Ujenzi wa choo kizuri na salama kwa matumizi sio jambo linalozingatiwa sana hasa kwenye nyumba za kupanga hasa hizi za bei za kawaida (10K-150K). Unakuta nyumba nzuri na mazingira n mazuri ila chooni utadhani kulisahaulika wakafosi kujenga ili choo kiwepo.
Vyoo vingi ni vidogo sana, na namna miundombinu inavyowekwa ndio shida kabisa hali inayopelekea shida kwa watumiaji. Angalia mfano pichani wa hicho choo kilivyosetiwa na kujengwa ni sahihi?
View attachment 3304752
Kuna kipindi nilikuwa nafuatilia ishu fulani mkoani nikaona gharama za gest ni kubwa sana kwa siku nitakazokuwa pale, nikaamua kupanga chumba mwezi mmoja na mbaya zaidi nililupia bila kuona choo na kwa uzuri wa mazingira ya nyumba ile sikuwa na shaka juu ya hali ya choo, choo chake ni kidogo mno na kifupi, binafsi nilikuwa nateseka na nna mwili wa kawaida tu ila kuna dada alikuwa bonge alafu kapanda hewani, sijui kwa upande wake hali ilikuwaje ila nahisi ni mateso.
Hapa tatizo huwa ni nini?
•mwenye nyumba
•fundi
•eneo
•bajeti hafifu ya ujenzi.
•Sababu za kibiashara(kupunguza gharama)
Ujenzi bora ni pamoja na choo kizuri.
NAWASILISHA..