Kwanini Madalali kwenye Masoko wana nguvu kiasi hiki? Wakulima tunaumizwa

Nyendo

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2017
Posts
1,455
Reaction score
5,134
Kwanza kabisa nipeni kiti nikae nifute machozi mkulima mimi! Hivi hawa madalali kwa nini wana nguvu kiasi hiki? Kwa nini wanaruhusiwa kuwepo licha ya unyonyaji wanaotufanyia wakulima? Ni huzuni sana, kilimo kimezungukwa na utapeli ambao unakaliwa kimya, wakulima tunaumia

Mkulima nahangaika shambani kuandaa shamba, kulima, kupanda, kupalilia, madawa na mavuno achilia mbali gharama za wasaidizi shambani na kadhalika halafu navuna zao langu napeleka sokoni nakosa uhuru na zao langu kisa uwepo wa kiumbe kinachoitwa dalali wa sokoni!!!

Dalali anakuja anapanga bei yeye kwenye bidhaa yangu inauzajwe kwa wakati huo, jamani utadhani alinisaidia kulima ila ndio ana nguvu na soko maana ukikataa kumpa mzigo anunue kwa bei anayotaka yeye atakusagia kunguni usiweze kuuza na bidhaa zitakuozea mbele ya macho yako na hakuna kitu utafanya.

Wakulima tunaonewa sana na madalali na kuibiwa pia, wanatumia uwepo wao kwenye masoko kuwalaghai walanguzi wa bidhaa kwa jumla ambao ndio wanauza kwenye masoko kuwa wao ndio wana bidhaa hivyo wakihitaji wawaone pia wanakuwa na mawasiliono na wauzaji mzigo ukifika wanawapigia kuwa wana mzigo wewe mkulima utabaki hapo na Lori lako mpaka ujute kufika mjini.

Nafikiri ni wakati sasa mfumo wa masoko ubadilike uwe huria ili mkulima awe na nguvu ya kuweza kupata masoko mwenyewe bila dalali ili mtu anayehitaji dalali amtumie na asiyehitaji dalali aweze kuuza mwenyewe bila kuwekekwa kauzibe.

Ni mimi mkulima naongea nikiwa na uchungu sana kwani madalali wanatajirika kwa mgongo wa mkulima ambaye anaendelea kuumia mgongo na kuzeeka masikini huku wajanja wakila kwa uraisi tu.

Pia soma: Je! Nini hatma ya mkulima na mazao yake Tanzania?
 
Kuna mtu anaitwa Vale Nafaka ana mashamba Arusha na Manyara lakini ndiyo Dalali aliyechangamka Mjini anadalalia wakulima kwa bei ndogo huku akiwapiga hela wale wakubwa
 
Ni huzuni mno kwa sisi wakulima
 
Kuna dalali kidogo tu anitapeli kama si Mwanasheria wangu na wasaidizi wake kuniita pembeni na kunizindua ningepigwa vibaya.

Huyu dalali anatumia njia za ushirikina kwa kukuuzia viwanja mwenye kiwanja mwenyewe alishangaa alisema leo huyu ana nini?. Mbona sio kawaida yake
 
Hatari sana, madalali ni jipu
 
Kuna dalali kidogo tu anitapeli kama si Mwanasheria wangu na wasaidizi wake kuniita pembeni na kunizindua ningepigwa vibaya.

Huyu dalali anatumia njia za ushirikina kwa kukuuzia viwanja mwenye kiwanja mwenyewe alishangaa alisema leo huyu ana nini?. Mbona sio kawaida yake
😅😅
 
Kwanza kabisa nipeni kiti nikae nifute machozi mkulima mimi! Hivi hawa madalali kwa nini wana nguvu kiasi hiki? Kwa nini wanaruhusiwa kuwepo licha ya unyonyaji wanaotufanyia wakulima? Ni huzuni sana, kilimo kimezungukwa na utapeli ambao unakaliwa kimya, wakulima tunaumia

Mkulima nahangaika shambani kuandaa shamba, kulima, kupanda, kupalilia, madawa na mavuno achilia mbali gharama za wasaidizi shambani na kadhalika halafu navuna zao langu napeleka sokoni nakosa uhuru na zao langu kisa uwepo wa kiumbe kinachoitwa dalali wa sokoni!!!

Dalali anakuja anapanga bei yeye kwenye bidhaa yangu inauzajwe kwa wakati huo, jamani utadhani alinisaidia kulima ila ndio ana nguvu na soko maana ukikataa kumpa mzigo anunue kwa bei anayotaka yeye atakusagia kunguni usiweze kuuza na bidhaa zitakuozea mbele ya macho yako na hakuna kitu utafanya.

Wakulima tunaonewa sana na madalali na kuibiwa pia, wanatumia uwepo wao kwenye masoko kuwalaghai walanguzi wa bidhaa kwa jumla ambao ndio wanauza kwenye masoko kuwa wao ndio wana bidhaa hivyo wakihitaji wawaone pia wanakuwa na mawasiliono na wauzaji mzigo ukifika wanawapigia kuwa wana mzigo wewe mkulima utabaki hapo na Lori lako mpaka ujute kufika mjini.

Nafikiri ni wakati sasa mfumo wa masoko ubadilike uwe huria ili mkulima awe na nguvu ya kuweza kupata masoko mwenyewe bila dalali ili mtu anayehitaji dalali amtumie na asiyehitaji dalali aweze kuuza mwenyewe bila kuwekekwa kauzibe.

