Kwanini Mabenki hayarudishi pesa wanazokata kama " Bima ya mkopo pindi deni la mhusika linapoisha

Kwanini Mabenki hayarudishi pesa wanazokata kama " Bima ya mkopo pindi deni la mhusika linapoisha

Kiongozi, nadhani kiuhalisia watu wengi hawajui kazi za bima, inawezekana nawe ukiwa mmoja wao. Bima ya gari sio bima ya mkopo. Lakini unachopaswa kujua ni nini dhumuni la bima. Kwanini bima zilianzishwa bila kujali ni ya gari, meli, mkopo n.k.

Mfano, kwa muktadha wa bima ya gari yaweza kuwa bima ndogo/ 3rd party au ikawa bima kubwa/comprehensive insurance. Kwa sheria za nchi ya Tanzania chombo chochote cha moto kinapaswa kuwa na bima, na sheria inasema wazi angalau/at least 3rd party insurance. Sasa ukiliangalia hili kwa mapana ni kwamba wanasema walau bima ndogo/3rd party insurance kwa sababu hii ni bima inayowakinga watumiaji wengine wa barabara dhidi ya madhara yatakayo sababishwa na chombo chako pindi kikiwa barabarani (hapa mkataba utaanisha ni mambo gani na kwa kiasi gani bima wataweza wafidia watakao athiriwa). Ukija kwenye comprehensive insurance/bima kubwa basi utagundua hii inakinga yote ya bima ndogo pamoja na chombo chenyewe.

Sasa mtu huyu aliyekata bima kubwa au ndogo kwa mwaka na mpaka inaisha muda wake hajapatwa na janga lolote, anaweza kwenda kudai fedha ile?. Jibu ni hapana. Vivo hivyo mtu yule aliyekata bima ya mkopo (kuulinda mkopo dhidi ya majanga yaliyo ainishwa) na akalipa mkopo wake mpaka mwisho bila ya majanga yale kutokea, je atalipwa fedha zake?. Jibu pia ni hapana.
Umeshaambiwa bima ya gari sio mkopo...bali mkopo wa benki ndo unayo hio...bima pia dhumuni la bima ya mkopo wa benki ni tofauti na bima ya gari mbona kitu kidogo sana hiki kukielewa?
 
Katika hali ya kawaida kabisa kila bima ina vitu inavyokinga na hii kiuhalisia ndio mipaka ya bima husika. Bima ya mkopo au mara nyingi huitwa credit life insurance ni bima inayokatwa dhidi ya majanga kama kifo au ulemavu wa kudumu kama vitamkumba yule anayekatiwa bima/insured.

Swala la mtu kuacha kazi au kutoroka bima huwa haihusiki maana sio sehemu ya makubaliano ya bima husika. Ziko bima mfano zinazokinga upotevu wa fedha dhidi ya wafanyakazi ulio waajiri, zipo bima zinazolinda bidhaa/stocks zilizoko dukani dhidi ya majanga kama moto na mengine ya asili/natural calamities n.k.

Scope/wigo wa bima husika ndio utatoa majibu ya risks/majanga gani ambayo bima hukinga na yapi haihusiki.

Sijui kama nimekujibu ipasavyo
Nimekuelewa kwa upande wa swali langu kipengele cha kwanza...
Lakn cha pili hujajbu,kuhusiana na taasisi ndogo za kifedha.
 
Nimekuelewa kwa upande wa swali langu kipengele cha kwanza...
Lakn cha pili hujajbu,kuhusiana na taasisi ndogo za kifedha.
Kiongozi, kwa kuzingatia umuhimu wa bima ya mkopo kulingana na kazi inazofanya naamini wanaitumia pia.

Unachopaswa kujua ni kwamba hamna mkopeshaji yuko tayari kuona fedha yake inapotea hata kama mkopaji atafariki au kupata ulemavu wa kudumu. Lengo la bima ya mkopo ni kuondoa usumbufu kwa mkopaji au ndugu wa marehemu lakini pia kuhakikisha kuwa fedha ya mkopeshaji inabaki salama.

Taasisi yoyote ya fedha iliyo smart ni lazima itumie huduma hii, maana inaweka heshima ya taasisi katika jamii/kutochukua mali au kulazimisha ndugu wa marehemu kulipa na pia taasisi kulinda fedha zake.

Saccos nyingi tu kwa mfano zinazokopa mikopo kwenye mabenki mara nyingi wanalazimika kwa wanachama wao kukatiwa bima ya mkopo pia, ili kupunguza mzigo endapo mwanachama wao atafariki.
 
