Kwanini Mabenki hayarudishi pesa wanazokata kama " Bima ya mkopo pindi deni la mhusika linapoisha

Kwanini Mabenki hayarudishi pesa wanazokata kama " Bima ya mkopo pindi deni la mhusika linapoisha

Akili yako kama yangu mkuu, umekata bima ya gari baada ya miaka 5 unaliuza kwa mtu mwingine ana unaachana na mambo ya magari au chombo chochote cha moto, vp hapo mleta mada unataka bima wakulipe hela yako hiyo.?
Umeshaambiwa bima ya gari sio mkopo...bali mkopo wa benki ndo unayo hio...bima pia dhumuni la bima ya mkopo wa benki ni tofauti na bima ya gari mbona kitu kidogo sana hiki kukielewa?
 
Nahisi wananchi wanatakiwa kujifunza na kuelewa nini maana au dhima ya bima, ukiyajua haya hutakuwa na maswali mabaya /yakijinga
 
kiuhalisia unatakiwa lipwa/..ila mabenki hawataki ujue hili....ukifuatilia kwa banki na kampuni husika ya bima utapata unachostahili....angalizo yoyote anayekukatalia haki yako omba kuongea na boss wake hadi utamfikia anayehusika....najibu kwa uzoefu
 
Kwahiyo let's say mtu akifilisika wakimpukutisha kile kiasi ambacho hakikupatikana wanakwenda kupambana ma watu wa bima wawalipe sio?
Niliwahi chukua mkopo toka benki moja (jina kapuni) na marejesho yake yalikuwa ni miaka mitatu. Baada ya mwaka mmoja, mwajiri akasitisha mkataba hivyo nikawa sina uwezo wa kulipa mkopo. Benki wakaja juu wanataka hela yao, tukakaa mezani nami nikawaambia sina kazi ya kunipa kipato cha kurejesha mkopo. Hatukuelewana, wakampa debt collector kazi ya kunidai.

Uzuri wake waliponipa mkopo walinipa na cover note ya insurance, nikampa huyo debt collector wao, nakala ya insurance cover note na barua yangu ya kuvunjwa mkataba wa kazi, nikamuomba tuonane mahakamani. Sikuwaona tena.

Ushauri wa bure: Wakikukata bima ya mkopo,wewe dai wakupe insurance cover note, likitokea la kutokea, wao wakapambane na kampuni ya bima. ILA mkopo ukiisha kwa mujibu wa mkataba, bima ya mkopo HAIRUDISHWI kwako mteja.
 
Ndio mara ya kwanza kusikia BIMA inakuwa refunded. Rejea kwenye vyombo vya Moto.
 
Mimi nilikopa kwa miaka 3 mfulurizo mkopo wa mwaka mmoja mmoja na kila nilipokuwa nakaribia kumaliza basi rejesho la mwisho nilikuwa napiga simu kwa Afisa wangu kwamba wakate kule.
Makubaliano ya Bima ya mkopo ilikuwa ni kuweka pesa ya rejesho moja, sasa sijui kwako mlikubaliana vipi, endelea kufatilia utapata jibu sahihi.
 
Kwa nn DG hajibu E-mail za Mteja wao?
 
Hiyo pesa ya bima hairudishwi. Ingekuwa inarudishwa unafikiri bima ingejiendeshaje?. Unafikiri wenyewe wapo kwa ajili ya kukulinda wewe tu upate ajali ndio wakulipe hela ulizoingia hasara?. Faida yao ya uwepo wao ndio hiyo wewe usipopata ajali,yaani wewe uweke laki 2 kwa kinga ya mamilioni yako ya pesa,bila wao kupata faida?. Bima yoyote unapokata hurudushiwi. Hata hizi bima za magari ziko hivyo. Mfano hizi za magari tunalipia kila mwaka. Kwa mantiki yako unahisi gari mpaka likapokufa kabisa halitembei tena utarudishiwa hela yako yote?. Wala usijihangaishe tena kuidai hiyo hela. Bima yoyote ukiilipia hakuna kinachorudi. Kitarudi tu ukipata hasara hapo katikati
 
kwa nini, wakati hii ni bima ya mkopo? na unakuwa ushaumaliza
Mkopo ni commodity kama gari au nyumba ambavyo ukivikatia bima na hakuna tatizo hadi muda unaisha inakuwa faida ya watoaji.
 
