Mheshimiwa Lissu kaingizana nchini jana kama farasi wa ngongo. Mapokezi yake tu ni ishara tosha kuwa huyu ni mtu wa namna gani kwa watu wake.
Kwenye hotuba yake mara tu baada ya kuwasili, anawaongelea waziwazi watanzania wote. Matatizo ya bei za vyakula, mzigo wa matozo na kodi ni shida kwa watanzania wote wakiwamo hawa chawa wa mama isipokuwa tu labda kwa walamba asali.
"Nani atamwunga mkono Mama na bei hizi za vyakula au msururu huu wa matozo na kodi yasiyokuwa na idadi?"
Nani atamwunga Mama mkono kwa ugumu huu wa maisha ambapo wenzetu wenye kulamba asali: mishahara, marupurupu na posho zao ni za kufuru kutokea kwenye kodi tunazokamuliwa sisi?
"Nani atamwunga Mama mkono kwenye ununuzi wa magari haya ya 400m/- plus kwa moja, kuwa ni halali kwa walamba asali na kila wanapojisikia?
Nk, nk yako mengi.
Kwani kero zote zinazotuhusu wananchi hatujawahi kuwapa orodha yote? Kwani nini wamekifanya kuziondoa au hata kuzipunguza?
"Siyo hawa waliotuelekeza kama vipi tuhamie kwingine?"
Ni wazi kuwa matatizo yetu ni ya kikatiba zaidi. Tunahitaji katiba nyingine ili raslimali na shida zetu ziwe zetu sote. Tunahitaji haki na usawa kwa wote.
Hapa ndipo ulipo ule mfupa ambao umemshinda fisi. Mfupa huu unahitaji wenye meno. Haupo uchawi, busara, sayansi wala nini.
"Anatakikana panya mwenye uthubutu wa kumfunga Paka kengele!"