Kwanini Mabenki hayarudishi pesa wanazokata kama " Bima ya mkopo pindi deni la mhusika linapoisha

Kwanini hiyo processing fee wasiijumlishe kwenye riba wanayotoza?
 
is this true? nani ananiwekea sign huko kampuni za bima kwamba nimelipa mimi?
Hapa kinachoonekana Kuna kaujanja wanakafanya hao watu wa benki.
Kwa sababu hao ndio wanafahamiana na watu wa bima kwa hiyo Mimi mkopaji sihusiki na kulipa bima inatakiwa watu wa benki ndio walipe hiyo pesa ya bima kwa sababu hao ndio wenye wasiwasi wa kupotea kwa pesa yao iliyokopwa na mteja Basi ni jukumu lao kulipia bima.
Ila kwa vile wabongo huwa hatufuatilii sheria utakuta unakubali kwa haraka haraka kila sharti utakalopewa kwa sababu ya kuharakisha kuipata pesa ya mkopo na hapo ndio watu wa benki wanacheza na hiyo weakness.
 
Reactions: Ctr
Niongezee kitu kingine; unapokatwa credit life premium unatakiwa kujazishwa terms and conditions za hizo insurance.

Ikitokea hujajaza haimanishi cover haipo ila inamanisha benki wamekusanya hizo premiums wakaenda kukata kwa niaba. Lakini there must be a clause in the documentations you have signed kuonesha ulilipia credit life.
Alternatively, benki inaweza kukuambia tutahitaji uwe na credit life insurance kwa hiyo nenda kakata unapotaka wewe then tuletee cover note ikiwa umeweka benki kama part ya beneficiary kwenye proceeds za insurance

Wengine wana life insurance zao binafsi so wanaweza pia kuweka benki kama beneficiary wa hizo proceeds zao pia ingawa ni lazima wafuatilie kujua kama ina room ya kutosha
 
Bima ni bahati nasibu,wanacheza mchezo was kupata au kukosa. Kumbuka bima ya mkopo, inaaply tu ukifariki kabla hujamaliza kulipa mkopo. Ukishindwa kulipa na upo hai amana yako inauzwa. Niambie mbona unapobet ukikosa hudai?
 
Tangu lini bima ikarudishwa? Kwa wale wanaotumia bima ya afya watanielewa Bima ni mchango ambao hutolewa kabla kwa lengo la kutatua jambo husika endapo litatokea na ikumbukwe mteja anaweza pata tatizo ambalo litagharimu fedha nyingi kuliko kiasi alicho changia, hapa inamaanisha bima ni mchango ambao kwa namna unavyo fanya kazi inategemea michango ya wengi kutatua matatizo ya wachache! So Bima its some inafanana kidogo na gumbling
 
Ukikata bima ya moto au ya gari na gari isipate ajali mwaka huo ,unarudishiwa hela yako? Sijawahi kuona. Kila mwaka tunalipia hata kama hatujapata ajali
 
Uko sawa mkuu. umeelimisha vyema
 
bima ya afya na hii na bima ya mkopo ni vitu viwili tofauti mkuu.
kinachoonekana wabongo wengi tunachukulia vitu kirahisi sana na ndio maana wajanja wanatumia huo mwanya kutengeneza pesa Kuna, unavyokopa Bank ndio wanaingia mkataba na bima na Kwa sababu hao ndio wanafahamiana kwa hiyo Mimi mkopaji nisingetakiwa kuhusika na kulipa bima inatakiwa watu wa benki ndio walipe hiyo pesa ya bima kwa sababu hao ndio wenye wasiwasi wa kupotea kwa pesa yao iliyokopwa na mteja Basi ni jukumu lao kulipia bima.

Ila kwa vile wabongo huwa hatufuatilii masuala muhimu yanayotuhusu utakuta unakubali kwa haraka haraka kila sharti utakalopewa kwa sababu ya kuharakisha kuipata pesa ya mkopo na hapo ndio watu wa benki wanacheza na hiyo weakness.
 