Ni mimi mkulima naongea nikiwa na uchungu sana kwani madalali wanatajirika kwa mgongo wa mkulima ambaye anaendelea kuumia mgongo na kuzeeka masikini huku wajanja wakila kwa uraisi tu.

Pia soma: Je! Nini hatma ya mkulima na mazao yake Tanzania?
Na mimi nashangaa sana, kwani wanunuaji hawaana uwezo wa kwenda wao wenyewe sokoni? Kwanini watumie middle men wakati pesa ni zao?

Madalali uchwara ndio husababisha bei za vitu kupanda sio kwa muuzaji tu hata kwa mlaji pia
 
Wale wapo na wanatambulika kabisa Kama hutaki madalali wakuuzie Tafuta sehemu mtaan kwako Unauzia hapo au usake masoko nje ya Soko mfano utafute wafanyabiashara wanauza bidhaa kwa Jumla kama mchele au maharagwe uwauzie. Ila ukishafika sokoni madalali wapo na wana nguvu ila hawapangi Bei wanakupa bei iliyo sokoni kwa wakati HJusika. Kuwa na nguvu kila mtu ana nguvu akiwa eneo lake l kujidai
 
Ulipochanganya ushirikina ndio nimeachana na hii comment
 
Wale wapo na wanatambulika kabisa Kama hutaki madalali wakuuzie Tafuta sehemu mtaan kwako Unauzia hapo au usake masoko nje ya Soko mfano utafute wafanyabiashara wanauza bidhaa kwa Jumla kama mchele au maharagwe uwauzie. Ila ukishafika sokoni madalali wapo na wana nguvu ila hawapangi Bei wanakupa bei iliyo sokoni kwa wakati HJusika. Kuwa na nguvu kila mtu ana nguvu akiwa eneo lake l kujidai
Nimesoma comment kabka sijaangalia ID nilivyomaliza tu nikajua huyu ni Dalalali, kutazama juu nakutana na Dalali Mkuu
 
Kwanza kabisa nipeni kiti nikae nifute machozi mkulima mimi! Hivi hawa madalali kwa nini wana nguvu kiasi hiki? Kwa nini wanaruhusiwa kuwepo licha ya unyonyaji wanaotufanyia wakulima? Ni huzuni sana, kilimo kimezungukwa na utapeli ambao unakaliwa kimya, wakulima tunaumia

Mkulima nahangaika shambani kuandaa shamba, kulima, kupanda, kupalilia, madawa na mavuno achilia mbali gharama za wasaidizi shambani na kadhalika halafu navuna zao langu napeleka sokoni nakosa uhuru na zao langu kisa uwepo wa kiumbe kinachoitwa dalali wa sokoni!!!

Dalali anakuja anapanga bei yeye kwenye bidhaa yangu inauzajwe kwa wakati huo, jamani utadhani alinisaidia kulima ila ndio ana nguvu na soko maana ukikataa kumpa mzigo anunue kwa bei anayotaka yeye atakusagia kunguni usiweze kuuza na bidhaa zitakuozea mbele ya macho yako na hakuna kitu utafanya.

Wakulima tunaonewa sana na madalali na kuibiwa pia, wanatumia uwepo wao kwenye masoko kuwalaghai walanguzi wa bidhaa kwa jumla ambao ndio wanauza kwenye masoko kuwa wao ndio wana bidhaa hivyo wakihitaji wawaone pia wanakuwa na mawasiliono na wauzaji mzigo ukifika wanawapigia kuwa wana mzigo wewe mkulima utabaki hapo na Lori lako mpaka ujute kufika mjini.

Nafikiri ni wakati sasa mfumo wa masoko ubadilike uwe huria ili mkulima awe na nguvu ya kuweza kupata masoko mwenyewe bila dalali ili mtu anayehitaji dalali amtumie na asiyehitaji dalali aweze kuuza mwenyewe bila kuwekekwa kauzibe.

Ni mimi mkulima naongea nikiwa na uchungu sana kwani madalali wanatajirika kwa mgongo wa mkulima ambaye anaendelea kuumia mgongo na kuzeeka masikini huku wajanja wakila kwa uraisi tu.

Pia soma: Je! Nini hatma ya mkulima na mazao yake Tanzania?
Soko huria ndio Lina madalali, soko ambalo lipo controlled ndio halina.

Mazao ambayo Yana Amcoss bei hupangwa mapema.
 
Na mimi nashangaa sana, kwani wanunuaji hawaana uwezo wa kwenda wao wenyewe sokoni? Kwanini watumie middle men wakati pesa ni zao?

Madalali uchwara ndio husababisha bei za vitu kupanda sio kwa muuzaji tu hata kwa mlaji pia
kwenye maisha huwezi ukafanya kila kitu mwenyewe..lazima uwe na mfuno wa kukurahisishia kazi...Tajiri kazi yake ni kuuza anahitajika awepo sokoni muda mwingi au unakuta ana biashara nyingi ndio maana anatumia madalali kumkusanyia mizigo na kisha kuipakia na kuituma..wao madalali huwa wana commission yao kwa tajiri. Ila wanapofika kwa wakulima napo humpinda mkulima ili wanunue kwa bei ya chini wapate na chochote kitu kutoka kwa mkulima. So dalali anakula pande mbili..kwa tajiri na kwa mkulima...Ndivyo system ilivyo
 
Madalali ni watu wa hovyo sana
 
Back
Top Bottom