Umeshaambiwa bima ya gari sio mkopo...bali mkopo wa benki ndo unayo hio...bima pia dhumuni la bima ya mkopo wa benki ni tofauti na bima ya gari mbona kitu kidogo sana hiki kukielewa?Akili yako kama yangu mkuu, umekata bima ya gari baada ya miaka 5 unaliuza kwa mtu mwingine ana unaachana na mambo ya magari au chombo chochote cha moto, vp hapo mleta mada unataka bima wakulipe hela yako hiyo.?
Niliwahi chukua mkopo toka benki moja (jina kapuni) na marejesho yake yalikuwa ni miaka mitatu. Baada ya mwaka mmoja, mwajiri akasitisha mkataba hivyo nikawa sina uwezo wa kulipa mkopo. Benki wakaja juu wanataka hela yao, tukakaa mezani nami nikawaambia sina kazi ya kunipa kipato cha kurejesha mkopo. Hatukuelewana, wakampa debt collector kazi ya kunidai.
Uzuri wake waliponipa mkopo walinipa na cover note ya insurance, nikampa huyo debt collector wao, nakala ya insurance cover note na barua yangu ya kuvunjwa mkataba wa kazi, nikamuomba tuonane mahakamani. Sikuwaona tena.
Ushauri wa bure: Wakikukata bima ya mkopo,wewe dai wakupe insurance cover note, likitokea la kutokea, wao wakapambane na kampuni ya bima. ILA mkopo ukiisha kwa mujibu wa mkataba, bima ya mkopo HAIRUDISHWI kwako mteja.
Katika form ulizojaza hakuna ya bima?is this true? nani ananiwekea sign huko kampuni za bima kwamba nimelipa mimi?
Mkopo ni commodity kama gari au nyumba ambavyo ukivikatia bima na hakuna tatizo hadi muda unaisha inakuwa faida ya watoaji.kwa nini, wakati hii ni bima ya mkopo? na unakuwa ushaumaliza
Bond sio bima!!hivi mkuu nikiweka bond simu kwako ukanipa 120K kwa makubaliano nikilipa deni lako na riba uliyonipa unirudishie simu yangu, nikimaliza deni utakatalia simu yangu?
Mi nimemaliza mkopo iwaje nilipe fidia ya wengine bado jibu halijakaa sawa
Mkuu google ujisomee sio unabisha tu. Mbona mie nina mkataba hapa wa mkopo na kila kitu kuhusu bima kimewekwa wazi mpk asilimia. Na mshukuru Mungu kwa hiyo bima otherwise kama hicho kipengere hakipo wangeweka kipengere cha kukata mkopo kutoka kwenye mafao yakoinaendaje bila taarifa zangu wala documentation za mhusika mkuu? yaani naanzanje kuwa mteja wa kampuni ya bima nikiwa mimi mwenyewe sijijui?
Wanakata wao sio wewe.inaendaje bila taarifa zangu wala documentation za mhusika mkuu? yaani naanzanje kuwa mteja wa kampuni ya bima nikiwa mimi mwenyewe sijijui?
hakuna siku bima inaweza kuwa kama bond.Maana hio ni kama bond endapo umetimiza matakwa yao yote una haki zote za kurudishiwa bond yako hio maana hata mahakamani ukipeleka hati kama bond kesi ikiisha unarudishiwa hati zako iweje hizo hela umerudisha na riba juu wao wasirudishe?
Mkuu upo real, nilichukua mkopo na bank Fulani. Nikaachishwa kazi, wakaniita na tukaelezana kuhusu insurance na tukaelewana. Kwa sasa insurance wanakava magepu wakinisikilizia kama nitapokea kijiti.Niliwahi chukua mkopo toka benki moja (jina kapuni) na marejesho yake yalikuwa ni miaka mitatu. Baada ya mwaka mmoja, mwajiri akasitisha mkataba hivyo nikawa sina uwezo wa kulipa mkopo. Benki wakaja juu wanataka hela yao, tukakaa mezani nami nikawaambia sina kazi ya kunipa kipato cha kurejesha mkopo. Hatukuelewana, wakampa debt collector kazi ya kunidai.
Uzuri wake waliponipa mkopo walinipa na cover note ya insurance, nikampa huyo debt collector wao, nakala ya insurance cover note na barua yangu ya kuvunjwa mkataba wa kazi, nikamuomba tuonane mahakamani. Sikuwaona tena.
Ushauri wa bure: Wakikukata bima ya mkopo,wewe dai wakupe insurance cover note, likitokea la kutokea, wao wakapambane na kampuni ya bima. ILA mkopo ukiisha kwa mujibu wa mkataba, bima ya mkopo HAIRUDISHWI kwako mteja.
Dada, kwani Bank wakimaliza deni lao wanakupokonya na kazi?Kwahiyo let's say mtu akifilisika wakimpukutisha kile kiasi ambacho hakikupatikana wanakwenda kupambana ma watu wa bima wawalipe sio?