Kwanini kutua kwa Airbus A380 nchini kunaibua hisia na gumzo?

KWANINI KUTUA KWA AIRBUS A380 NCHINI KUNAIBUA HISIA NA GUMZO?

Airbus A380 ndiyo ndege kubwa na nzito zaidi ya abiria ulimwenguni kwa sasa.
Yapata urefu wa mita 73, kimo cha mita 24, uzito wa juu wa kuruka tani 560, pamoja na uwezo wa kubeba hadi abiria 853 endapo itapangwa viti katika mfumo wa daraja la uchumi (Economy Class).

Kwa mujibu wa kampuni ya Airbus, ndege yao A380 inahudumiwa na viwanjwa vya ndege 140 ulimwenguni kote, na viwanja vya ndege 400 inaweza kutua wakati wa dharura.
Kumbuka hadi sasa ulimwenguni, kuna jumla ya viwanja vya ndege inayofikia 40,000 kwa mujibu wa 'database' ya www.world-airport-codes.com

Kwasababu hizo, ili kuhudumia Airbus380, viwanja vya ndege vinahitaji kuhakikisha njia zao za kurukia ndege (Runways) ni pana vya kutosha kwa matairi, Njia za michepuko (Taxiways) ngumu, pamoja na maegesho kwenye majengo yaweze kuruhusu mabawa makubwa kupita pasipo kuzuia shughuli zingine za uwanja wa ndege.

Lakini pia A380 ni ndege ya ghorofa (Double Decker) hivyo kuhudumia inahitaji njia za juu za abiria au ngazi kwaajili ya kupanda na kushuka pasipo usumbufu wowote.

Hivyo basi, kutua kwa Airbus380 katika uwanja wa ndege wa kimataifa Julius Nyerere (JNIA) na kupata huduma za dharura zinazostahili, ni sehemu ya viwanja vichache duniani vyenye sifa, usalama na uwezo wa kupokea ndege husika.

Tambua kwamba, uwezo wa kuhudumia ndege zenye mahitaji maalumu, inaongeza hadhi ya uwanja wa ndege kitaifa na kimataifa.

Swali la kujiuliza,
je, kwanini kwa awamu mbili tofauti ndege za Airbus380 zilichagua kutua kwa dharura uwanja wa ndege wa kimataifa Julius Nyerere ikiwa kuna viwanja vya ndege katika nchi nyingi zinazopakana au zilizo njiani?

kwa maoni na hoja zenye tija kwa watu wote tukutane kwenye "Comments"

Shukrani
Ndege ikiwa kubwa tunaiita dege.
 
Ila lile dude linakula wese balaa. Pipa kwa sekunde. Tangi lake ni kama swimming pool saba.
Mkuu hivi umefikiria ulichoongea hapo ? Yaani sihitaji hata ku-google kuona hio kitu sio realistic... kwa unachosema hii tungeweza kuiita ndege ya mafuta na sio ndege ya watu wala isingekuwa one of the most efficient kwenye matumizi per person
 
Mkuu ni kweli. Dude linakula wese balaa pipa 60 kwa dakika. Siyo lita mkuu namaanisha PIPAna uhakika nachosema. Umeshaona tanki lake linaeza jaza robo ya bwawa la Nyerere. Tanki lake ni futi 100 kwa urefu.
 
Ila lile dude linakula wese balaa. Pipa kwa sekunde. Tangi lake ni kama swimming pool saba.
Hahaaaa!!!hii kali sasa safari linazosafiri masaa 6 non-stop huwa linatembea na pipe ya mafuta toka kwenye pump ?kwani kwa ubugiaji huo hakuna tenki la mafuta linaloweza kutosha mafuta ya safari hiyo
 
Mkuu ni kweli. Tenki lake ni zaidi ya futi 100 na linaweza jaza robo la bwawa la Nyerere. Sehemu kubwa asilimia 80 la hilo dege ni tenki.
 