Ukikata bima ya moto au ya gari na gari isipate ajali mwaka huo ,unarudishiwa hela yako? Sijawahi kuona. Kila mwaka tunalipia hata kama hatujapata ajali
Ukikata bima ya moto au ya gari na gari isipate ajali mwaka huo ,unarudishiwa hela yako? Sijawahi kuona. Kila mwaka tunalipia hata kama hatujapata ajali
bima ya gari na hii na bima ya mkopo ni vitu viwili tofauti mkuu.
kinachoonekana wabongo wengi tunachukulia vitu kirahisi sana na ndio maana wajanja wanatumia huo mwanya kutengeneza pesa Kuna, unavyokopa Bank ndio wanaingia mkataba na bima na Kwa sababu hao ndio wanafahamiana kwa hiyo Mimi mkopaji nisingetakiwa kuhusika na kulipa bima inatakiwa watu wa benki ndio walipe hiyo pesa ya bima kwa sababu hao ndio wenye wasiwasi wa kupotea kwa pesa yao iliyokopwa na mteja Basi ni jukumu lao kulipia bima.

Ila kwa vile wabongo huwa hatufuatilii masuala muhimu yanayotuhusu utakuta unakubali kwa haraka haraka kila sharti utakalopewa kwa sababu ya kuharakisha kuipata pesa ya mkopo na hapo ndio watu wa benki wanacheza na hiyo weakness.
 
Nakubaliana na wewe mkuu lakini bado nadhani haya mabank yanatupiga hapa na kwa vile Akili za wabongo wengi zinachukulia vitu kirahisi sana na ndio maana wajanja wanatumia huo mwanya kutengeneza pesa , kama ulivyosema unavyokopa Bank ndio wanaingia mkataba na bima na Kwa sababu hao ndio wanafahamiana kwa hiyo Mimi mkopaji nisingetakiwa kuhusika na kulipa bima inatakiwa watu wa benki ndio walipe hiyo pesa ya bima kwa sababu hao ndio wenye wasiwasi wa kupotea kwa pesa yao iliyokopwa na mteja Basi ni jukumu lao kulipia bima.

Ila kwa vile wabongo huwa hatufuatilii masuala muhimu yanayotuhusu utakuta unakubali kwa haraka haraka kila sharti utakalopewa kwa sababu ya kuharakisha kuipata pesa ya mkopo na hapo ndio watu wa benki wanacheza na hiyo weakness.
 
ujinga ni kujifanya unajua kila kitu mkuu
kinachoonekana wabongo wengi ukiwemo wewe tunachukulia vitu kirahisi sana na ndio maana wajanja wanatumia huo mwanya kutengeneza pesa Kuna, unavyokopa Bank ndio wanaingia mkataba na bima na Kwa sababu hao ndio wanafahamiana kwa hiyo Mimi mkopaji nisingetakiwa kuhusika na kulipa bima inatakiwa watu wa benki ndio walipe hiyo pesa ya bima kwa sababu hao ndio wenye wasiwasi wa kupotea kwa pesa yao iliyokopwa na mteja Basi ni jukumu lao kulipia bima.

Ila kwa vile wabongo huwa hatufuatilii masuala muhimu yanayotuhusu utakuta unakubali kwa haraka haraka kila sharti utakalopewa kwa sababu ya kuharakisha kuipata pesa ya mkopo na hapo ndio watu wa benki wanacheza na hiyo weakness.
 
Mkuu, unajua lakini bima inavyofanya kazi?. Maana naona unachanganya mambo hapa na si vinginevyo.

Bima inafanya kazi kama sehemu ya kumitigate/kuzia risks/majanga endapo tukio fulani litajitokeza na kuathiri mali ya yule anayekata bima. Ukiingia ndani zaidi ni kwamba bima zinafanya kazi katika utaratibu wa kukusanya fedha kidogo kidogo toka kwa watu wengi na kisha kuwafidia wale watakao pata matatizo katika kipindi bima ikiwa hai/valid.

