicho cha Ester ila biblia inayotumiwa na waprotestant inavitabu 66.

Mfano kunakitabu kisuri sana kina mafundisho ya Hekima kinaitwa Yoshua bin Sira kwenye biblia zakiprotestant hakipo.
 
Tanzanians kuna reason kubwa behind theological rejection ya hicho kitabu !!!
That book ukisoma utagundua hakiko consistent with other biblical books kimalize chote utaona matango pori yaliomo humo

By the way wanakitumia Ethiopian Orthodox church tyu
Mkuu Tlg ubarikiwe kwa darasa zuri unalowapa hiki kizazi kinachojifanya kinajua sana kila kitu kuliko watangulizi wao kiimani
 
  • Thanks
Reactions: Tlg
Ni hv kwa kifupi tu huko nyuma kuna tukio kubwa sana lilitokea na hadi leo athari zake zinatawala maisha yetu.tukio hilo ni interaction kati ya binadamu na viumbe fulani wengine wa Mwenyezi Mungu(huwa tunawaita tu malaika hii inatupa upofu sana)walikuwa 200 wakiongozwa na mkuu wao Azazel waliposhuka ktk kilele cha mlima Hermon na kuigiza maumbile ya kibinadamu.kilichowaleta ni kutamani binadamu.walitaka kukaa nao,wawatawale,wazae nao,waanzishe empire yao tofauti na utaratibu waliopangiwa na Mungu.wakafanya hivyo.ikazaliwa offspring ya ajabu,majitu makubwa yenye nguvu za kutisha na akili za ajabu na roho za ajabu maana nusu binadamu nusu malaika.waliitwa nephilims,leo tunawaita titans(usifikiri hadithi ya kigiriki hii)!kutokana na hiyo offspring kuwa imbalance,ilileta vurugu kubwa duniani,na kama Mungu asingeingilia kati mbegu ya binadamu pure ingetoweka.hao malaika pamoja na hayo matoto yao ndio walifundisha binadamu mambo meengi ambayo leo yana sehemu kubwa ktk sayansi,elimu na tamaduni zetu hasa mashariki ya mbali,India na america.base yao kuu ilikuwa bara la Atlantis lililokuwepo katikati ya america na ulaya.kitendo hiki kilimchukiza Mungu mno akaamua kutuma gharika ya maji na kuteketeza dunia nzima pamoja na bara la Atlantis isipokuwa binadamu mmoja anaitwa Nuhu na watoto wake na baadhi ya wanyama ambao hawakuchafuliwa(nephilims walizaana hata na mijusi,kilichotoka hapo ni balaa).LAKINI kuna laana alitamka Mungu,kwamba roho za viumbe hao hataziangamiza,ataziacha na zitakuwa chanzo cha kila uovu duniani kwa umri wote wa dunia hadi mwisho ili viumbe wake wote wapate darasa how serious was this mistake!roho hizo ndizo zilimuongoza Nimrod kuijenga Babylon na kuanzisha idol worshiping na tamaduni za Atlantis zikaanza kurudi taratibu huku spidi yake ikivurugwa na elimu ya dini ya mitume na manabii wa Mungu.ilibidi utaratibu wa kuinteract na binadamu ili kutimiza lengo lao waufanye kwa siri,taratibu,miaka na miaka,wakiibadili dunia taratibu hadi mazingira yakiruhusu,roho hizi zikiwa ndani ya miili ya kibinadamu,zitaigeuza dunia nzima kuwa kama Atlantis!ndipo hapa vyama vya siri na dini zisizoeleweka vinaposhamiri underground.
Ndugu Yangu Umechambua Vzr Sana Mpaka Nimefarijika Kiukweri Yani Respect
 
Ndugu Yangu Umechambua Vzr Sana Mpaka Nimefarijika Kiukweri Yani Respect
Mkuu hicho kitabu kimewekwa humu ni vzuri ukisome chote kabla hujafanya conclusion.... Ukisubiri wakuchambulie utalishwa matango pori

Mfano hiyo Atlantis wanasema imezama ila ukiwauliza mabaki hata ya miamba ya huo mji yakwapi hawajui ilihali bara lililozama likazaa kisiwa cha borneo na sumatra mpaka leo lipo huko asia ya kusini hadi australia

Kwa ufupi Atlantis ilitumika kwenye hadithi za plato na kitabu chake cha republic kma mfano wa nchi PERFECT ambayo inatakiwa viongozi wote wa dunia wafuate mfano wa nchi ile zaidi ya hapo watu wanatunga mambo kuwa hilo bara lilikuwepo ila ushahidi haupo
 
Shukran sana mkuu kwa kunileta huku....

