Kwanini Mabenki hayarudishi pesa wanazokata kama " Bima ya mkopo pindi deni la mhusika linapoisha

Kiongozi, nadhani kiuhalisia watu wengi hawajui kazi za bima, inawezekana nawe ukiwa mmoja wao. Bima ya gari sio bima ya mkopo. Lakini unachopaswa kujua ni nini dhumuni la bima. Kwanini bima zilianzishwa bila kujali ni ya gari, meli, mkopo n.k.

Mfano, kwa muktadha wa bima ya gari yaweza kuwa bima ndogo/ 3rd party au ikawa bima kubwa/comprehensive insurance. Kwa sheria za nchi ya Tanzania chombo chochote cha moto kinapaswa kuwa na bima, na sheria inasema wazi angalau/at least 3rd party insurance. Sasa ukiliangalia hili kwa mapana ni kwamba wanasema walau bima ndogo/3rd party insurance kwa sababu hii ni bima inayowakinga watumiaji wengine wa barabara dhidi ya madhara yatakayo sababishwa na chombo chako pindi kikiwa barabarani (hapa mkataba utaanisha ni mambo gani na kwa kiasi gani bima wataweza wafidia watakao athiriwa). Ukija kwenye comprehensive insurance/bima kubwa basi utagundua hii inakinga yote ya bima ndogo pamoja na chombo chenyewe.

Sasa mtu huyu aliyekata bima kubwa au ndogo kwa mwaka na mpaka inaisha muda wake hajapatwa na janga lolote, anaweza kwenda kudai fedha ile?. Jibu ni hapana. Vivo hivyo mtu yule aliyekata bima ya mkopo (kuulinda mkopo dhidi ya majanga yaliyo ainishwa) na akalipa mkopo wake mpaka mwisho bila ya majanga yale kutokea, je atalipwa fedha zake?. Jibu pia ni hapana.
Umeshaambiwa bima ya gari sio mkopo...bali mkopo wa benki ndo unayo hio...bima pia dhumuni la bima ya mkopo wa benki ni tofauti na bima ya gari mbona kitu kidogo sana hiki kukielewa?
 
Nimekuelewa kwa upande wa swali langu kipengele cha kwanza...
Lakn cha pili hujajbu,kuhusiana na taasisi ndogo za kifedha.
 
Nimekuelewa kwa upande wa swali langu kipengele cha kwanza...
Lakn cha pili hujajbu,kuhusiana na taasisi ndogo za kifedha.
Kiongozi, kwa kuzingatia umuhimu wa bima ya mkopo kulingana na kazi inazofanya naamini wanaitumia pia.

Unachopaswa kujua ni kwamba hamna mkopeshaji yuko tayari kuona fedha yake inapotea hata kama mkopaji atafariki au kupata ulemavu wa kudumu. Lengo la bima ya mkopo ni kuondoa usumbufu kwa mkopaji au ndugu wa marehemu lakini pia kuhakikisha kuwa fedha ya mkopeshaji inabaki salama.

Taasisi yoyote ya fedha iliyo smart ni lazima itumie huduma hii, maana inaweka heshima ya taasisi katika jamii/kutochukua mali au kulazimisha ndugu wa marehemu kulipa na pia taasisi kulinda fedha zake.

Saccos nyingi tu kwa mfano zinazokopa mikopo kwenye mabenki mara nyingi wanalazimika kwa wanachama wao kukatiwa bima ya mkopo pia, ili kupunguza mzigo endapo mwanachama wao atafariki.
 
Asante kwa ufafanuzi mzuri kiongozi.
 
Kwa wenzetu inarudishwa, bongo hairudi!
Ngoja tutafute aliyepewa dhamana ya kurekebisha hali hii. Ikionekana wanatuibia inabidi wote tuliofanyiwa dhuruma tukaidai fidia mahakamani. Wanaweza filisika eti!
 
Hio Bima wanalipa kampuni za bima ambazo incase of death or permanent disability bima wanailipa bank. Sasa nazani kwa hapa tz no refund
 
Hela ya bima huwa hairudishwi. Ni kama kukatia gari bima, unaweza ukalipia bima hata miaka 10 bila kupata ajali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…