Tafsiri yao sio wote watapata majanga kwa mara moja, na wakati mwingine miongoni mwa wengi ni wachache tu ndio watakaopata majanga katika kipindi cha uhai wa bima, hivyo hawa wachache watalipwa kutokana na kile ambacho kililipwa na wengi.

Unachopaswa kujua bima ni biashara, na bima ni shughuli inayoitaji utaalamu wa juu sana. Usiichukulie kwa lugha za mtaani kuwa bima ni kuweka bondi/dhamana. Hivi ni vitu viwili tofauti kwa muktadha wa masuala ya fedha.

Nikirudi kwenye mada yako, katika hali ya kawaida kabisa na wewe ukiwa ni muelewa, ulikopa huo mkopa na kisha ukakatiwa bima ya mkopo kama unavyosema 200k. Assume ni mkopo tu hata wa milioni 5. Ukalipa marejesho mawili, bahati mbaya ukapata ulemavu wa kudumu/total disability au ukafariki dunia. Kwa akili ya kawaida, deni lililobaki nani anapaswa kulipa?.

Jibu ni rahisi. Taratibu zitafuatwa kuhakikisha taarifa muhimu za marehemu/mlemavu zinapatikana na kisha benki wataenda kudai/claim kiasi chote cha mkopo pamoja na riba kilichobaki kutoka shirika la bima. Bima wakiona kila kitu kiko sawa basi watawalipa benki fedha yao. Na benki haitokaa imsumbue aliyepata majanga au ndugu za marehemu juu ya ulipaji wa deni husika. Huu ndo utaratibu unaotumika na ni lugha nyepesi kabisa jinsi bima inavyofanya kazi.

Mifano ni mingi, watu wanakata comprehensive insurance/bima kubwa tuseme kwa gari ya milioni 20, mfano analipa milioni + kama ada ya bima/premium. Mtu huyu huyu gari ikipata mzinga na ikawa total loss, analipwa fedha inayolingana na thamani ya gari (aliyoitaja bima kipindi anakata bima) toa uchakavu. Tuchukulie mtu kalipwa na bima milioni 15. Sasa jiulize, kwamba hizo zingine wamezitoa wapi mpaka wakaweza mlipa.

Kwa kifupi fedha ya bima huwa hairudishwi, na bima ya mkopo iko kihalali ili kulinda/safeguards maslahi ya pande zote mbili endapo majanga yatatokea.

Mwisho kabisa kumbuka fedha iliyoko benki ni akiba za watu hivyo wakati wowote zinapaswa kuwa salama hata kama zitatumika kukopeshwa.
 
hivi mkuu nikiweka bond simu kwako ukanipa 120K kwa makubaliano nikilipa deni lako na riba uliyonipa unirudishie simu yangu, nikimaliza deni utakatalia simu yangu?
Ufafanuzi hivi hii ni kitu mfano mtu unaandika 300k K husimama badala ya nini ? Naomba kufahamu chief
 
Umeelezea vzuri sana kiongozi,
Swali langu,je bima wanalipa pia kwa mtu aliyeacha kazi bila kufuata tatatibu(kutoroka)?
Na Je,Bima wanafanya kazi pia na taasisi ndogo ndogo za kifedha i.e Bayport and the like?
 
Umeelezea vzuri sana kiongozi,
Swali langu,je bima wanalipa pia kwa mtu aliyeacha kazi bila kufuata tatatibu(kutoroka)?
Na Je,Bima wanafanya kazi pia na taasisi ndogo ndogo za kifedha i.e Bayport and the like?
Katika hali ya kawaida kabisa kila bima ina vitu inavyokinga na hii kiuhalisia ndio mipaka ya bima husika. Bima ya mkopo au mara nyingi huitwa credit life insurance ni bima inayokatwa dhidi ya majanga kama kifo au ulemavu wa kudumu kama vitamkumba yule anayekatiwa bima/insured.

Swala la mtu kuacha kazi au kutoroka bima huwa haihusiki maana sio sehemu ya makubaliano ya bima husika. Ziko bima mfano zinazokinga upotevu wa fedha dhidi ya wafanyakazi ulio waajiri, zipo bima zinazolinda bidhaa/stocks zilizoko dukani dhidi ya majanga kama moto na mengine ya asili/natural calamities n.k.