Kiongozi, kwa kuzingatia umuhimu wa bima ya mkopo kulingana na kazi inazofanya naamini wanaitumia pia.

Unachopaswa kujua ni kwamba hamna mkopeshaji yuko tayari kuona fedha yake inapotea hata kama mkopaji atafariki au kupata ulemavu wa kudumu. Lengo la bima ya mkopo ni kuondoa usumbufu kwa mkopaji au ndugu wa marehemu lakini pia kuhakikisha kuwa fedha ya mkopeshaji inabaki salama.

Taasisi yoyote ya fedha iliyo smart ni lazima itumie huduma hii, maana inaweka heshima ya taasisi katika jamii/kutochukua mali au kulazimisha ndugu wa marehemu kulipa na pia taasisi kulinda fedha zake.

Saccos nyingi tu kwa mfano zinazokopa mikopo kwenye mabenki mara nyingi wanalazimika kwa wanachama wao kukatiwa bima ya mkopo pia, ili kupunguza mzigo endapo mwanachama wao atafariki.
Asante kwa ufafanuzi mzuri kiongozi.
 
Kwa wenzetu inarudishwa, bongo hairudi!
Ngoja tutafute aliyepewa dhamana ya kurekebisha hali hii. Ikionekana wanatuibia inabidi wote tuliofanyiwa dhuruma tukaidai fidia mahakamani. Wanaweza filisika eti!
 
Habari zenu wanajamvi
Miaka sita (6) iliyopita nilichukua mkopo bank ya CRDB kwa dhamana ya utumishi na marejesho yakiwa yanakatwa moja kwa moja kwenye mshahara, moja ya masharti ya ule mkopo ilikuwa ni lazma ukatiwe bima dhidi ya kifo au ulemavu wa kudumu, maafisa mikopo wa CRDB walinielimisha vizuri sana kuhusu hii bima amabayo wanaikata kwenye kile kiasi ulichoomba mkopo, nadhani ni kama 200k+ kama sikosei.wakanielieza kwamba

Kile kiasi cha pesa kilichokatwa kwenye mkopo nilioomba kama Bima kinasimamia upotevu wa fedha,mali iliyokatiwa Bima kutokana na kutokuwepo kwa uaminifu kutoka kwa waajiri wakati wafanyakazi wakiwa kazini. Bima hii pia inasimamia usalama wamali iliyochukuliwa kama dhamana. Wakaendelea kusema,

Bima hiyo inalipia hasara ya fedha anayoipata mkopeshaji ( ambao ni wao CRDB Bank) kutokana na matatizo aliyopata mdeni kufuatia majanga ya kifo au ulemavu wa kudumu kabla hajamaliza kulipa deni. Husaidia kupunguza hasara ikilinganishwa na dhamana iliyowekwa. Kwa wakopaji wasio na dhamana za kazi Bima hii ina hakikisha familia ya mhanga haiachwi bila makazi au mzigo wa kuendelea kulipia deni linalodaiwa pale mkopaji anapofariki au kupata ulemavu wa kudumu.

HOJA YANGU
Deni langu lilikuwa la miaka mitano (5) na mwaka jana nilimalizana na hili deni, yaani hawanidai tena tangu mwaka jana, nilitegemea baada ya deni kumalizika hawa CRDB bank wanirudishie ile pesa yangu Zaidi ya 200K kwa vile mkopo wao tayari nimeurudisha wote pamoja na riba na bila usumbufu, mwanzoni mwa mwaka huu niliwatumia barua kuwakumbusha kuhusu kunirejeshea hii pesa hawajanijibu hadi leo, jana nimewatumia email kupitia kwa DG wao bado pia naona kimya.

Hii kitu imeekaaje kwa hapa bongo, au ndo bank inadhulumu wateja wao…, nakumbuka nilikopaga pesa stanbic bank nikiwa Kenya kwa mda wa mwaka mmoja na baada ya mkopo kuisha nikarejesehewa hii pesa tena wakani email kabisa kunitaarifu.

Najua wakopaji kwenye hizi taasisi za kifedha wako wengi na najua na wao hawajui kama wanatakiwa kurudishiwa hii pesa baada ya mikopo kumalizika , naombeni kujulishwa kama hapa bongo hii pesa huwa hairudi hata kama deni lao umemaliza lote?
Hio Bima wanalipa kampuni za bima ambazo incase of death or permanent disability bima wanailipa bank. Sasa nazani kwa hapa tz no refund
 
Hela ya bima huwa hairudishwi. Ni kama kukatia gari bima, unaweza ukalipia bima hata miaka 10 bila kupata ajali.
 
Back
Top Bottom