Kwanini Mabenki hayarudishi pesa wanazokata kama " Bima ya mkopo pindi deni la mhusika linapoisha

Ndo leo nasikia eti bima inarudishwa. Ina maana utakuwa bima ni nini? Bima sio deposit. Hiyo pesa inakuwa imeshachukuliwa na Insurer. Ni sawa uende uakadai bima ya afya makato yako sababu hukuumwa mwaka mzima. Si wehu huo.
 
Mkuu tafadhari tofautisha bima ya mkopo na hizi bima zingine.... Inawezekana na wewe ukawa mwehu mkuu
 
hivi mkuu nikiweka bond simu kwako ukanipa 120K kwa makubaliano nikilipa deni lako na riba uliyonipa unirudishie simu yangu, nikimaliza deni utakatalia simu yangu?

Huu mfano wako hauendani, bima wao wamechukua risk ya kulipa mkopo wa 5M(mfano) km ikitokea umeshindwa kulipa, sasa ukisema wakulipe faida yao ni nini? Maana yake hiyo 200k ni gharama ya wao kubeba risk ya kulipia hilo deni Incase umeshindwa kulipa. Na hiyo ndo biashara ya bima ilivyo
 
Asante, nafikiri wengi hawaelewi maana ya bima.
 
Sio kwamba ukifariki au kupata tatizo deni halijaisha wanakata kwenye mafao?
 
sijawahi sikia bima inarudisha fedha kama janga lilitegemewa halija tokea, mfano mimi nikikata bima ya gari na gari yangu ikawa haija pata ajali hadi inachakaa unataka nirudishiwe pesa si ndo hivyo
 
sijawahi sikia bima inarudisha fedha kama janga lilitegemewa halija tokea, mfano mimi nikikata bima ya gari na gari yangu ikawa haija pata ajali hadi inachakaa unataka nirudishiwe pesa si ndo hivyo
Hapana mkuu bima ya mkopo na gari tofauti.... Hebu soma terms and conditions zao....
 
،ukiniuliza faida yao ni nini, nashindwa kukuelewa maana Mimi sikuingia mkataba na wa watu WA bima na wala sikuwahi kuonana nao, niliingia mkataba na bank na wao wana wajibu wa
 
ndio mkuu lazma warudishe, vinginevyo watakuwa wanawaibia wateja wao
ndio maana kuna baadhi ya wanawachuoni wa kiislamu wanatoa fatwa kwamba bima za namna hiyo ni haramu kwa sababu BIMA NI KAMARI YA KISASA HIYO.

ukiwa halijatokea haki kila mtu apate pesa yake, lakini dhulma ni kuwa hata kama halikutokea pesa hairudi, ni kama kamari y biko na mzuka tu
 
Nakushauri hili bandiko lako lipeleke pia Twitter, kwani ni issue muhimu sana na kule Twitter CRDB wana account yao na wanajibu papo kwa papo maswali ya wateja...
 
Nakushauri hili bandiko lako lipeleke pia Twitter, kwani ni issue muhimu sana na kule Twitter CRDB wana account yao na wanajibu papo kwa papo maswali ya wateja...
Sawa mkuu
 
hivi mkuu nikiweka bond simu kwako ukanipa 120K kwa makubaliano nikilipa deni lako na riba uliyonipa unirudishie simu yangu, nikimaliza deni utakatalia simu yangu?
Tofautisha kati ya bima na kuweka kitu kama dhamana(bond).

Bima hairudishwi kama tatizo halijatokea.
Ukipata tatizo wanalipa pesa nyingo kuliko uliyolipua bima, sasa jiulize hiyo pesa wanatoa wapi na faida wanatoa wapi?

Bima ni kama biashara ya bahati nasibu/kamari(betting) au kama forex trading au biashara ya stock market.
 
hivi mkuu nikiweka bond simu kwako ukanipa 120K kwa makubaliano nikilipa deni lako na riba uliyonipa unirudishie simu yangu, nikimaliza deni utakatalia simu yangu?
Bima sio bond.

Hivi zile bima za magari huwa wanaturudishia muda wake ukimalizika?
 
Unaweza fikiria humu tuna watu wengi ambao ama hawajaenda kabisa shule na pia sio hata watumishi.

Lakini unanakuta wanaolalamika ndiyo watu wanaokatwa NHIF lakin huwaoni wakidai.

Itabidi bima ifundishwe kama somo walau kuanzia darasa 5.
 
Bima katika mikopo ni nzuri sana.

Jirani yangu alikopa kama 30m, baada ya miezi 3 akafariki.

Tulipopeleka cheti cha kifo benki haikumdai mke wa marehemu na nyumba yao waliyoweka bond ikasalimika.

Mama na watoto wakabaki salama na mtaji umeongezeka dukani.

Shikamoo bima.
 
Mkopo ni sheria msikubali makubaliano ya mdomo bila maandishi, ikiwa hakuna documentation hilo deni una liwasilishaje sasa?! Unalipia hupewi receipt na haiko kwenye mkataba wa deni sasa unalipaje na una daije?!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…