nerilan
JF-Expert Member
- Dec 11, 2013
- 454
- 691
Kiongozi, nadhani kiuhalisia watu wengi hawajui kazi za bima, inawezekana nawe ukiwa mmoja wao. Bima ya gari sio bima ya mkopo. Lakini unachopaswa kujua ni nini dhumuni la bima. Kwanini bima zilianzishwa bila kujali ni ya gari, meli, mkopo n.k.
Mfano, kwa muktadha wa bima ya gari yaweza kuwa bima ndogo/ 3rd party au ikawa bima kubwa/comprehensive insurance. Kwa sheria za nchi ya Tanzania chombo chochote cha moto kinapaswa kuwa na bima, na sheria inasema wazi angalau/at least 3rd party insurance. Sasa ukiliangalia hili kwa mapana ni kwamba wanasema walau bima ndogo/3rd party insurance kwa sababu hii ni bima inayowakinga watumiaji wengine wa barabara dhidi ya madhara yatakayo sababishwa na chombo chako pindi kikiwa barabarani (hapa mkataba utaanisha ni mambo gani na kwa kiasi gani bima wataweza wafidia watakao athiriwa). Ukija kwenye comprehensive insurance/bima kubwa basi utagundua hii inakinga yote ya bima ndogo pamoja na chombo chenyewe.
Sasa mtu huyu aliyekata bima kubwa au ndogo kwa mwaka na mpaka inaisha muda wake hajapatwa na janga lolote, anaweza kwenda kudai fedha ile?. Jibu ni hapana. Vivo hivyo mtu yule aliyekata bima ya mkopo (kuulinda mkopo dhidi ya majanga yaliyo ainishwa) na akalipa mkopo wake mpaka mwisho bila ya majanga yale kutokea, je atalipwa fedha zake?. Jibu pia ni hapana.

Umeshaambiwa bima ya gari sio mkopo...bali mkopo wa benki ndo unayo hio...bima pia dhumuni la bima ya mkopo wa benki ni tofauti na bima ya gari mbona kitu kidogo sana hiki kukielewa?