Wapinzani walikuwa na haki ya kumchukia Magufuli kutokana na mambo aliyowatenda.
Lakini cha kushangaza upinzani mkubwa sana umeibuka kutoka katika kikundi kidogo ndani ya chama chake mimi nawaita wanufaika wa chama.
Kukaibuka wakina KIGOGO 2014 hadi alipofariki uwanaharakati wao ukaisha.
Mwanaharakati Kigogo amekaa kimya kwenye kesi ya Mbowe, hapa shida ya Kigogo sio mfumo bali ni Magufuli mwenyewe.
Chuki nyingine ikahamia kwa Bashiru.
Nikajiuliza wako wapinzani wengi waliohamia CCM na kupewa vyeo vikubwa lakini kwanini wamchukie Dr. Bashiru tu?
Na kumzushia ameiba hela BOT kipindi cha maombolezo. Nikagundua tatizo Bashiru alikata mirija yao kwenye tume ya kukagua mali za Chama.
Mimi nimepanga fremu za CCM nalipa kodi laki 1.5 lakini nasikia kodi ya halali inayoingia kwenye chama ni elfu 50 nyingine watu hula kwa urefu wa kamba. Wenyeviti wa CCM wilaya waligeuza miradi ya chama kuwa miradi yao binafsi na walikuwa wanalindana.
Hii ilipelekea miradi mingi ya chama kufilisika mfano Tegeta Sekondari sasa imeuzwa kwa chuo kikuu Mzumbe.
Bashiru alifichua yote hayo kwenye kamati yake na kamba za watu zikakatwa, wenye kamba hawakufurahishwa kabisa ila hawakuwa na lakufanya. Kwahiyo tatizo la Magufuli na Bashiru ndani ya CCM ni:
1. Kuwanyima vyeo wenye chama chao.
2. Kuwapa vyeo wakuja ndani ya chama.
3. Kukata mirija ya watu ndani ya chama.
Hayo mengine ya raisi mshamba, anateuwa wasukuma, dikteta na ya Bashiru kutoa hela BOT au alitaka kumchenga mama ili aweke rais mwingine ni uzushi tu uliosambazwa na watu wale wale kupitia akaunti ileile.
Watu wamerudi ulaji wao utarudi soon na akauti ile ya uwanaharakati KIGOGO imepotea na itaibuka tena tukipata rais mwingine mshamba mwenye msimamo.
Bado tuna safari ndefu Watanzania.
"Mungu ibariki Tanganyika"