Uchaguzi 2020 Kwanini Lissu atashinda kwa kishindo?

Uchaguzi 2020 Kwanini Lissu atashinda kwa kishindo?

Yericko nilinunua kitabu chako na yaliyo andikwa humo ndani nilikuchulia kwa level nyingine na nilipenda sana kuona michango yako baada ya kusoma kitabu cha ili niweze kukufanyia synthesis analysis na nijue what personality are you made of ?

Asante sana nina majibu sasa.

Nimefanya study mbili na surveys mbili zote za kisiasa na kuwa funded The Bretton Woods Institution kama contribution yake kwa United Nations University, upande wa Evolution, Reform and Change. Ninao surveyors' contacts 35000 karibu kila kijiji nchi nzima.

Mpaka muda huu 12.30 PM, na contribute humu JF, mwenendo wa wapigaji kura ni kinyume mno na ulivyoandika. Leo nimetambua kelele za kuibiwa kura huanzia wapi?

Nipo Lyamungo Sinde, Machame, Hai Contituency. Nafanya Independent, Physical and Verifiable Audit ( Re Audit) for Predictive electoral voting surveys report findings.

Nitatoa majibu tarehe 30th October. Kwenye wiki la kwanza la Nov 2020 nita publish publicly, nitaku tag. .

Nilisoma novel Book na sio intellegece book from intellegent person Na kufikiri labda naweza kukitumia muda mwingine kama ref. book na kufanya hypothesis analysis na critical path management. Nakuomba usome Intellegene analysis,

1) A target centric approach, muandishi Robert M. Clerk/

2) Deception countered by Robert M. Clerk.

3) The Rise and fall of an Intellegence Discipline.
by www.cia.gov>studies>pgfs-

Pole sana umetuumiza sana tuliojaribu kuamini labda intellect yako ni nzuri sana kumbe unaweza kubahatisha na tuu.

ASANTE SANA , UKIANDIKA KITABU CHA KIUTAALAMU JIZUIE KUANDIKA VITU AMBAVYO MAJIBU YAKE HUNA UFAHAMU NAYO.

Kuna majanga makubwa sana yanaweza kutokea kwenye jamii pale ambapo tutaruhusu siasa kutumika sehemu zinazohitaji taaluma tofautitofauti

Ushauri mzuri sana huu toka kwa mkuu Magembe kwa Yeriko na wengine wanaopenda kuandika
 
Msg hii itakuwa ya kumbukumbu kwani nitakapo kuwa naiona nitakuwa nakumbukia mateso na matendo maovu yaliyofanywa na utawala wa CCM kwa kutupumbaza watz. Mungu mbariki Rais mpya ajaye kesho.
Vipi kwa sasa unakumbuka nini au ndo unaumwa kabisa?
 
Twende taratibu, Leo baada ya kukamilisha zoezi la kampeni kwa muda wa miezi miwili, naomba nitoe upembuzi wa kiutafiti kwanini Tundu Lissu atamshinda kwa mbali John Magufuli. Iwe kwa tume hiihii ya ccm au vyovyote lakini Lissu atashinda na atatangazwa na kuwa Rais wa Tanzania.

Tanzania katika jiografia ya kisiasa hugawanywa mapande matano makuu. Kanda ya Ziwa, Kanda ya Kaskazini, Kanda ya Pwan, Kanda ya Kati, Kanda ya Kusini na Kanda ya Nyanda za Juu Kusini.

Kanda ya Ziwa, Kanda ya Kati na Kanda ya Kusini ni eneo ambalo kwa chaguzi tano zilizopita zilisimama kama ngome muhimu za ccm, Na hata uchaguzi uliopita wa 2015 eneo hili ndiko CCM ilipata kura nyingi, na kumfanya Magufuli kuwa Rais ingawa kulikuwa na udanganyifu mkubwa wa matokeo.

Katika mzio huohuo huku Chadema ikidhibiti kanda ya Kaskazini, kanda ya Pwani, na Kanda ya Nyanda za Juu Kusini. Lakini udhibiti huu haukuwa wa kiwango kikubwa lakini ndiko ambako kijiografia Upinzani una nguvu sana.

Mwaka 2015 kulikuwa na vituo vya kupigia kura 60,000 nchi nzima, Chadema hakuwa na mtandao wa kudhibiti vituo vyote vya kupigia kura hali hiyo ilijidhihirisha katika ukusanyaji wa matokeo na utangazaji vituoni humo.