Mkuu,unajua kuna mambo hata huwezi kusema unajikuta unabaki nayo wewe mwenyewe tu huku ukijiuliza mambo mengi sana.Siyo kila kitu ni cha kusema kila mahali maana unaweza kujikuta watu wanaanza kukuchukulia wa ajabu sana na pengine wanaanza kuhisi labda una shida upstairs kumbe siyo.....

Niliwahi,na bado nina hisia hasi sana kuhusu watu weupe na chanzo au asili yao.Niliwahi kumuambia mtu mmoja tena ni memba wa hapa JF kwamba niliwahi kujiuliza sana kati ya mtu mweusi na mweupe ni nani aliyepungua,yaani ni yupi anaonekana ana "mapungufu"...

Nilipokuja kukumbana na ishu ya melanin hapo ndipo nikaanza kupata ka picha kadogo sana kwa mbaaali....

Mkuu,kuna mambo ya kutisha sana huko sirini na kuna makundi makubwa makubwa sana yanayoheshimika sana mbele za watu yamehusika na ufichaji huu wa kutisha sana wa mambo haya,good thing ni kwamba BWANA WA MABWANA alisema "hakuna kilicjho sirini ambacho hakitafichuliwa" na leo hapa tunajadili mambo ambayo kuna watu hata hawapiti kusoma maana wanaona ni upuuzi....

Niliwahi kusema na ninasema tena,ogopa sana mambo yanayoonwa ni ya kipuuzi kama haya maana yamebeba ukweli mwingi sana tena sana.....

Huwa tunaangalia movie kama movie tu lakini hawa "wajinga" huwa wanapitisha humo ujumbe wao wa kweli na yale wanayoyapanga.tatizo moja kubwa la ukweli ni kwamba uko mama moto,utauficha sana lakini moshi utakukereketa na utatoka tu,ukweli upo hivyo,utakusumbua sana lakini utausema hata kwa namna nyingine na wao wanasema sana kupitia movie.....

Hivi ni kwanini kwa mfano kwenye Movie ya Babylon A.D aliyocheza Vin Diesel amevaa t-shirt imeandikwa Afreeca mwanzoni tu inapoanza,tena ni nyeusi?

Ni kwanini jina la Movie linaonekana baana ya kuonekana "Statue of Liberty"? Unajua hiyo sanamu ni ya nani?

Mkuu,nataka nikupe ushauri ambao utakuja kushangaa sana na pengine utatoa machozi siku zijazo kama tutajaaliwa uzima,anza kuangalia movie kwa mtazamo mwingine kabisa na soma sana habari za "siri" utakuja kuniambia kitu.....

Ninaandika haya nikiwa na hzuni sana maana wengi wanadharau sana mambo haya lakini iko siku watalia na kusaga meno.Tunapenda sana kudharau yanayodharaulika,ni nani anaweza kufikiria kuwa kichaa huwa ni mpelezi wakati mwingine?

Mkuu,wewe na mimi tuna nafasi moja muhimu sana hapa duniani.Waangalie Wabantu wote duniani na uwaache kama walivyo,iko siku utaelewa ni kwanini.....

Nakuomba mkuu uwe mpole tu.....
Chief Umeongea Kwa Hisia Mpaka Moyo wangu umepata Tetemeko La Mwili

Inaonekana Una Mengi Sana Moyo Mwako Ambayo Binadam wengine Unaweza Kushare Nao Hayo Mambo Mazur uliyo Nayo
 
Mkuu,ndiyo maana nasema kwamba kuna mambo ukisema yana madhara.Sizungumzii madhara ya kimwili lakini kwa watu ambao wanakuwa wanakutazama kwa namna fulani hivi wataanza kuhisi labda una matatizo....

