Kwanini Landrover Defender zinapendwa sana?

Hiyo Land Rover ilikuwa gari ya kwanza kutumika sehemu nyingi za nchi za Africa. Ugumu wake sio kwenye injini hizo za Tdi200/ Tdi300 au Td5, uimara wake umedhihirika kwenye body.

Hizo injini za Tdi200/300 hazikufanya vizuri huko ulaya mpaka jumuiya ya ulaya zikakataliwa kutokana na uchafuzi wa hewa(Euro Emission Regulations).

Hata kwenye soko saizi hakuna serikali au taasisi kubwa duniani wanaonunua kwa wingi hizo gari UN na NATO walihamia kwenye L/cruiser. Hata waasi nao walihamia kwenye Hilux na L/Cruiser.
 
Mie naonaga hii gari ya Mhindi iko over rated.. Serikalini walizishibokea sana miaka hiyo ila wakaona zinakufa mapema kuliko Landcruser ya mkonga, wakazi diss!
Hizi gari saizi zipo chini ya mhindi wanaitwa Khan.

Hawa jamaa wamepitia magumu wamewahi kumilikiwa mpaka na BMW miaka ya nyuma baada ya kuyumba kiuchumi.
 
Naonaga watu wanasifia sana mfumo wake wa direct injection kwamba imachanganya faster
 
naonaga watu wanasifia sana mfumo wake wa direct injection kwamba imachanganya faster
Mimi najua injini zake zina nguvu tena ukiwa kwenye RPM ya kawaida na utumiaji mzuri wa mafuta.

Ila ukiingia porini lazima uende gereji hapo ndipo watu wakazikimbia sababu ya kuua bush na bearing.
 
Mimi najua injini zake zina nguvu tena ukiwa kwenye RPM ya kawaida na utumiaji mzuri wa mafuta.

Ila ukiingia porini lazima uende gereji hapo ndipo watu wakazikimbia sababu ya kuua bush na bearing.
Tatizo la Land rover kuua bush kwa haraka kwa kweli ni kero...ukiingia tu pori kidogo lazima ukirudi ubadilishe bush zoote
 
Waasi hawataki ujinga na chuma ya mjapani! 1Hz kwa kwenda mbele 🤣🤣🤣 hadi ikazua mjadala kwanini waasi wananunua LC nyingi mno? Nani anawapa hizo gari?

Aliuliza bwana trump!
 
Kumbe hio ndio balaa lake.
Kuna Land rover moja ya shirika nilikuwa nagongea gongea kipindi fulani, kwa kweli ni gari nzuri sana upande wa engine, power ya kutosha na mafuta zinakula vizuri tofauti na Toyota pia haziyumbi barabarani.

Faida yake nyingine ni kwamba ukiwa Off-road huwezi kwama hata iweje, inapita popote pale ambapo pana upenyo wa njia.... Tatizo lake ni matunzo bhana, unaitunza kama demu vile, ukienda pori ukirudi lazima ubadilishe bush or bearings e.t.c spares zake zikiharibika hakuna kuunga unga lazma ubadilishe, ukishafungua spare hairudishiki....pia Coolant fluid ukijaza kupita kiasi inafloat mzee.... Ila ni gari nzuri sana... Hapo kwenye matunzo ndo Toyota anampiga bao
 
Wazungu wenyewe wamezishtukia 🤣🤣🤣 wako zao kwa Toyota Landcruiser, Sequoia na Tacoma
 
Wazungu wenyewe wamezishtukia [emoji1787][emoji1787][emoji1787] wako zao kwa Toyota Landcruiser, Sequoia na Tacoma
[emoji3][emoji3] ni sawa na kampuni za Tours zilizonunua Landrovers nyingi kipindi cha Utalii ukiwa juu sana, hizo gari zilikuwa zinawachefua sana zikirudi kutoka porini ni matatizo sana....ila wenye Land cruiser mkonge wanapeta tuu... Chuma inafika inapita carwash asubuhi inarudi porini tena
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…