Uchaguzi 2020 Kwanini Lissu atashinda kwa kishindo?

Uchaguzi 2020 Kwanini Lissu atashinda kwa kishindo?

Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Joined
Dec 22, 2010
Posts
17,005
Reaction score
20,425
Twende taratibu, Leo baada ya kukamilisha zoezi la kampeni kwa muda wa miezi miwili, naomba nitoe upembuzi wa kiutafiti kwanini Tundu Lissu atamshinda kwa mbali John Magufuli. Iwe kwa tume hiihii ya ccm au vyovyote lakini Lissu atashinda na atatangazwa na kuwa Rais wa Tanzania.

Tanzania katika jiografia ya kisiasa hugawanywa mapande matano makuu. Kanda ya Ziwa, Kanda ya Kaskazini, Kanda ya Pwan, Kanda ya Kati, Kanda ya Kusini na Kanda ya Nyanda za Juu Kusini.

Kanda ya Ziwa, Kanda ya Kati na Kanda ya Kusini ni eneo ambalo kwa chaguzi tano zilizopita zilisimama kama ngome muhimu za ccm, Na hata uchaguzi uliopita wa 2015 eneo hili ndiko CCM ilipata kura nyingi, na kumfanya Magufuli kuwa Rais ingawa kulikuwa na udanganyifu mkubwa wa matokeo.

Katika mzio huohuo huku Chadema ikidhibiti kanda ya Kaskazini, kanda ya Pwani, na Kanda ya Nyanda za Juu Kusini. Lakini udhibiti huu haukuwa wa kiwango kikubwa lakini ndiko ambako kijiografia Upinzani una nguvu sana.

Mwaka 2015 kulikuwa na vituo vya kupigia kura 60,000 nchi nzima, Chadema hakuwa na mtandao wa kudhibiti vituo vyote vya kupigia kura hali hiyo ilijidhihirisha katika ukusanyaji wa matokeo na utangazaji vituoni humo.

Uchaguzi wa mwaka huu umekuwa tofauti, Zilizokuwa ngome za CCM sasa katika kampeni tumeona zimekuwa ngome za Chadema, Hili halijaja kama muujiza tu, kwanza lilitanguliwa na kampeni ya Mwenyetiki Mh Freeman Mbowe iliyoitwa Bamboo Tree, hii ilikuwa ni kampeni ya Chadema ni msingi ambayo ilifanikisha kusimika Chama hadi ngazi ya chini kabisa ya vitongoji na kupata viongozi wa chama kila msingi kila mtaa na katika hilo chama kikafika nchi nzima yaani kila kitongoji kuna chadema ni msingi, na kila msingi una wanachama wasiopungua 30.

Hili lilikuwa zoezi la kimyakimya, na Magufuli alipokuja kustua alikuwa ameshachelewa ndio pigo hilo lililomfanya Magufuli aogope uchaguzi wa serikali za mitaa akauvuruga, lakini mtandao wa chama ukaendelea kusukwa kwa nguvu zote. Kosa kubwa la Magufuli ambalo linamuondoa madarakani ni yeye kuamini Katika nguvu ya kidola (ujeshi), yeye kama Mwenyekiti na Rais kapora shughuli za chama na kuzipeleka ikulu. Kwa mara ya kwanza ccm kama chama hakijashiriki uchaguzi hakina meneja kampeni wala mjibu propaganda, badala yake Rais kama taasisi ndio walioratibu na kushiriki kampeni. Magufuli akawa kampeni meneja na Mgombea yeye.

Sasa Uchaguzi huu wa 2020 kuna vituo vya kupigia kura 80,000 kwamjibu wa Tume ya Uchaguzi Tanzania, na vituo hivi vinaenda sambamba na idadi ya vitongoji ambavyo Chadema ndiko ina wanachama 30 kila kitongoji wanaotambuliwa kwa jina la Msingi.
Kwakutumia watu hao 30 kila msingi ambao ndio Kituo cha kupigia Kura, Chadema inakura za wanachama wa msingi 2.4M, Hawa wanachama 30 wanatakiwa kila mmoja kwenda na wapigakura 10. Hii inamaana kuwa kila msingi utakuwa na wanachama si chini ya 300.

