Kwanini kupata mtoto mwenye ulemavu wa akili, viungo, kipofu, bubu, kiziwi, n.k ni aibu na fedheha kwa wazazi wengi?

Kwanini kupata mtoto mwenye ulemavu wa akili, viungo, kipofu, bubu, kiziwi, n.k ni aibu na fedheha kwa wazazi wengi?

sky soldier

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2020
Posts
5,407
Reaction score
19,264
Nasema hivi maana mambo ya aibu ndio huwa tuanakazania kuyaficha na ndivyo ilivyo kwa wazazi wenye hawa watoto huwa hawapendi watoto wao wenye ulemavu kujulikana ni watoto wao, wanawafungia majumbani huku wakijificha nyuma ya kivuli cha kuwalinda.

yani mtoto anachukuliwa kama mzigo flani hivi, niliwahi kushuhudia laivu bila chenga hospitali flani mtoto kazaliwa na ulemavu wa ngozi, baba wa mtoto alikana mtoto huyo sio wake na ndio ukawa mwisho wa mahusiano na mzazi mwenzake.
 
Nasema hivi maana mambo ya aibu ndio huwa tyanakazaniwa kufichwa na ndivyo ilivyo kwa wazazi wenye hawa watoto whuwa hawapendi watoto wao wnye ulemavu kyjuikana ni watoto wao, wanawafungia majumbani huku wakkijificha nyuma ya kivuli cha kuwalinda...
Wewe mwenyewe binafsi Mungu Mwenyezi akikuchunuku mtoto mlemavu utajisikiaje?

Kuna mambo binadamu huyapokea kwa shingo upande kwa kuwa hawana namna ya kuyabadilisha.

Hakuna mzazi anayefurahi kuzaa kilema isipokuwa kulipokea jambo hilo kwa sababu hakuna namna, limetokea!

Baada ya kuzaa mlemavu, familia inatakiwa ibadilishe saikolojia na kumkubali na kumpenda mtoto wao huyo kwa kuwa Mungu anakuwa kaamua na dunia hairudi reverse!

Kumficha ficha ni ishara ya kumkataa na kumtenga.

Matendo ya namna hiyo baadaye huleta laana kwa wazazi kwa majaribu ambayo wazazi wanakuwa wamepewa na M/Mungu.
 
bahati nzuri feeling siyo kosa kosa ni matendo baada ya mihemiko. Hata Mimi nikipata watoto hivyo nita feel bad lakini itabidi niwatendee matendo ambayo yapo against na feeling zangu. Nitawafanya wawe na furaha na amani ni wasijute kuzaliwa.
 
Watanzania tulio wengi tunatazama watoto wetu kama wakombozi wetu kipindi tutakapokuwa hatuna nguvu za kujitafutia.....ndio maana wazazi wanafanya uwekezaji kwa watoto wao huku wakitarajia mafanikio ya watoto wao ndio mafanikio yao.

Hali inakuwa tofauti akizaliwa mtoto ambaye ni mlemavu awe wa akili au viungo. Kuna asilimia kubwa sana ya mtoto huyo kuwa tegemezi kwako mpaka KABURINI kinyume na matarajio ya wazazi na walezi wengi.

Hii inatokana na mifumo mingi ya kiserikali na kijamii kwa ujumla kuwatenga walemavu kiutendaji na kiuwajibikaji, bado kuna walemavu Wana elimu nzuri lakini hawapati fursa za ajira kama wasiokuwa walemavu.

Serikali inatakiwa kuliangalia hili kisera na kiuwajibikaji kwa kuwa kiuhalisia sisi sote ni walemavu watarajiwa.
 
Weka hali yako kama hivi, umepanga kwenda kuishi South Africa maisha yako yaliyobaki, umefunga mizigo yako, unafika airport ndege inayokwenda South Africa inawasili. Unaingia unapata kiti, mnafunga mikanda na ndege inaruka.

Mkiwa anagani mnatangaziwa kuna machafuko ya hali ya hewa na ndege haiwezi kufika South Africa inabidi mtue Zambia kwa dharura.

Unafika Zambia unapewa makazi na unaambiwa haya ndiyo yatakua maisha yako. Inabidi uanze kuzoea maisha ya Zambia.

Ndivyo ilivyo unapobeba mimba na kuzaa mtoto mwenye ukemamvu. Unabidi uzoee maisha ya kulea mtoto mlemavu.
 
kwa niliowaona, kheri hata kwa uziwi lakini katimilika. Kuna wale ambao labda wana autism yaani anakuwa hatulii, anapiga kelele kila mara yaani kiufupi hajitambui na bado unakuta ana ulemavu wa viungo unaohitaji full support ya mzazi.. Ni kazi sana na wachache wanaweza hata kuwa na fahari ya kuwa na mtoto wa namna hiyo

wenye kipato kiasi huishia kuwapeleka shule at least wawe na muda mchache wa kuwaangalia kuliko wakishinda nao maana hata kazi hawawezi kufanya

ila katika hizi cases ndio nilitambua kuwa mama sio kitu cha kawaida kutokea duniani. Mama ni mtu extraordinary, anaweza kukupenda hata kama dunia nzima haioni sababu hata moja ya kukupenda na kukushikilia. Watakupigania na kukupenda hadi tone la mwisho. Respect sana kwa wamama wote
 
Yohana 9: 1 Hata alipokuwa akipita alimwona mtu, kipofu tangu kuzaliwa.

