KING MIDAS
JF-Expert Member
- Dec 1, 2010
- 8,589
- 16,936
KWANINI KUTUA KWA AIRBUS A380 NCHINI KUNAIBUA HISIA NA GUMZO?
Airbus A380 ndiyo ndege kubwa na nzito zaidi ya abiria ulimwenguni kwa sasa.
Yapata urefu wa mita 73, kimo cha mita 24, uzito wa juu wa kuruka tani 560, pamoja na uwezo wa kubeba hadi abiria 853 endapo itapangwa viti katika mfumo wa daraja la uchumi (Economy Class).
Kwa mujibu wa kampuni ya Airbus, ndege yao A380 inahudumiwa na viwanjwa vya ndege 140 ulimwenguni kote, na viwanja vya ndege 400 inaweza kutua wakati wa dharura.
Kumbuka hadi sasa ulimwenguni, kuna jumla ya viwanja vya ndege inayofikia 40,000 kwa mujibu wa 'database' ya www.world-airport-codes.com
Kwasababu hizo, ili kuhudumia Airbus380, viwanja vya ndege vinahitaji kuhakikisha njia zao za kurukia ndege (Runways) ni pana vya kutosha kwa matairi, Njia za michepuko (Taxiways) ngumu, pamoja na maegesho kwenye majengo yaweze kuruhusu mabawa makubwa kupita pasipo kuzuia shughuli zingine za uwanja wa ndege.
Lakini pia A380 ni ndege ya ghorofa (Double Decker) hivyo kuhudumia inahitaji njia za juu za abiria au ngazi kwaajili ya kupanda na kushuka pasipo usumbufu wowote.
Hivyo basi, kutua kwa Airbus380 katika uwanja wa ndege wa kimataifa Julius Nyerere (JNIA) na kupata huduma za dharura zinazostahili, ni sehemu ya viwanja vichache duniani vyenye sifa, usalama na uwezo wa kupokea ndege husika.
Tambua kwamba, uwezo wa kuhudumia ndege zenye mahitaji maalumu, inaongeza hadhi ya uwanja wa ndege kitaifa na kimataifa.
Swali la kujiuliza,
je, kwanini kwa awamu mbili tofauti ndege za Airbus380 zilichagua kutua kwa dharura uwanja wa ndege wa kimataifa Julius Nyerere ikiwa kuna viwanja vya ndege katika nchi nyingi zinazopakana au zilizo njiani?
kwa maoni na hoja zenye tija kwa watu wote tukutane kwenye "Comments"
Shukrani