Kwanini kwenye shughuli za kisiasa Bakwata hupewa uzito kama dhehebu mfano KKKT na Katoliki wakati linawakilisha waislamu wote?

Kwanini kwenye shughuli za kisiasa Bakwata hupewa uzito kama dhehebu mfano KKKT na Katoliki wakati linawakilisha waislamu wote?

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Huwa nashangaa kwenye shughuli za serikali au vyama vya siasa Bakwata huwa na mwakilishi mmoja sawa na madhehebu mengine kama KKKT, Anglican, Katoliki, TAG na Pentecostal wakati Bakwata ni Baraza kuu la waislamu wote.

Kwanini Bakwata isiwe na uwakilishi wa mashehe hata watatu ili kuleta uwiano wa viongozi wa dini wanaoketi siti za mbele na kufanya maombi ya kufungua mikutano na kuliombea taifa?

Ni hilo swali tu dogo lakini muhimu.

Mungu wa mbinguni awabariki sana!

Maendeleo hayana vyama!
 
BAKWATA babalao hawa hata Chadema wameshindwa kuwashawishi kuusanganya umma

Zitto na genge lake la mashskhe njaa wanaiogopa BAKWATA iliyoimara kama mbingu wamebaki kupinga tu

State agent
 
Mashehe wa BAKWATA wanapenda kuonekana kwa TV sana Mpaka najiuliza ivi wanapata mda wa kuongea na waumini wao kweli
 
Sasa hao wengine tofauti na Bakwata wanatambulika na serikali?!
Kutambulika ni kusajiliwa. Kuna Jumuiya na Taasisi za Kiislamu na kadhalika. Hata makanisa/madhehebu yote hayawakilishwi kwenye shughuli hizo. Kikubwa ni kuwa makanisa hayo yamesajiliwa kwa mujibu wa sheria na taratibu zilizopo.
 
Ina maana waislamu wa Bakwata wanatoka dhehebu mojja au dhehebu zaidi ya moja kama ilivyo CCT?
 
Maswali mengine ujibu mwenyewe. Nijuavyo, BAKWATA hakuna Sunni
Ok ngoja aje Allen Kilevela maana babu yake ni miongoni mwa waasisi wa Bakwata....... Binafsi najivunia kusoma shule ya Bakwata mkoani Iringa ambayo walimu walikuwa ni TX kutoka Pakistan na Iran!
 
Back
Top Bottom