Kwanini kusiwe na Shirika la Meli la Muungano ili kuepuka usajili wa kiholela?

Parabolic

JF-Expert Member
Joined
Dec 3, 2013
Posts
2,922
Reaction score
3,252
Kufuatia tukio la kukamatwa kwa meli iliyokuwa na bendera ya Tanzania, iliyokuwa na tani 6.6 za dawa za kulevya aina cocaine katika eneo la La Unión, El Salvador Februari 19, 2026,, kuna haja ya kutafakari upya suala la usajili wa meli nchini.

Wakati Serikali ya Jamhuri ya Muungano ikiwa na Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC), Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar nao wana Shirika la Meli Zanzibar. Mashirika haya yote yanafanya kazi zinazoingiliana ndani ya Jamhuri ya Muungano.

Matokeo yake sasa Shirika la Meli la Zanzibar limekuwa likisajili meli katika maeneo mbalimbali duniani na zinapokamatwa, zinaonekana zimesajiliwa Tanzania. Bendera ya Tanzania inatumika vibaya kufanyia uhalifu huko duniani.

Tukio la El Salvador sio la kwanza. Aprili 22, 2025 Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran (IRGC) limekamata meli mbili zilizokuwa na bendera ya Tanzania, zikidaiwa kuwa zilisafirisha mafuta ya dizeli kwa njia ya magendo katika Ghuba ya Uajemi,

Septemba 15, 2023 Serikali ya Iran ilitangaza kukamatwa kwa meli iliyosheheni mafuta ya magèndo inayopeperusha benders ya Tanzania.

Januari 5, 2018 meli iliyokuwa ikipeperusha bendera ya Tanzania ilikamatwa na kushikiliwa huko Santo Domingo, Jamhuri ya Dominican ikiwa na dawa za kulevya aina ya Cocaine kilo 1,600.

Kwa mifano hii yote, bado Serikali haini umuhimu wa kuunganisha haya mashirika ili kuwa na kauli moja katika usajili wa meli zinazozurura huko duniani? Imefika mahali sasa majangili na wahalifu wengine wanatumia bendera ya Tanzania kufanyia uhalifu kisa tu wamesajiliwa Zanzibar. Hii ndio faida ya Muungano?
 
Parabolic una hoja nzuri na muhimu sana. Sijui kwanini hadi sasa Serikali haijazungumzia hili

Miaka ya nyuma kama ulivyo eleza, ''Wakubwa'' waliishukia Tanzania kwa meli za magendo ya mafuta kukwepa vikwazo Iran. Ni zigo lililoelekea kuwaumiza Watanzania hasa Watanganyika kwasbabu meli zilisajiliwa Zanzibar

Matukio yote ya usajili wa meli kiholela unafanyika Zanzibar kwasababu SMZ inachukua pesa. Madhara ya usajili holela anaubeba Mtanganyika kupitia Tanzania kwasababu Zanzibar wanapeperusha bendera ya Tanzania.

Pesa zinazopatikana kutokana na usajili wa meli hizo haramu zibaki Zanzibar licha ya ukweli kwamba zimetumia Bendera ya Tanzania.

Kwanini tuna taasisi za Muungano na za Zanzibar? Ni kwamba Taasisi za Muungano ni za Tanganyika katika ubatizo wa Tanzania. Taasisi za Zanzibar ni za huko tu. Kinachofanyika ni ku 'abuse'' kwa kutumia kauli ya '' Kila Mzanzibar ni Mtanzania lakini si kila Mtanzania ni Mzanzibar''

JokaKuu Pascal Mayalla Mzee Mwanakijiji
 
'' Kila Mzanzibar ni Mtanzania lakini si kila Mtanzania ni Mzanzibar''
JokaKuu Pascal Mayalla Mzee Mwanakijiji
Kwa mukhtadha huo, kila mali ya Tanzania pia ni ya Tanzania na Zazibari, ila kila mali ya Zanzibar ni ya Zanzibar. only. Kwenye uhalifu, aliyekutwa na ngozi, ndiye aliyekula nyama, meli hiyo ni meli yetu na mzigo ni mzigo wetu!.
P
 