2 Wanafunzi wake wakamwuliza wakisema, Rabi, ni yupi aliyetenda dhambi, mtu huyu au wazazi wake, hata azaliwe kipofu?

3 Yesu akajibu, Huyu hakutenda dhambi, wala wazazi wake; bali kazi za Mungu zidhihirishwe ndani yake.
 
kwa niliowaona, kheri hata kwa uziwi lakini katimilika. Kuna wale ambao labda wana autism yaani anakuwa hatulii, anapiga kelele kila mara yaani kiufupi hajitambui na bado unakuta ...
Nilifanikiwa kutembelea shule kadhaa zinazotoa elimu kwa wenye mahitaji maalum!

Sawa elimu ni bure! Lakini mazingira ni duni sana, vitanda na magodoro vimechakaa sana, maji ya shida, chakula hakielezeki..

Nilitamani sana mazingira yao yaboreshwe ili iwe kama sehemu ya faraja kwenye maisha yao!

Mungu atupe uzima, kuna kitu naplan kufanya kwa ajili yao!!
 
Nilifanikiwa kutembelea shule kadhaa zinazotoa elimu kwa wenye mahitaji maalum!

Sawa elimu ni bure! Lakini mazingira ni duni sana, vitanda na magodoro vimechakaa sana, maji ya shida, chakula hakielezeki...
Mbaya zaidi hata wakipata ajira, wafanyakazi wenzao hawana elimu ya kuishi nao katika mazingira ya kazi.

Pia kuna mashirika kibao yanayojifanya kupokea misaada ya kuwasaidia ila pesa zinaishia mifukoni mwa wachache, nadhani ndio maana angels nyingi sana zilifutwa baada ya kustukia hii michezo
 
Nilifanikiwa kutembelea shule kadhaa zinazotoa elimu kwa wenye mahitaji maalum!

Sawa elimu ni bure! Lakini mazingira ni duni sana, vitanda na magodoro vimechakaa sana, maji ya shida, chakula hakielezeki....
Mkuu shule zenye unafuu ni zile zenye wafadhili maana huwa wanatoa pesa kiasi kwa ajili ya kuboresha mazingira.

Na hata hizo zinazopewa bado hawazipokei directly maana zinapitia kwenye mifumo rasmi ya serikali na unajua pesa ikishashikwa na mikono mingi hadi ije kumfikia mlengwa, huwa kiasi tofauti na ilivyotolewa.

Pia hawa wasimamizi wa elimu nao hawaweki msisitizo kwa shule zenye mahitaji maalumu. Patia picha mwalimu mmoja atawezaje kudeal na wanafunzi wenye ulemavu tena wenye mahitaji tofauti tofauti.

mwisho wa siku ni lazma tu atashindwa
 
kwa niliowaona, kheri hata kwa uziwi lakini katimilika. Kuna wale ambao labda wana autism yaani anakuwa hatulii, anapiga kelele kila mara yaani kiufupi hajitambui na bado unakuta ana ulemavu wa viungo unaohitaji full support ya mzazi.. Ni kazi sana na wachache wanaweza hata kuwa na fahari ya kuwa na mtoto wa namna hiyo

wenye kipato kiasi huishia kuwapeleka shule at least wawe na muda mchache wa kuwaangalia kuliko wakishinda nao maana hata kazi hawawezi kufanya

ila katika hizi cases ndio nilitambua kuwa mama sio kitu cha kawaida kutokea duniani. Mama ni mtu extraordinary, anaweza kukupenda hata kama dunia nzima haioni sababu hata moja ya kukupenda na kukushikilia. Watakupigania na kukupenda hadi tone la mwisho. Respect sana kwa wamama wote

Chini ya jua hakuna kitu Cha thamani kama kuzaliwa na wazazi wanaojua wajibu na majukumu yao.......

Mpaka unafikia utu uzima na kujitegemea nafsi yako inakuambia kuwa una deni dhidi ya wazazi wako........
 
Nasema hivi maana mambo ya aibu ndio huwa tuanakazania kuyaficha na ndivyo ilivyo kwa wazazi wenye hawa watoto huwa hawapendi watoto wao wenye ulemavu kujulikana ni watoto wao, wanawafungia majumbani huku wakijificha nyuma ya kivuli cha kuwalinda.

yani mtoto anachukuliwa kama mzigo flani hivi, niliwahi kushuhudia laivu bila chenga hospitali flani mtoto kazaliwa na ulemavu wa ngozi, baba wa mtoto alikana mtoto huyo sio wake na ndio ukawa mwisho wa mahusiano na mzazi mwenzake.
Point yako ni kweli. Inategemes kama mtoto unaweza mchukua , mfano akili haipo vizuri, epilepsy attacks, kujiendea choo nk. Inakuwa ngumu kumchukua kila mahali
 
Chini ya jua hakuna kitu Cha thamani kama kuzaliwa na wazazi wanaojua wajibu na majukumu yao.......

Mpaka unafikia utu uzima na kujitegemea nafsi yako inakuambia kuwa una deni dhidi ya wazazi wako........
na hilo deni huwa halilipiki mkuu

huwezi ilipa sacrifise ya mzazi zaidi ya kuwafanya waishi pasipo kujuta au kuhuzunika sababu ya uwepo wako katika maisha yao
 
na hilo deni huwa halilipiki mkuu

huwezi ilipa sacrifise ya mzazi zaidi ya kuwafanya waishi pasipo kujuta au kuhuzunika sababu ya uwepo wako katika maisha yao
Lengo sio kulipa bali litakufanya uwe karibu na kuwaheshimu wazazi wako.....
 
Back
Top Bottom