Taratibu tutakuwa tunaelezana tu.Siku moja mwaka 2011 nilimueleza bro wangu mmoja kuhusu uwepo wa mambo yanayofichwa na yanayofanywa na aina fulani ya watu wasiofahamika na wengi.Bro wangu huyu aliniangalia kisha akatikisa kichwa kuonesha amenisikia,lakini sikujua kuwa alikuwa ameanza kuhisi nina shida kichwani hadi alipokuja kupata ushahidi wa niliyomwambia halafu akaja kuniambia ukweli wa namna alivyoniona.....

Tangu siku hiyo nimekuwa makini sana kusema sema mambo hovyo maana unaweza kujikuta unaharibu mahusiano yako na watu bila sababu ya msingi maana mtu ataanza kuhisi labda unavuta bangi au una shida fulani za kufanana na hizo na akaanza kukukwepa.....

Ninakuwa mpole na taratibu tutakuwa tunaambizana yale yalayotustahili mkuu....
Naammm Hapo Nimekuelewa Sana
 
Yaani tu kwa mfano....

"Sisi" tuna mamlaka gani hapa duniani?

Wanaoweza kuamua ni kitabu kipi kiwepo kwenye maandiko yatakayoitwa matakatifu ni Papa,mkuu wa makanisa ya Anglikana,KKKT na makanisa mengine,makanisa yote haya wakuu wake ni Wazungu na hawapo hapa Afrika wapo huko,na hawa ndiyo hatari sana kwa usalama wa imani zetu.....

Wanaoweza kukubali kwamba jambo fulani la kiekolojia na tutakubali kwa shangwe ni hao hao Wazungu..

Wanoweza kukubali suala fulani ni hatari kwa afya na tutakubali kwa shangwe ni WHO,hawapo hapa Afrika...

Wanaoweza kukubali kuwa kuna maradhi yasiyotibika na tutakubali kwa shangwe ni hao hao...

Wanoweza kusema jambo fulani lina ushahidi kisayansina tukakubali kwa shangwe ni hao hao....

Wanaoweza kusema kusema kuwa angali kuna nini na tukakubali kwa shangwe ni hao hao....

Wanaoweza kusema jambo na likakubalika na tukasema "lina ushahidi" ni hao hao.....

Hawa hawa ambao tumewapa mamlaka yote haya kwenye maisha yetu ndiyo hao hao ambao wamekuwa wakitumaliza sana kwa kila takataka za sumu na bado tunaona sawa tu.Yaani sisi ni misukule haswa....

Leo wanatuambia tena huku wakituona ni wapuuzi wa kutupwa kuwa eti ushoga ni suala la kimaumbile tunashangilia tu....

Sisi tuko wapi? Tunaamua wapi na kwenye nini na kitu gani?
Chief Ninakufatilika Kwa Umakin Mkubwa Sana Tafadhari Mwaga Data Za Kutosha Mungu Atakulinda Na Kukupa Afya Njema
 
Mchango tu:

Kosa la kwanza ni 'kumtafuta mungu wa kweli' wakati ni suala la imani.

Kosa la pili ni kudhani unaweza kuja kupata jibu hilo.

Unajua kwa nini?
Kwa sababu mungu wa kweli yukoje?
Yaan utajuaje mungu ni nani... Yupo katika form ipi... Kama huamini unadhani 'utamwona'?

Binafsi, Mungu ni Mungu.
Sina namna ya kum-describe kwa sababu yeye ni Mungu na sijawahi kumuona Mungu kabla...

Hata kama umeambiwa umeumbwa kwa mfano wake, haimaanishi moja kwa moja ni muonekano... Hiyo ni just lost in translation. Mfano wake inaweza kuwa katika intelligence, au reasoning au ethics, etc. Kwa sababu those things are what makes us unique.

Nashauri tusome vitabu vyote hata vilivyokuwa removed, maana hekima inakuja baada ya 'kujua yote'.
 
