Kwanini kwenye nyumba za kupanga ujenzi wa vyoo vizuri hauzingatiwi?

BINAFSI nnazo nyumba za makazi za kupangisha mkuu, (Nna jumla ya wapangaji 36) nyumba tofauti tofauti.

Nna vyumba VYA kuanzia elfu 20 Hadi laki 1

Ila kiukweli ujenzi WA choo kizuri ni gharama mno.

Na nilichojifunza,
choo kizuri ukikijenga kikawa Cha public, kinachakaa haraka utadhani vyoo vya stendi. (Wapangaji wengi WA public toilet hawajali na Sio watunzaji, hasa kama mwenye nyumba haukai hapo)

Kwasasa,
vyoo vizuri nawajengea wapangaji WA self TU.

Ila KIUHALISIA ujenzi WA Chumba self ni gharama MNO, tunajenga TU ili tupate wapangaji wanaoeleweka na watunzaji WA nyumba.

Ukijenga Chumba self, gharama zake ni sawa na kujenga single mbili standard kabisa.
 
Hivi lile box lililokuwa linazunguka katika kila uso wa uzi likihamasisha watu kubet lilienda wapi?

Tunauomba uongozi wa JF utuwekee box lenye picha ya mama likihamasisha uchaguzi mkuu
 
Hailipi, alafu wapangaji wengi waharibifu wa miundombinu, hawazingatii usafi, Choo bora jenga nyumbani kwako
 
Nyumba nyingi za hivyo huwa mwanzoni hazikujengwa kwa lengo la kupangisha...so baadae mwenye nyumba anaamua kuforce anaongeza vyumba vingine lakini vyoo na chemba zake zinakuwa za zamani hasa mikoani wana hii tabia sana wakiona mji umechangamka na uhitaji wa vyumba ni mkubwa.
Nilishawahi kupanga chumba self-contained mkoani nilijiona kama nakaa chooni ni shida sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…