Uchaguzi wa mwaka huu umekuwa tofauti, Zilizokuwa ngome za CCM sasa katika kampeni tumeona zimekuwa ngome za Chadema, Hili halijaja kama muujiza tu, kwanza lilitanguliwa na kampeni ya Mwenyetiki Mh Freeman Mbowe iliyoitwa Bamboo Tree, hii ilikuwa ni kampeni ya Chadema ni msingi ambayo ilifanikisha kusimika Chama hadi ngazi ya chini kabisa ya vitongoji na kupata viongozi wa chama kila msingi kila mtaa na katika hilo chama kikafika nchi nzima yaani kila kitongoji kuna chadema ni msingi, na kila msingi una wanachama wasiopungua 30.

Hili lilikuwa zoezi la kimyakimya, na Magufuli alipokuja kustua alikuwa ameshachelewa ndio pigo hilo lililomfanya Magufuli aogope uchaguzi wa serikali za mitaa akauvuruga, lakini mtandao wa chama ukaendelea kusukwa kwa nguvu zote. Kosa kubwa la Magufuli ambalo linamuondoa madarakani ni yeye kuamini Katika nguvu ya kidola (ujeshi), yeye kama Mwenyekiti na Rais kapora shughuli za chama na kuzipeleka ikulu. Kwa mara ya kwanza ccm kama chama hakijashiriki uchaguzi hakina meneja kampeni wala mjibu propaganda, badala yake Rais kama taasisi ndio walioratibu na kushiriki kampeni. Magufuli akawa kampeni meneja na Mgombea yeye.

Sasa Uchaguzi huu wa 2020 kuna vituo vya kupigia kura 80,000 kwamjibu wa Tume ya Uchaguzi Tanzania, na vituo hivi vinaenda sambamba na idadi ya vitongoji ambavyo Chadema ndiko ina wanachama 30 kila kitongoji wanaotambuliwa kwa jina la Msingi.
Kwakutumia watu hao 30 kila msingi ambao ndio Kituo cha kupigia Kura, Chadema inakura za wanachama wa msingi 2.4M, Hawa wanachama 30 wanatakiwa kila mmoja kwenda na wapigakura 10. Hii inamaana kuwa kila msingi utakuwa na wanachama si chini ya 300.

Kwenye sayansi ya siasa tunaamini tabia ya mpiga kura hubadilika kila baada ya dakika 30 kulingana na mambo yanayomzunguka. Hivyo tunaamini wanachama 200 kati ya 300 waliopatikana katika kila msingi wataipigia kura Chadema.

Kwa nadharia hiyo itakuwa ni: Watu 200 x Vituo 80,000 = Jumla ni Kura 16,000,000. Hivyo hadi sasa kabla ya U Chadema ina jumla ya Kura za Wanachama wake halisi 16,000,000.

Na makadirio ya Tume ni kuwa na wapiga kura 29,000,000 sasa kwa nadharia tu ile ya wanachadema wa misingi 16,000,000 wanabaki watu 13,000,000 ambao tutagawana na ccm. Kwa msingi huo Chadema inakadiriwa kupata kura 6,000,000 kwenye hizo 13,000,000 wanazogawana na ccm na hivyo Jumla Chadema itakuwa na kura 22,000,000 zitakazofanya washinde uchagizi sawa na 93%

Kesho kila mmoja mwenye sifa ya kupiga kura akampigie kura Tundu Lissu, Zile kelele za ccm kwamba wameleta maendeleo kwa umoja wetu tuwajulishe kuwa mabarabara, Fly-overs na ndege hazipigi kura. Kura zinapigwa na Watumishi wa umma ambao kwa miaka mitano hawajapngezewa mishahara yao, Kura zinapigwa na watu wenye njaa, Kura zinapigwa na watu wasio na ajira, Kura zinapigwa na watu waliobomolewa nyumba zao bila fidia, Kura zinapigwa na watu waliotumbuliwa na kukosa haki zao, Kura zinapigwa na watu walipotelewa na ndugu zao kwakuuawa na wengine kutekwa nakupotea hadi leo.

Na Yericko Nyerere

View attachment 1613947
Na kaandika kitabu cha ujasusi...
.
......wajinga kweli ndo waliwao
 
Back
Top Bottom