Daaa Asante sana kaka kwa kunikumbuka

Sema niseme machache tu, watu wanauchukia ukweli na hawapendi kuujua ukweli, la msingi niseme hivi miongoni mwa watu walioishi masha ya kumjua na kutembea katika njia za Mungu Enoch ni mmoja wapo na katika biblia watu ambao wameenda Mbinguni pasipo kuonja mauti Enock ni mmoja wapo Genesis 5:24
Naongeza pia uzito huu Enoch is described as a man who "walked with God for 300 years" (Genesis 5:23)
Sasa inakuwa ni ajabu leo mtu aliyeishi maisha ya Kumtegemea Mungu siku zote na kisha Kazi zake zikapingwa.
Wahubiri ni kama wanawapa limbwata waumini ili wasielewe,
Ila kupitia hapo tuu jiulize
Mfano leo kazi za petro zifutwe zote inakuja kweli?
Sasa wanachukuliwa wepesi wepesi tu labda kwasababu hawajajua relation ya kitabu husika na biblia nadhani sababu wanakisikia kwa masimulizi pasipo kukisoma.
Ndio Maana Mungu anasema tunaangamia kwa kukosa maarifa,
Hasemi tunaangamia kwa kukosa ulinzi wake la hasha kwa kukosa maarifa.
Una uhakika gani kiliandikwa na Enoch yule yule bwana? Hata akina sauli tu walikuwa wawili zama tofauti una uhakika gani enoch ni mmoja tu? Kuna uwezekano kuna maandiko yaliyopotoka maana pia kuna vitabu vinaitwa vya musa na vinatumiwa na wachawi na secret societies.

Tumeambiwa tuchunguze roho hizo iwapo zinatoka kwa Mungu, na tunawatambuaje wasiotoka kwa Mungu au visivyo toka kwa Mungu ... NI KWA MATUNDA YAO kama andiko linaleta uchonganishi na kuchanganyikiwa mjiulize mara mbili iwapo kweli ni andiko lililoletwa kwa roho mtakatifu.

Inasemekana baadhi ya maandiko ya hicho kitabu cha Enoch yanasuggest wazungu ni uzao wa malaika wabaya na binadamu, ili iweje labda kwa wakati huu ambao we have more pressing matters like the second coming of Jesus Christ[emoji53].
Tusipotezewe muda na vitabu vilivyoondolewa maana kuna hekima pia iliyotumika na inawezekana ndio mbinu za kuleta kutoamini miongoni mwa waumini na mara paap Yesu huyu hapa, KUMBUKA MAANDIKO "ASIYEAMINI AMEKWISHA KUHUKUMIWA..."
 
Mchango tu:

Kosa la kwanza ni 'kumtafuta mungu wa kweli' wakati ni suala la imani.

Kosa la pili ni kudhani unaweza kuja kupata jibu hilo.

Unajua kwa nini?
Kwa sababu mungu wa kweli yukoje?
Yaan utajuaje mungu ni nani... Yupo katika form ipi... Kama huamini unadhani 'utamwona'?

Binafsi, Mungu ni Mungu.
Sina namna ya kum-describe kwa sababu yeye ni Mungu na sijawahi kumuona Mungu kabla...

Hata kama umeambiwa umeumbwa kwa mfano wake, haimaanishi moja kwa moja ni muonekano... Hiyo ni just lost in translation. Mfano wake inaweza kuwa katika intelligence, au reasoning au ethics, etc. Kwa sababu those things are what makes us unique.

Nashauri tusome vitabu vyote hata vilivyokuwa removed, maana hekima inakuja baada ya 'kujua yote'.
Iyo Paragraph Ya Mwisho Nimeielewa Zaid Chief
 
Una uhakika gani kiliandikwa na Enoch yule yule bwana? Hata akina sauli tu walikuwa wawili zama tofauti una uhakika gani enoch ni mmoja tu? Kuna uwezekano kuna maandiko yaliyopotoka maana pia kuna vitabu vinaitwa vya musa na vinatumiwa na wachawi na secret societies. Tumeambiwa tuchunguze roho hizo iwapo zinatoka kwa Mungu, na tunawatambuaje wasiotoka kwa Mungu au visivyo toka kwa Mungu ... NI KWA MATUNDA YAO kama andiko linaleta uchonganishi na kuchanganyikiwa mjiulize mara mbili iwapo kweli ni andiko lililoletwa kwa roho mtakatifu.
Inasemekana baadhi ya maandiko ya hicho kitabu cha Enoch yanasuggest wazungu ni uzao wa malaika wabaya na binadamu, ili iweje labda kwa wakati huu ambao we have more pressing matters like the second coming of Jesus Christ[emoji53].
Tusipotezewe muda na vitabu vilivyoondolewa maana kuna hekima pia iliyotumika na inawezekana ndio mbinu za kuleta kutoamini miongoni mwa waumini na mara paap Yesu huyu hapa, KUMBUKA MAANDIKO "ASIYEAMINI AMEKWISHA KUHUKUMIWA..."

