Uchaguzi 2020 Kwanini kura za Uchaguzi Mkuu hazihesabiwi hadharani kama za CCM kuchagua wagombea?

Uchaguzi 2020 Kwanini kura za Uchaguzi Mkuu hazihesabiwi hadharani kama za CCM kuchagua wagombea?

Kwa upinzani wa kutegemea mgombea atokee chama tawala unatarajia nini? Kwamba upinzani utashinda?
 
Tanzania imeamka! na alieiamsha si mwingine ni Mkulu mwenyewe ambae anahitaji watu makini waliochaguliwa kwa haki kumsaidia kazi! shime watanzania tupaze sauti kura zihesabiwe vituoni mbele ya wapiga kura na hapo tutakuwa tumepata short cut ya kudai tume huru ya uchaguzi ambayo mchakato wake ni mrefu! ila ni lazima polisi wawepo wa kutosha vituoni kuepusha vurugu!!

Tunakuomba Rais wetu mpendwa amuru hili lifanyike kura zihesabiwe kwa uwazi majimboni mbele ya wapiga kura manake wewe huna cha kupoteza hata kupiga kura ya Urais sisi wapiga kura wako tunaona ni kupoteza pesa tu, kazi ipo kwa wabunge na madiwani! Please Mkulu nyoosha nchi katika hili pia, utamaduni wa uwazi uliouanzisha mchakato wa mteule wa Urais Zanzibar uendelezwe maana ule ulikuwa uzalendo kumzidi Nyerere!!

Zitto Kabwe , Fatma Karume, Nyalandu na Membe hii ni agenda nzuri kuisimamia si mnataka utawala wa sheria na haki nyie? shikilieni hili sasa!

Mods please wekeni huu uzi first page hata mwezi mzima ili tupate haki uchaguzi huu!
 
Kwani sasa huhesabiwaje?

Utaratibu wa tume upo sawa,nashangaa wapinzani wanavyodai tume huru.
 
Huko umefika mbali sana. Kikubwa ni kuwa kabla tu ya uchaguzi, wasimamizi wa uchaguzi hula KIAPO CHA KUTUNZA SIRI ZA UCHAGUZI.
 
subutu hilo halitawezekana katu abadan kha!!! unataka wasirudi madarakani
 
Hoja yako ni njema ila utapingwa sana,wamezoea vya kunyonga vya kuchinja hawawezi.Hawahesabu kura hadharani maana wanafahamu hawatashinda,hivyo ili washinde kwa kishindo lazima kura zihesabiwe gizani.Hiyo ndiyo CCM Mpya inayokubaliki.
 
Huko umefika mbali sana. Kikubwa ni kuwa kabla tu ya uchaguzi, wasimamizi wa uchaguzi hula KIAPO CHA KUTUNZA SIRI ZA UCHAGUZI.
Kiapo?Sawa viongozi wote pia hula viapo na bado wanashiriki matendo yaliyo kinyume na viapo vyao.
Watawala hawa hawajali viapo,wamevunja viapo Vingi kuanzia ndoa zao,imani zao za dini,hata viongozi wa dini nao wanavunja viapo vyao sembuse kazi ya uchaguzi ambayo siyo ya kudumu?
 
NDIO maana nakwambia huwa kuna KIAPO CHA KUTUNZA SIRI. SASA kama uchaguzi una SIRI, nani atakubali kura zihesabiwe hadharani??
Kiapo?Sawa viongozi wote pia hula viapo na bado wanashiriki matendo yaliyo kinyume na viapo vyao.
Watawala hawa hawajali viapo,wamevunja viapo Vingi kuanzia ndoa zao,imani zao za dini,hata viongozi wa dini nao wanavunja viapo vyao sembuse kazi ya uchaguzi ambayo siyo ya kudumu?
 
Kwani sasa huhesabiwaje?

Utaratibu wa tume upo sawa,nashangaa wapinzani wanavyodai tume huru.
Ulichojaaliwa ni uwezo wako mkubwa wa kujitoa fahamu.
Mgombea mmojawapo anapoweza kupanga safu ya kumshindisha, kwako ndio USAWA huo?
 
NDIO maana nakwambia huwa kuna KIAPO CHA KUTUNZA SIRI. SASA kama uchaguzi una SIRI, nani atakubali kura zihesabiwe hadharani??
Ndugu nina uhakika hujawahi kutoka nje ya nchi! kama umetoka basi ni kwenda kama mzigo si kujilipia na kuwa huru! una mawazo mgando ( conservative) kama Nyerere!!

Magufuli is different! he is genius, he is special, ni mzalendo kuzidi Nyerere, Magufuli ni mzungu na anawaza outside the box ndo maana pale Dodoma walimwambia Mzee kamera ziondolewe sasa tuanze mkutano akamuuliza Katibu Mkuu kwani kuna siri gani?

nami nakuuliza wewe sisi ndio tumekuja kituoni kupiga kura tumemaliza kwanini tulichokifanya sisi nyie wasimamizi mkifanye siri? si mpige kura wenyewe kisha mfanye siri kwanini mtuite sisi tupige kura halafu mtufiche zoezi la kuhesabu kura??

huu usiri ni upumbavu ni uprmitive, inafaa ukomeshwe!!wakati wake ni sasa!!
 
Ndugu nina uhakika hujawahi kutoka nje ya nchi! kama umetoka basi ni kwenda kama mzigo si kujilipia na kuwa huru! una mawazo mgando ( conservative) kama Nyerere!! Magufuli is different! anawaza outside the box ndo maana pale Dodoma walimwambia Mzee kamera ziondolewe tuanze mkutano akauliza Katibu kwani kuna siri gani? nami nakuuliza sisi ndio tumekuja kupiga kura tumemaliza kwanini tulichokifanya sisi nyie wasimamizi mkifanye siri? huu usiri ni upumbavu inafaa ukomeshwe!!
Lakini ndio huyo huyo aliyehakikisha anakuwa peke yake. Angekuwa na Membe asingekubali iwe live. Ok inshort WANANCHI Mara nyingi huwa hawaichagui CCM hivyo CCM haiwezi kukubali kuhesabu kura za Urais hadharani. Usishangae kwanini hawataki matokeo ya Urais yahojiwe mahakamani
 
uko sahihi kuwa sisiem wamezuia demokrasia isifanyike ndani mwake, ila mtu mmoja Rais hana athari kubwa kama wabunge 300 na madiwani kama wote nchi nzima!!
Sote tunajua hata Membe mwenyewe deep down in his heart anajua hata kama angepewa form angeshindwa na Magufuli!
 
uko sahihi kuwa sisiem wamezuia demokrasia isifanyike ndani mwake, ila mtu mmoja hana athari kubwa kama wabunge 300 na madiwani kama wote nchi nzima!!
Madiwani wanatangazwa na Mtendaji wa kata (KADA ) Wabunge wanatangazwa na Wakurugenzi (MAKADA) hawa wote ni wa kufuata maelekezo tu.
 
Back
Top Bottom