Niliwahi chukua mkopo toka benki moja (jina kapuni) na marejesho yake yalikuwa ni miaka mitatu. Baada ya mwaka mmoja, mwajiri akasitisha mkataba hivyo nikawa sina uwezo wa kulipa mkopo. Benki wakaja juu wanataka hela yao, tukakaa mezani nami nikawaambia sina kazi ya kunipa kipato cha kurejesha mkopo. Hatukuelewana, wakampa debt collector kazi ya kunidai.
Uzuri wake waliponipa mkopo walinipa na cover note ya insurance, nikampa huyo debt collector wao, nakala ya insurance cover note na barua yangu ya kuvunjwa mkataba wa kazi, nikamuomba tuonane mahakamani. Sikuwaona tena.
Ushauri wa bure: Wakikukata bima ya mkopo,wewe dai wakupe insurance cover note, likitokea la kutokea, wao wakapambane na kampuni ya bima. ILA mkopo ukiisha kwa mujibu wa mkataba, bima ya mkopo HAIRUDISHWI kwako mteja.