Scope/wigo wa bima husika ndio utatoa majibu ya risks/majanga gani ambayo bima hukinga na yapi haihusiki.

Sijui kama nimekujibu ipasavyo
 
Kiongozi hakuna bima ya kukatwa kwa maneno, unapaswa ujue hilo. Mimi nadhani ni vyema watu tujifunze au kuuliza kuliko kuyasemea mambo yaliyo ya kitaalam kwa kuchanganya na story za huko mtaani.

Bima ni mkataba kati ya pande mbili au zaidi. Kama ni mkataba basi tunategemea pawe na maandishi au aina ya risiti zinazo tuonyesha kuwa mkataba huu ni baina ya fulani na fulani, kwa kipindi cha muda fulani, na mkataba huu ni juu ya majanga fulani fulani. Lengo la kuwa na mkataba huu ni kulinda maslahi ya pande zote mbili, moja kampuni ya bima ili kama litazuka jambo lililo nje ya majanga mliyo kubaliana basi wawe na haki kisheria ya kutokulipa. Pili ni kwa mkata bima husika, ili pindi apatapo majanga awe na mamlaka kisheria ya kupatiwa huduma/haki zinazoendana na mkataba walio ingia hapo awali.

Sasa kwenye bima kuna mkataba ambao mteja hupewa, hii document/nyaraka huitwa cover note. Hii inabeba taarifa zote za msingi za mkataba ulio ingiwa. Nyaraka hii ndio kielelezo kuwa mtu X alikata bima kwenye kampuni Y, na sasa mtu X amefariki akiwa na mkopo wa benki Z. Hivyo miongoni mwa viambatanisho ambavyo benki Z itapeleka kwenye kampuni Y ya bima ni pamoja na Insurance Cover Note. Ni MUHIMU pia kujua kuwa kwa bima yoyote itayokatwa kwa ajili ya kuhusisha mkopo wa taasisi ya fedha basi taasisi hiyo itatambulika kama mnufaika wa kwanza/FIRST LOSS PAYEE endapo janga litatokea. Hii inaweza ikawa ni bima ya gari au hata nyumba kama chombo/kitu husika kimetumika kama dhamana ya mkopo kwenye taasisi ya fedha/benki.


Kitaalamu kabisa Insurance Cover Note ya credit life ni miongoni mwa nyaraka muhimu sana ambazo huhifadhiwa pamoja na mikataba mingine ya mkopo.

Nililo liona hapo ni mteja labda hakupewa elimu ya kutosha kuhusu matumizi sahihi ya bima ya mkopo, na pia inawezekana hakupewa nakala ya bima ya mkopo pia.

Nadhani nitakuwa nime eleweka.
 
Hichi unacho kizungumza hakipo mkuu. Labda kama walicho kurudishia ni aina fulani ya tozo waliyoifanya wakati wa kukupa mkopo, na mwisho ukilipa na kumaliza basi wanarudisha.

Mfano, waweza ongea na mteja kuhold/kuzuia rejesho moja la kwanza la mkopo kutoka kwenye fedha ambayo unampa kama mkopo. Hii inaweza kufanyika endapo tarehe za kuchukua mkopo zikawa zimekaribia na tarehe za mshahar kutoka hivyo kufanya makato yashindwe kuanza mwezi husika.

Baada ya kufanya hivyo, mteja anaweza endelea lipa mkopo wake kwa utaratibu wa kawaida, akifika mwisho anajikuta mkopo wake umekwisha ila kuna rejesho moja kalipa zaidi. Fedha hii ndiyo mteja hurudishiwa kwenye akaunti. Wengine wanaweza wakairudisha mapema kabisa baada ya rejesho la kwanza kutoka kwenye mshahara wako kama litakuja kwa wakati. Hivyo kukwepa adha ya wewe kuisubiri fedha yako mpaka umalize mkopo ndo ulipwe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…