Kuna Vitu huwa tunajipa vichwa ngumu sana kama mtu unaweza kuchanganyikiwa basi utachanganyikiwa tu
na kama umeona kuna mkanganyiko nakuomba usije jaribu kitu hiki cha kusoma biblia iliyoandikwa kwa kiingereza na ukaufuata msitari huo huo katika kiswahili.

Kwa kufanya uchunguzi kama huo imenisaidia kuelewa sana neno tofauti na nilivyokuwa mwanzo

Kuna mahali ukisoma katika kiswahili unakuta kabisa maana imepotea ama inapungua ukisoma katika kiingereza unakuta kile kitu kipo full kabisa.

Mfano mzuri chukua bible yako soma isaya 60 then anza kulinganisha na bible ya kiingereza hapo sasa ndio utajua Neno La Mungu linakaa moyoni wala sio kitabuni.

Kusoma vitabu vilivyoondolewa katika biblia na kujua sababu inatukomaza kiroho pia.

nakumbuka hapa kunawengine wanasomakwasababu wanahitaji wakafundishe wengine, wengine wanasoma kama burudani,wengine wanasoma kwasababu mtumishi anawashauri wasome neno la Mungu.
Hata biblia yenyewe inamikanganyiko usipokuwa makini kwahiyo suala la kuzuia mtu kusoma sio tatizo.

Ndio maana hata ukisoma Biblia haisemi uwe unasoma Biblia inasema Usome Neno.

Neno halikai katika maandishi neno Linakaa Moyoni mwako ndio maana Biblia anaweza kuibeba hata mchawi ama mtenda dhambi na asidhurike lakini mtenda dhambi na ama mchawi hawezi kumgusa mtu aliye na neno la Mungu.

Ndio Maana wakristo waleo mnapata shida sana mtu akikwambia thibitisha kwa Mungu yupo mnakuwa mnatoa mirejeo isiyokuwa na mantiki kwasababu hamtaki kujifunza na mnawazuia watu kujifunza.

Usidhani kwa kumkir Mungu tu unaokoka hata ukikosa maarifa na Ukawa na Mungu unaaangamia tu.
Ndioa Maana anasema watu wangu mnaangamia kwa kukosa maarifa.
Ukiona hujanielewa replya hapa nakuja kuwaeleza tena.
 
Na Unaposema asiyeamini amekwisha kuhukumiwa nikwamba mtu hawezi kuamini kile unachoamini wewe bali anapaswa kuamini kile anachoamini yeye.

ndio maana hata Yesu hakuwalazimisha watu wamuamini bali aliwafundisha mambo mema aliwahubiria habari njema watu walipoona huyu mambo anayotufundisha yanauzito ndio wakaanza kumwamini.

na hicho ndicho kilifanya wakristo wengi wazamani wokovu wao kuwa na nguvu sana sababu waliamini kwa kuelewa sio kwakuaminishwa.

Sasa wewe hutaki watu waelewe unataka waaminishwe wapi na wapi?
Mungu mwenyewe anataka uelewe ndipo uamini kwa ridhaa yako sembuse wewe?

kumjua Mungu na Kumuamini Ni Hiari sio Lazima. Ila Ukisha Kumuamini basi tambua kutembea Katika wokovu ndio Lazima usipofanya hivyo unatupwa nje.
Msiongee kwa kukariri mnataka watu wawaambie mwandishi ni nani hakuna jambo kama hilo, ndio maana ninyi wakristo mnakaalia hata kuwaabudu watu walioko israel mkujua yakuwa mnabarikiwa.

]ila Huku Nyuma mnashindwa kutambua nini biblia inasema juu ya Mzaituni Mwitu.

Mnashindwa kutambua Israeli kimaandiko yuko wapi sasa.
bali Mnakaririshwa tu point zisizo na maana na kisha unataka nasisi tukalili kama wewe.

