Kwanini kodi ya gari la miaka ya karibuni iko juu sana

N'yadikwa

JF-Expert Member
Joined
Aug 10, 2014
Posts
7,427
Reaction score
10,905
Yaani ukiagiza Japan gari la Miaka ya 1990's ushuru wa TRA upo chini. Ila ukijiroga uagize gari la miaka ya 2010's utafurahi na roho yako jinsi ushuru wa TRA ulivyo juu.

Unakaa unajiuliza hivi hii nchi kuna mtu ana roho ya korosho hataki watanzania waendeshe magari mazuri?

Nani anafanya hivi. Na kwa maslahi ya nani?!

Inaudhi sana!

MY TAKE
Tuendelee tu hivihivi. Ili sisi wenye hela tuendeshe magari mazuri na wakata ufuta waendelee kuendesha mikweche. Kenya Hoiyee.
 
Mibunge yako iliyojaa mishavu mikubwa kama imemeza vyura ndiyo inayopitishaga sheria hizo za Kodi za kumuumiza mtanzania!,TRA wao wanasimamia sheria ya kodi iliyotungwa na Mibunge yako isiyokuwa na huruma kwa Mtanzania!
 
Lete mfano!
 
Mibunge yako iliyojaa mishavu mikubwa kama imemeza vyura ndiyo inayopitishaga sheria hizo za Kodi za kumuumiza mtanzania!,TRA wao wanasimamia sheria ya kodi iliyotungwa na Mibunge yako isiyokuwa na huruma kwa Mtanzania!
Mbona umekuwa too personal mkuu. Are you meant to attack my personality? Mimi mleta sledi?
 
Hopefully watakuwa wamepewa hela na wazungu ili takataka zipunguue huko kwao ndo wakaset mitambo ya kodi
Unajua aina hii ya ushuru ndiyo inaruhusu chuma chakavu kujaa nchini. Factor ya kikokotozi ipo kwenye CIF pricing kwa vile taxman anavyoperceive, very naniliii yaanii
 
Mibunge yako iliyojaa mishavu mikubwa kama imemeza vyura ndiyo inayopitishaga sheria hizo za Kodi za kumuumiza mtanzania!,TRA wao wanasimamia sheria ya kodi iliyotungwa na Mibunge yako isiyokuwa na huruma kwa Mtanzania!
Wabunge wengi elimu ya darasani hawana ya kutosha, wanatunga sheria ambazo wasomi walio kwenye mataasisi wanazifuata
 
Kiuhalisia gari new models zinapendezesha jiji, Kwa kuwa new models zina gharama hata kama ni used basi serikali ingeweka kodi chini kuweza ku balance.

Gari kali ni mapambo mjini, sijui shida serikali bado kuna vikongwe wanafikiri gari ni anasa, mbona wao hawatumii Land Cruisers za 1990's or early 2000's.

Tunakuwa na jiji lina barabara nzuri halafu magari yamejaa ni ya 1990's.

Kwanza gari nyingi za zamani leo hii nchi zilizoendelea zimepiga marufuku ziwe discontinued kwa sababu zinachangia pakubwa uchafuzi wa hali ya hewa.
 
Kwa hiyo wameamua nchi yetu iwe dampo ,
 
Ukifika Nairobi, au Kigali mji ni msafi hata magari yanavutia huoni mioshi au chuma chakavu road. Bongo kumiliki gari ya 2010s ni anasa. Nairobi unakutana na Isuzu FTR au FSR zimebeba mzigo saaafi na hizo ni gari zimekuwa assembled hapohapo Kenya. Sisi huku unakutana na Isuzu Injection za wakati wa Uhuru, jamaa wanaimba 'toa taka, toa taka'.

Huku unakutana na baadhi ya magari barabarani unaweza kudhani kichaka kinawaka moto, kumbe ni gari linaenda, ukikosea kuovateki yanakukuta ya ajali mbaya ya 'Usichezee Shilingi Chooni' Iringa miaka ile.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…