hivi mkuu nikiweka bond simu kwako ukanipa 120K kwa makubaliano nikilipa deni lako na riba uliyonipa unirudishie simu yangu, nikimaliza deni utakatalia simu yangu?
Bond sio bima!!
 
Pesa ya bima hairudushwi kwa kuwa kanuni ya bima ni watu kuchangia na mmoja wapo akipata janga ile michango ya wenzake ndio inaenda ku cover janga. Kwani bima ya afya usipoumwa kwa huo mwezi unarudishiwa. Soma kuhusu bima utaelewa
 
inaendaje bila taarifa zangu wala documentation za mhusika mkuu? yaani naanzanje kuwa mteja wa kampuni ya bima nikiwa mimi mwenyewe sijijui?
Mkuu google ujisomee sio unabisha tu. Mbona mie nina mkataba hapa wa mkopo na kila kitu kuhusu bima kimewekwa wazi mpk asilimia. Na mshukuru Mungu kwa hiyo bima otherwise kama hicho kipengere hakipo wangeweka kipengere cha kukata mkopo kutoka kwenye mafao yako
 
Maana hio ni kama bond endapo umetimiza matakwa yao yote una haki zote za kurudishiwa bond yako hio maana hata mahakamani ukipeleka hati kama bond kesi ikiisha unarudishiwa hati zako iweje hizo hela umerudisha na riba juu wao wasirudishe?
hakuna siku bima inaweza kuwa kama bond.
1. Bima ya mkopo haitumiki kucover mkopo endapo mteja atashindwa lipa mkopo.
2. Bima ya mkopo kamwe haiwezi rudishwa.
3. Bima inapelekwa ya kampuni ya bima, endapo itatokea maafa kama kifo kwa mdaiwa basi itakuwa jukumu la kampuni ya bima kulipa mkopo uliobaki.
 
Niliwahi chukua mkopo toka benki moja (jina kapuni) na marejesho yake yalikuwa ni miaka mitatu. Baada ya mwaka mmoja, mwajiri akasitisha mkataba hivyo nikawa sina uwezo wa kulipa mkopo. Benki wakaja juu wanataka hela yao, tukakaa mezani nami nikawaambia sina kazi ya kunipa kipato cha kurejesha mkopo. Hatukuelewana, wakampa debt collector kazi ya kunidai.

Uzuri wake waliponipa mkopo walinipa na cover note ya insurance, nikampa huyo debt collector wao, nakala ya insurance cover note na barua yangu ya kuvunjwa mkataba wa kazi, nikamuomba tuonane mahakamani. Sikuwaona tena.

Ushauri wa bure: Wakikukata bima ya mkopo,wewe dai wakupe insurance cover note, likitokea la kutokea, wao wakapambane na kampuni ya bima. ILA mkopo ukiisha kwa mujibu wa mkataba, bima ya mkopo HAIRUDISHWI kwako mteja.
Mkuu upo real, nilichukua mkopo na bank Fulani. Nikaachishwa kazi, wakaniita na tukaelezana kuhusu insurance na tukaelewana. Kwa sasa insurance wanakava magepu wakinisikilizia kama nitapokea kijiti.
Ningemaliza mkopo, Deni lisingewahusu. Tuchukue mfano wa nyumba na Gari na insurance.
 
Kwahiyo let's say mtu akifilisika wakimpukutisha kile kiasi ambacho hakikupatikana wanakwenda kupambana ma watu wa bima wawalipe sio?
Dada, kwani Bank wakimaliza deni lao wanakupokonya na kazi?
 
Back
Top Bottom