Hata kama ni hivyo mkuu haiwezi kutumia pipa moja (lita 200) kwa sekunde!!!kwanza uwezo wake wa juu wa tanks zake kuhifadhi mafuta ni kama lita 320,000.
 
TAA si wametoa report, Ndege imetua kwa dharura kutokana na Hali mbaya ya hewa na ujazaji wa mafuta.

Japo kukwepa Anga la Sudan halikuwekwa wazi ila pia ni sababu.

Kwa nini imetua JKNIA? Si unajiongeza tu kwa sababu uwanja wetu una uwezo na Tanzania ndio nchi salama zaidi kwa Africa mashariki na Kati.
 
Tujipange na kujitangaza Dar iwe Hub ndege kubwa za long ranges....kuweka mafuta hapa kwetu ni opportunity mpya tuichangamkie......ndege kwenda Brazil...Argentina kutoka Dubai na Qatar ....South America....ziwe anaweka mafuta hapa ......hasa kurudi ....
Bonge la wazo aisee
 
Nafikiri safari hii wameshindwa kwenda Nairobi kutokana na ukaribu wake na Sudan ,
Sababu ya kujaza mafuta hapa ni kwa kuwa wana avoid Sudan airspace
 
KWANINI KUTUA KWA AIRBUS A380 NCHINI KUNAIBUA HISIA NA GUMZO?

Airbus A380 ndiyo ndege kubwa na nzito zaidi ya abiria ulimwenguni kwa sasa.
Yapata urefu wa mita 73, kimo cha mita 24, uzito wa juu wa kuruka tani 560, pamoja na uwezo wa kubeba hadi abiria 853 endapo itapangwa viti katika mfumo wa daraja la uchumi (Economy Class).

Kwa mujibu wa kampuni ya Airbus, ndege yao A380 inahudumiwa na viwanjwa vya ndege 140 ulimwenguni kote, na viwanja vya ndege 400 inaweza kutua wakati wa dharura.
Kumbuka hadi sasa ulimwenguni, kuna jumla ya viwanja vya ndege inayofikia 40,000 kwa mujibu wa 'database' ya www.world-airport-codes.com

Kwasababu hizo, ili kuhudumia Airbus380, viwanja vya ndege vinahitaji kuhakikisha njia zao za kurukia ndege (Runways) ni pana vya kutosha kwa matairi, Njia za michepuko (Taxiways) ngumu, pamoja na maegesho kwenye majengo yaweze kuruhusu mabawa makubwa kupita pasipo kuzuia shughuli zingine za uwanja wa ndege.

Lakini pia A380 ni ndege ya ghorofa (Double Decker) hivyo kuhudumia inahitaji njia za juu za abiria au ngazi kwaajili ya kupanda na kushuka pasipo usumbufu wowote.

Hivyo basi, kutua kwa Airbus380 katika uwanja wa ndege wa kimataifa Julius Nyerere (JNIA) na kupata huduma za dharura zinazostahili, ni sehemu ya viwanja vichache duniani vyenye sifa, usalama na uwezo wa kupokea ndege husika.

Tambua kwamba, uwezo wa kuhudumia ndege zenye mahitaji maalumu, inaongeza hadhi ya uwanja wa ndege kitaifa na kimataifa.

Swali la kujiuliza,
je, kwanini kwa awamu mbili tofauti ndege za Airbus380 zilichagua kutua kwa dharura uwanja wa ndege wa kimataifa Julius Nyerere ikiwa kuna viwanja vya ndege katika nchi nyingi zinazopakana au zilizo njiani?

kwa maoni na hoja zenye tija kwa watu wote tukutane kwenye "Comments"

Shukrani
Nimesafiri ndani ya hiyo ndege, Dubai-Tokyo-Dubai.
Ni ndege kubwa sana, lakini iko very comfortable.
Angekuwepo Magufuli angeinunua cash cash.
 
Back
Top Bottom