Kwanini kodi ya gari la miaka ya karibuni iko juu sana

Kwanini kodi ya gari la miaka ya karibuni iko juu sana

Ukifika Nairobi, au Kigali mji ni msafi hata magari yanavutia huoni mioshi au chuma chakavu road. Bongo kumiliki gari ya 2010s ni anasa.
Ni kweli kabisa, si majengo tu na barabara zinazofanya mji upendeze, gari mpya za kisasa zinapendezesha sana mji hata kwa wageni wakifika wanavutiwa.
 
Ni kweli kabisa, si majengo tu na barabara zinazofanya mji upendeze, gari mpya za kisasa zinapendezesha sana mji hata kwa wageni wakifika wanavutiwa.
Sasa bongo hata uzunguke Temeke,Ubungo,Kinondoni Kigamboni hadi masaki kukutana na Toyota Crown ya 2017 ni nadra, gari Japan au Singapore wanaiuza USD 8,000 ushuru taxman wa Bongo kakadiria USD 14,000. Acha tusukume Escudo zetu 1st generation kyakyakya
 
Hopefully watakuwa wamepewa hela na wazungu ili takataka zipunguue huko kwao ndo wakaset mitambo ya kodi
Hizi fikra kuna wakati huwa nakuwa nazo kwamba huenda WAMEHONGWA ili chuma chakavu zije huku Tanzania.

Sheria irekebishwe iwe marufuku kuja huku gari yenye umri zaidi ya miaka 10.
 
Na kwa kuzingatia kwamba mabarabara sasa yanatanuliwa. Nikiamini kutoka Bandarini Dar es Salaam hadi Tunduma, Namanga na Rusumo barabara zitakuwa nne nne, ni wakati sasa tukawa na magari latest/ya kisasa sio hii mikweche Isuzu Injection nakadhalika.

Watunga Sheria hembu fanyeni jambo pale Bungeni mtusaidie tupate Sheria inayoleta nafuu kwa Watanzania kununua magari ya kisasa.

Hapa Tanzania hata gari za mizigo (ambazo ni muhimu sana kuendesha uchumi wa watu) mathalani hizi Mitsubishi Canter au Toyota Coaster barabarani nyingi ni za early 2,000s au late 1990's. Kwanini!? Kwa sababu Ukijiroga ukaagiza Coaster Mayai kama ile inayobeba Watumishi wa BOT bei yake ni Mamia ya Mamilioni ya Tsh.

Kuagiza Lori la Howo la Mchina ambalo Mchina analiuza very cheap ushuru wake ni wa kufa mtu.

Hembu tutoke hapa. Tujenge hii nchi jamani
 
Yaani ukiagiza Japan gari la Miaka ya 1990's ushuru wa TRA upo chini. Ila ukijiroga uagize gari la miaka ya 2010's utafurahi na roho yako jinsi ushuru wa TRA ulivyo juu.

Unakaa unajiuliza hivi hii nchi kuna mtu ana roho ya korosho hataki watanzania waendeshe magari mazuri?

Nani anafanya hivi. Na kwa maslahi ya nani?!

Inaudhi sana!

MY TAKE
Tuendelee tu hivihivi. Ili sisi wenye hela tuendeshe magari mazuri na wakata ufuta waendelee kuendesha mikweche. Kenya Hoiyee.
Huoni gari la mwaka 1990 ni la zamani na gari la mwaka 2010 ni la kisasa zaidi?
 
Kiuhalisia gari new models zinapendezesha jiji, Kwa kuwa new models zina gharama hata kama ni used basi serikali ingeweka kodi chini kuweza ku balance.

Gari kali ni mapambo mjini, sijui shida serikali bado kuna vikongwe wanafikiri gari ni anasa, mbona wao hawatumii Land Cruisers za 1990's or early 2000's.

Tunakuwa na jiji lina barabara nzuri halafu magari yamejaa ni ya 1990's.

Kwanza gari nyingi za zamani leo hii nchi zilizoendelea zimepiga marufuku ziwe discontinued kwa sababu zinachangia pakubwa uchafuzi wa hali ya hewa.
Wajapan wakija huku Tanzania wanaona kama wapo nyuma miaka 25 iliyopita. Gari zetu nyingi ni za mwaka 2000-2006.

Nahisi huwa wanacheka sana. Wenzetu kenya ni tofauti aisee..vyuma chakavu washavikataa kitambo
 
Wajapan wakija huku Tanzania wanaona kama wapo nyuma miaka 25 iliyopita. Gari zetu nyingi ni za mwaka 2000-2006.

Nahisi huwa wanacheka sana. Wenzetu kenya ni tofauti aisee..vyuma chakavu washavikataa kitambo
Inatakiwa nasi tuchukue hatua. Shida ni political will ipo?
 
Ukiachana na mwaka wa zamani kuwa na ushuru kidogo lakini pia kuna Pickup, lorries na the likes ambazo ni muhimu kwenye shughuli za kijamii unakuta ushuru ni mkubwa ajabu. Serikali inajukumu la kutusaidie tuishi maisha ya first world. Waache kuangalia kodi ambayo inazuia watu kuishi maisha ya dunia ya kwanza.
 
Kuna kiwanda cha kuunga magari kinazinfuliwa hapa leo na Raisi, muwekezaji anamuomba raisi magari yanayoagizwa nje yaongezewe kodi ili kulinda kiwanda hiki
 
Back
Top Bottom