Tutajifunza na Tutaamini kile tulichoelewa pasipo kusukumwa na mtu maana hata siku ya hukumu ni mtu peke yake atajibia wala hatakuwa na wakili.

Jifunze kuongelea imani kwa nafsi yako bali kwa watu wote wanaokuzunguka.
Na kajifunze upya hiyo hukumu ni ipi usije ukaendelea kuzungumza jambo ambalo halipo
 
Sidhani kama umeelewa nilichoandika, nilichoongelea ni kuchunguza iwapo vinatokana na Mungu na iwapo vilishachunguzwa vikaonekana si sawa basi visiwe kipaumbele wakati kuna masuala ya muhimu zaidi.

Nimeona watu wamekuwa posessed na roho za ajabu wakianzia kwenye vitabu vya hivyo wanavyodai vilitolewa kwenye biblia. Sio kila maarifa yatakujenga au yanajenga kiimani, chuja.
 
Na Unaposema asiyeamini amekwisha kuhukumiwa nikwamba mtu hawezi kuamini kile unachoamini wewe bali anapaswa kuamini kile anachoamini yeye.
ndio maana hata Yesu hakuwalazimisha watu wamuamini bali aliwafundisha mambo mema aliwahubiria habari njema watu walipoona huyu mambo anayotufundisha yanauzito ndio wakaanza kumwamini.
na hicho ndicho kilifanya wakristo wengi wazamani wokovu wao kuwa na nguvu sana sababu waliamini kwa kuelewa sio kwakuaminishwa.
Sasa wewe hutaki watu waelewe unataka waaminishwe wapi na wapi?
Mungu mwenyewe anataka uelewe ndipo uamini kwa ridhaa yako sembuse wewe?
kumjua Mungu na Kumuamini Ni Hiari sio Lazima.
Ila Ukisha Kumuamini basi tambua kutembea Katika wokovu ndio Lazima usipofanya hivyo unatupwa nje.
Msiongee kwa kukariri mnataka watu wawaambie mwandishi ni nani hakuna jambo kama hilo, ndio maana ninyi wakristo mnakaalia hata kuwaabudu watu walioko israel mkujua yakuwa mnabarikiwa.
]ila Huku Nyuma mnashindwa kutambua nini biblia inasema juu ya Mzaituni Mwitu.
Mnashindwa kutambua Israeli kimaandiko yuko wapi sasa.
bali Mnakaririshwa tu point zisizo na maana na kisha unataka nasisi tukalili kama wewe.
Tutajifunza na Tutaamini kile tulichoelewa pasipo kusukumwa na mtu maana hata siku ya hukumu ni mtu peke yake atajibia wala hatakuwa na wakili.
Jifunze kuongelea imani kwa nafsi yako bali kwa watu wote wanaokuzunguka.
Na kajifunze upya hiyo hukumu ni ipi usije ukaendelea kuzungumza jambo ambalo halipo
Hicho kipengele cha Asiyeamini amekwishahukumiwa sijakitunga mimi, kipo ktk biblia.

Yohana 3:18 Amwaminiye yeye hahukumiwi asiyeamini amekwisha kuhukumiwa;kwa sababu hakuliamini jina la mwana pekee wa Mungu.
Anza kusoma yoh 3:16 mpk hapo 18
 
Ndio Maana nasema tunaishi kwa kukariri maandiko andiko likiwa tunajiwekea mipaka ambayo hata Mungu mwenyewe hajaiweka.
Soma yohana Hiyo Hiyo Msaitari wa 36 Unasema Hivi ""Amwaminiye Mwana yuna uzima wamilele; asiyemwamini mwana hataona uzima, bali ghadhabu ya Mungu inamkalia""
Baada ya hapo soma Yohana Hiyo Hiyo 5:24 Unasema hivi ""Amin Amin Nawaambia yeye alisikiaye neno langu na kumwamini yeye aliyenipeleka yuna uzima wamilele; wala haingii hukumuni, bali amepita kutoka mautini kuingia uzimani"

Hilo Neno ulilosema hapa sio mahala pake wala halihusiani kabisa
Kwanini halihusiani nikwasababu Mungu hamkumu mwanadamu kwasasa bali humfundisha na kumuonya na kumtaka arejee kwake hukumuni baada ya kifo tu.

