Kwanini Maafisa Habari wa timu wapo juu hapa nchini

babacollins

JF-Expert Member
Joined
Dec 23, 2010
Posts
901
Reaction score
212
Miaka kadhaa iliyopita katika ligi za ulaya,hususani Uingereza, timu hazikuwa na afisa habari bali alikuwapo muandishi wa habari kutoka kwenye chombo cha habari, aliyeandamana na timu sehemu tofauti tofauti.

Kwa kuwa vyombo vya habari vinajali zaidi vichwa vya habari"vinavyouza" waandishi hao wakaacha kutafuta habari za "kiufundi" kutoka benchi la ufundi badala yake wakatafuta habari za nani kagombana na nani kwenye timu, nani haoengei na nani, nani hana furaha kwenye timu n.k.

Habari za namna hii zikivuja kutoka ndani ya timu kwa kiasi kikubwa huathiri matokeo ya timu uwanjani na hatimaye biashara za klabu. Ili kulinda maslahi mapana ya timu na klabu taratibu timu zikaanza kuwa na maafisa habari wa ndani ya timu kwa kuwa pia wapenzi wa mpira ni muhimu kupata taarifa za timu/klabu.

Pamoja na mambo mengine maafisa habari wakawa na kazi kubwa ya kuwasadia wachezaji na benchi la ufundi kwa ujumla kukabiliana na vyombo vya habari kwa kuzingatia maslahi ya timu/klabu. Hii pia ilisaidia kuwarejesha waandishi wa habari kujikita zaidi katika kulihoji benchi la ufundi mambo ya msingi na ya kiufundi ambalo haswa ndio lenye taarifa zaidi za "kimpira".

Sio bure vyombo vingi vya habari hapa nchini vinalenga kuwahoji zaidi maafisa habari kuliko makocha/benchi la ufundi kwa kuwa vyombo hivyo vinahitaji vichwa vya habari vyenye "kuuza" habari. Maafisa habari bado wataendelea kujulikana sana mpaka hapo timu/klabu zitakapo kuwa na maslahi mapana haswa ya kibiashara.

Mimi mchezaji kiongozi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…