Makamo wa pili wa zenji Hemedi Abdullah anakazia

View: https://youtube.com/shorts/EGGF3e8gYgk?si=4HqHIP8bdyDTsWYd

Kimsingi kuna zanzibar na Tanzania bara
 
Parabolic una hoja nzuri na muhimu sana. Sijui kwanini hadi sasa Serikali haijazungumzia hili

Miaka ya nyuma kama ulivyo eleza, ''Wakubwa'' waliishukia Tanzania kwa meli za magendo ya mafuta kukwepa vikwazo Iran. Ni zigo lililoelekea kuwaumiza Watanzania hasa Watanganyika kwasbabu meli zilisajiliwa Zanzibar

Matukio yote ya usajili wa meli kiholela unafanyika Zanzibar kwasababu SMZ inachukua pesa. Madhara ya usajili holela anaubeba Mtanganyika kupitia Tanzania kwasababu Zanzibar wanapeperusha bendera ya Tanzania.

Pesa zinazopatikana kutokana na usajili wa meli hizo haramu zibaki Zanzibar licha ya ukweli kwamba zimetumia Bendera ya Tanzania.

Kwanini tuna taasisi za Muungano na za Zanzibar? Ni kwamba Taasisi za Muungano ni za Tanganyika katika ubatizo wa Tanzania. Taasisi za Zanzibar ni za huko tu. Kinachofanyika ni ku 'abuse'' kwa kutumia kauli ya '' Kila Mzanzibar ni Mtanzania lakini si kila Mtanzania ni Mzanzibar''

JokaKuu Pascal Mayalla Mzee Mwanakijiji
Kwani ZNZ sio Tanzania?
 
Unazingua Mkuu...Zama za Kudai Tanganyika yetu,wewe unataka kuingiza kimeo Kingine.
 
Kwa mukhtadha huo, kila mali ya Tanzania pia ni ya Tanzania na Zazibari, ila kila mali ya Zanzibar ni ya Zanzibar. only. Kwenye uhalifu, aliyekutwa na ngozi, ndiye aliyekula nyama, meli hiyo ni meli yetu na mzigo ni mzigo wetu!.
P
Huu mfano ni mzuri sana. Kwa mfano, dhahabu iliyouzwa ili ''kuleta uzani'' pesa ni za BoT na Zanzibar wana 9%
Sababu ni kwamba BoT na dhahabu ni za Tanzania ambayo Zanzibar ni sehemu yake.
Mafuta na gesi ya Zanzibar ''zitakapouzwa'' mapato ni ya Zanzibar kwasababu '' Zanzibar si Tanzania''.

Ni kweli mwizi ni aliyekamatwa na ngozi na kwa hili la meli ni Tanzania. Kinachosumbua ni kwamba mapato ya usajili wa meli ni ya Zanzibar tu. Kwa maneno mengine Mtanganyika analipa gharama za uhalifu asiohusika nao.
 
Tunatakiwa tufike mahali tuongee tuwe kitu kimoja. Huu mgawanyiko unaleta kero nyingi zisizo na sababu.
 
Ni kweli mwizi ni aliyekamatwa na ngozi na kwa hili la meli ni Tanzania. Kinachosumbua ni kwamba mapato ya usajili wa meli ni ya Zanzibar tu. Kwa maneno mengine Mtanganyika analipa gharama za uhalifu asiohusika nao.
Ni kweli Mtanganyika kwa jina la Tanzania, kimataifa ndie mzazi wa Zanzibar, na ndiye mdhamini wa Zanzibar katika issues zote za Kimataifa, hivyo mtoto akiboronga, ni baba ndiye ana wajibika chini ya kanuni ya fiduciary responsibility kwa wajibu wa mzazi kwa mtoto, kosa ni la mtoto, lakini anayewajibika ni mzazi!。
P
 
Kufuatia tukio la kukamatwa kwa meli iliyokuwa na bendera ya Tanzania, iliyokuwa na tani 6.6 za dawa za kulevya aina cocaine katika eneo la La Unión, El Salvador Februari 19, 2026,, kuna haja ya kutafakari upya suala la usajili wa meli nchini.

