Wale wanajeshi unaowaona wanaruka kwa parachuti ile inakua sio ajali ni sehemu ya kazi, ikitokea ajali hata wao huwa wanapoteza maisha, ikitokea kwenye ndege kukawa na huo muda utakaotosha watu kujiandaa na kuweza kutoka kwa kutumia parachuti basi muda huo unatosha kwa rubani kutua kwenye kiwanja cha karibu kabla ya ajali na ndivyo wamekua wakifanya.
Hivi sasa wataalam wanachemsha vichwa kuona namna ya kuwa na parachuti moja ile sehemu wanayokaa abiria ili ikitokea ajali rubani abonyeze tu kitufe ambacho kitaitenga sehemu ya abiria na kufungua parachuti, lakini bado Luna changamoto nyingi kulifanikisha hilo.
Kwahiyo kinachofanyika hivi sasa ni kuongeza utaalam zaidi kwenye kuzuia ajali zisitokee.