Wanadamu walikuwa wanahukumiwa na Mungu moja kwamoja nikipindi kabla Yesu hajaja kutukomboa yaani unafanya kosa asubuhi jioni unachapwa adhabu zilikuwa ni kupelekwa utumwani, kupigwa mawe hata kufa, kutengwa ama anawaletea maadui mnauliwa vibaya mno.

Sasa jifunze Mungu hawezikukuhukumu kwasasa kwasababu bado neema ipo laiti angekuwa anahukumu basi hii dunia ingejaa watakatifu tu, maana wasiomwamini Yesu wote wangekuwa wapotezwa kiitambo sana.

Sasa ninaposema acha watu wajifunze nina maana hiii hata usiposoma vitabu vya enoch na ukasoma biblia tu napo unaweza ukapotea kiroho vile vile maana neno lina upana na uzito wake vile vile.

Kwahiyo nikumpa tahadhari msomaji tu kuwa anaposoma atumie sana hekima na maarifa ya Mungu kuliko ya kibinaadamu.

maana kadri unavyoidi kukosa maarifa ndivyo unaangamia. Ndio maana tunawalaumu watumishi hawatufundishi vitu vingine lakini kumbe nisisi wavivu wakutafuta maarifa.

Wau wangu wanaangamia kwa kukosa Maarifa.
 
Ndio Maana nasema tunaishi kwa kukariri maandiko andiko likiwa tunajiwekea mipaka ambayo hata Mungu mwenyewe hajaiweka.
Soma yohana Hiyo Hiyo Msaitari wa 36 Unasema Hivi ""Amwaminiye Mwana yuna uzima wamilele; asiyemwamini mwana hataona uzima, bali ghadhabu ya Mungu inamkalia""
Baada ya hapo soma Yohana Hiyo Hiyo 5:24 Unasema hivi ""Amin Amin Nawaambia yeye alisikiaye neno langu na kumwamini yeye aliyenipeleka yuna uzima wamilele; wala haingii hukumuni, bali amepita kutoka mautini kuingia uzimani""
Hilo Neno ulilosema hapa sio mahala pake wala halihusiani kabisa
Kwanini halihusiani nikwasababu Mungu hamkumu mwanadamu kwasasa bali humfundisha na kumuonya na kumtaka arejee kwake hukumuni baada ya kifo tu.
Wanadamu walikuwa wanahukumiwa na Mungu moja kwamoja nikipindi kabla Yesu hajaja kutukomboa yaani unafanya kosa asubuhi jioni unachapwa adhabu zilikuwa ni kupelekwa utumwani,kupigwa mawe hata kufa, kutengwa ama anawaletea maadui mnauliwa vibaya mno.
Sasa jifunze Mungu hawezikukuhukumu kwasasa kwasababu bado neema ipo laiti angekuwa anahukumu basi hii dunia ingejaa watakatifu tu, maana wasiomwamini Yesu wote wangekuwa wapotezwa kiitambo sana.
Sasa ninaposema acha watu wajifunze nina maana hiii hata usiposoma vitabu vya enoch na ukasoma biblia tu napo unaweza ukapotea kiroho vile vile maana neno lina upana na uzito wake vile vile.
Kwahiyo nikumpa tahadhari msomaji tu kuwa anaposoma atumie sana hekima na maarifa ya Mungu kuliko ya kibinaadamu.
maana kadri unavyoidi kukosa maarifa ndivyo unaangamia.
Ndio maana tunawalaumu watumishi hawatufundishi vitu vingine lakini kumbe nisisi wavivu wakutafuta maarifa.
Wau wangu wanaangamia kwa kukosa Maarifa.
Unapenda kubishana, sioni hoja yako. I agree to disagree tuishie hapo
 
Unapenda kubishana, sioni hoja yako. I agree to disagree tuishie hapo
Ha ha ha ha
Hizo Ni Kauli Za Wajuaji wanaposhindwa kutetea hoja Hakuna Kubishana Hapa tunaeleweshana tu.

Napingana sana na kauli kama hizo zinaonnyesha uchanga wakimawazo maana jambo la kujadiliana halafu mtu unaseama anapenda kubishana ni kauli za ujuaji maana yake lolote utakaloongea likubalike.
hakuna maisha kama hayo face the challenge and be more wisely
 
Back
Top Bottom