Wakati Serikali ya Jamhuri ya Muungano ikiwa na Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC), Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar nao wana Shirika la Meli Zanzibar. Mashirika haya yote yanafanya kazi zinazoingiliana ndani ya Jamhuri ya Muungano.

Matokeo yake sasa Shirika la Meli la Zanzibar limekuwa likisajili meli katika maeneo mbalimbali duniani na zinapokamatwa, zinaonekana zimesajiliwa Tanzania. Bendera ya Tanzania inatumika vibaya kufanyia uhalifu huko duniani.

Tukio la El Salvador sio la kwanza. Aprili 22, 2025 Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran (IRGC) limekamata meli mbili zilizokuwa na bendera ya Tanzania, zikidaiwa kuwa zilisafirisha mafuta ya dizeli kwa njia ya magendo katika Ghuba ya Uajemi,

Septemba 15, 2023 Serikali ya Iran ilitangaza kukamatwa kwa meli iliyosheheni mafuta ya magèndo inayopeperusha benders ya Tanzania.

Januari 5, 2018 meli iliyokuwa ikipeperusha bendera ya Tanzania ilikamatwa na kushikiliwa huko Santo Domingo, Jamhuri ya Dominican ikiwa na dawa za kulevya aina ya Cocaine kilo 1,600.

Kwa mifano hii yote, bado Serikali haini umuhimu wa kuunganisha haya mashirika ili kuwa na kauli moja katika usajili wa meli zinazozurura huko duniani? Imefika mahali sasa majangili na wahalifu wengine wanatumia bendera ya Tanzania kufanyia uhalifu kisa tu wamesajiliwa Zanzibar. Hii ndio faida ya Muungano?
Ukiufuatilia muungano utakuwa chizi, mambo kibao yako ndivyo sivyo. Wana bendera yao sasa kwanini wanapoingia contacts ambazo yaliyomo si ya muungano inakuwaje hawatumii utambulisho wao (hapa namaanisha bendera) bali wanatumia utambulisho wa muungano(hapa namaanisha bendera ya Tanzania).
 
Kwa maneno mengine Mtanganyika analipa gharama za uhalifu asiohusika nao.
Hii ni sawa na mfano maarufu huko Mtaani . " Pesa za miradi zitolewazo ni za fulani, lakini madeni ya mikopo ni ya wote hapo Mtaani".

Wanamtaa wanauliza Sasa hela za mkopo zinaenda wapi na huyu Fulani anatoa wapi hizi hela.?
 
Ni kweli Mtanganyika kwa jina la Tanzania, kimataifa ndie mzazi wa Zanzibar, na ndiye mdhamini wa Zanzibar katika issues zote za Kimataifa, hivyo mtoto akiboronga, ni baba ndiye ana wajibika chini ya kanuni ya fiduciary responsibility kwa wajibu wa mzazi kwa mtoto, kosa ni la mtoto, lakini anayewajibika ni mzazi!。
P
Whilst Msigwa jumba bovu analiangushia Zanzibar as if it is a sovereign state.
 
Kwa mifano hii yote, bado Serikali haini umuhimu wa kuunganisha haya mashirika ili kuwa na kauli moja katika usajili wa meli zinazozurura huko duniani? Imefika mahali sasa majangili na wahalifu wengine wanatumia bendera ya Tanzania kufanyia uhalifu kisa tu wamesajiliwa Zanzibar. Hii ndio faida ya Muungano?
1. Kwanza tujuze hii meli isajiliwa Zanzibar au Bara.
2. Mambo ya muungano huwa hayaingizwi tu kama vile unajaza dagaa kwenye kapu.
3. Siungi mkono wazo la kuunganisha mashirika haya.

Unataka yaunganishwe halafu yaongozwe Bara na yakiomgozwa Zanzibar iwe nongwa.

Wacha tuende hivihivi na tutafika. Bado kuna maeazo ya kuifjibiti Zanzobar kama vile muungano huu kwa ajili ya Bara/Tanganyika.
 
Back
Top Bottom