Kwenye sayansi ya siasa tunaamini tabia ya mpiga kura hubadilika kila baada ya dakika 30 kulingana na mambo yanayomzunguka. Hivyo tunaamini wanachama 200 kati ya 300 waliopatikana katika kila msingi wataipigia kura Chadema.

Kwa nadharia hiyo itakuwa ni: Watu 200 x Vituo 80,000 = Jumla ni Kura 16,000,000. Hivyo hadi sasa kabla ya U Chadema ina jumla ya Kura za Wanachama wake halisi 16,000,000.

Na makadirio ya Tume ni kuwa na wapiga kura 29,000,000 sasa kwa nadharia tu ile ya wanachadema wa misingi 16,000,000 wanabaki watu 13,000,000 ambao tutagawana na ccm. Kwa msingi huo Chadema inakadiriwa kupata kura 6,000,000 kwenye hizo 13,000,000 wanazogawana na ccm na hivyo Jumla Chadema itakuwa na kura 22,000,000 zitakazofanya washinde uchagizi sawa na 93%

Kesho kila mmoja mwenye sifa ya kupiga kura akampigie kura Tundu Lissu, Zile kelele za ccm kwamba wameleta maendeleo kwa umoja wetu tuwajulishe kuwa mabarabara, Fly-overs na ndege hazipigi kura. Kura zinapigwa na Watumishi wa umma ambao kwa miaka mitano hawajapngezewa mishahara yao, Kura zinapigwa na watu wenye njaa, Kura zinapigwa na watu wasio na ajira, Kura zinapigwa na watu waliobomolewa nyumba zao bila fidia, Kura zinapigwa na watu waliotumbuliwa na kukosa haki zao, Kura zinapigwa na watu walipotelewa na ndugu zao kwakuuawa na wengine kutekwa nakupotea hadi leo.

Na Yericko Nyerere

IMG-20201026-WA0001.jpg
 
Nimeona Mayalla na mwenzie MM wamekuja na propaganda zao hapa, wanajaribu kucheza mind games kuhadaa akili za watanzania, hawajui watanzania wa leo sio wale wa mwaka 47, anyway kumbe siku hizi ni makada!.

Polepole na uongo wake nae anasema CCM ina wanachama mamilioni nchi nzima, wakati pakiitishwa mkutano wa CCM hapo nje lazima watafute malori yakasombe watu huko vijijini, kama wangekuwa na hao wanachama mamilioni kwanini wasijitokeze wa maeneo ya jirani na huo mkutano waje kujaza idadi?!

Kumbe hayo mamilioni ya Polepole nayo ni uongo mtupu, ukweli ni kwamba CCM imechokwa haina watu.
 
Teh teh teh 😂 😂😂😂😂😂 mna vituko nyie. Hebu angalia Mara mbili mkutano wenu wa mwisho wa kufunga Kampeni hapo Kawe and then rudia kusoma ulichoandika!
 
Nimeona Mayalla na mwenzie MM wamekuja na propaganda zao hapa, wanajaribu kucheza mind games kuhadaa akili za watanzania, hawajui watanzania wa leo sio wale wa mwaka 47.
Wanajichoresha tu na kujidhalilisha. Mabadiliko hayakwepeki. Na kama kuna mtu anadhani Watanzania wa leo watakuwa tayari kuishi maisha ya Kijima ya enzi za Mwalimu, basi anajidanganya.
 
We jamaa umechanganyikiwa kweli, hapo ushapata idadi ya kura kwa ushindI wa 93%, na bado unahimiza watu wakapige kura?!!, Si tayari mshashinda au hujiamini na takwimu zako?!, Kesho hamtaamini kitakachotokea, ni mitano tena kwa magufuli,
Mbowe atakuwa waziri mkuu kwenye chama cha saccoss,
emoji38.png
emoji38.png
emoji38.png
 
Uchambuzi umekaa kishabiki na sio logic... Tundu Lissu ashinde kwa asilimia 90 unadhani ni rahisi hivyo?
 
Back
Top Bottom