Kwanini Magufuli alichukiwa ndani ya CCM?

Kwanini Magufuli alichukiwa ndani ya CCM?

1995 Lyatonga alishinda na huu ndio ukweli!
2010 Slaa alitoka hadharani wakati matokeo yanatangazwa akiwa na ushahidi kuwa matokeo ya urais yanayotangazwa na NEC ni tofauti na recodi walizo nazo kutoka majimboni.
 
Wapinzani walikuwa na haki ya kumchukia Magufuli kutokana na mambo aliyowatenda.

Lakini cha kushangaza upinzani mkubwa sana umeibuka kutoka katika kikundi kidogo ndani ya chama chake mimi nawaita wanufaika wa chama.

Kukaibuka wakina KIGOGO 2014 hadi alipofariki uwanaharakati wao ukaisha.

Mwanaharakati Kigogo amekaa kimya kwenye kesi ya Mbowe, hapa shida ya Kigogo sio mfumo bali ni Magufuli mwenyewe.

Chuki nyingine ikahamia kwa Bashiru.
Nikajiuliza wako wapinzani wengi waliohamia CCM na kupewa vyeo vikubwa lakini kwanini wamchukie Dr. Bashiru tu?

Na kumzushia ameiba hela BOT kipindi cha maombolezo. Nikagundua tatizo Bashiru alikata mirija yao kwenye tume ya kukagua mali za Chama.

Mimi nimepanga fremu za CCM nalipa kodi laki 1.5 lakini nasikia kodi ya halali inayoingia kwenye chama ni elfu 50 nyingine watu hula kwa urefu wa kamba. Wenyeviti wa CCM wilaya waligeuza miradi ya chama kuwa miradi yao binafsi na walikuwa wanalindana.

Hii ilipelekea miradi mingi ya chama kufilisika mfano Tegeta Sekondari sasa imeuzwa kwa chuo kikuu Mzumbe.

Bashiru alifichua yote hayo kwenye kamati yake na kamba za watu zikakatwa, wenye kamba hawakufurahishwa kabisa ila hawakuwa na lakufanya. Kwahiyo tatizo la Magufuli na Bashiru ndani ya CCM ni:

1. Kuwanyima vyeo wenye chama chao.

2. Kuwapa vyeo wakuja ndani ya chama.

3. Kukata mirija ya watu ndani ya chama.

Hayo mengine ya raisi mshamba, anateuwa wasukuma, dikteta na ya Bashiru kutoa hela BOT au alitaka kumchenga mama ili aweke rais mwingine ni uzushi tu uliosambazwa na watu wale wale kupitia akaunti ileile.

Watu wamerudi ulaji wao utarudi soon na akauti ile ya uwanaharakati KIGOGO imepotea na itaibuka tena tukipata rais mwingine mshamba mwenye msimamo.

Bado tuna safari ndefu Watanzania.

"Mungu ibariki Tanganyika"
Hivi mpk leo huamini kuwa ni marehemu?
 
Ccm lilikuwa limegeuka kuwa pango la wanyang'anyi.

Kila aina ya ufisadi ccm ndiyo ilikuwa makao makuu, genge lenyewe likiongozwa na mwenyekiti fisadi Kikwete.

Magufuli alipokuja akakata mirija mingi ya mafisadi ndani ya chama na akafhibiti kukitumia chama kujinufaisha.

Kikwete na genge la wezi wenzie ndo wakamchukia.
Bora wezi ambao wanasababisha mzunguko wa pesa kuliko wezi wachache wanaoziba kabisa mzunguko
 
Kwa nijuavyo hata wakati wa JK, upinzani hawakukubalina na mambo mengi tu.

Tofauti ya wakati uliopita na wakati wa JPM, wakati wa JPM mitandao ya kijamii ilikuwa na nguvu zaidi na wafuasi wengi.

Waliofuatilia siasa za wakati wa awamu ya nne, rais JK, alisemwa sana kwa ubaya. Na alitukanwa hadi hadharani; mkwere wa watu alichukulia sawa tu.

Na wakati mwingine aliwajibu kwa mafumbo.
Ila msukuma hakuweza kukubaliana na ukosoaji wa hadharani au popote pale. Hii ndio tofauti hata kwa awamu hii ya sasa.

Kwenye siasa, viongozi wengi hawako tayari kukosolewa hata kama wanakosea!

Tena binafsi naona bora hata JPM, alijidhihirisha wazi kuliko hao wengine wanafanya kwa siri.

Ama sivyo, 'mama' asingehangaika na suala la job ikiwa hakukuwa na ukweli wowote! Na inawezakana hata sasa anachukiwa sana tu, ila muda haujafika.

Ni maoni tu!
Unasema JPM msukuma?
Alikwambia nani?
 
Unasema JPM msukuma?
Alikwamnia nani?
Kwani hakuwa msukuma?

Japo mambo ya ukabila binafsi huwa siyazingatii sana.
Ila nadhani alikuwa wa kabila hilo kutokana na historia yake, lafudhi yake na hata kuzungumza!
 
Kweli kabisa
HUwezi kujua hata kama huyu wa sasa wanampenda maana hata hawa hawa wanaomponda wakati yuko hai walikuwa wanamsifu na kuabudu.

Hawa hawa wakina Mwigulu ndio walikuwa wanasema apewe muda.

Kujua yupo rafiki wa kweli ukiwa na madaraka au pesa ni ngumu sawa na kupata mke anayekupenda kwa dhati ukiwa tajiri.
 
Kwani hakuwa msukuma?

Japo mambo ya ukabila binafsi huwa siyazingatii sana.
Ila nadhani alikuwa wa kabila hilo kutokana na historia yake, lafudhi yake na hata kuzungumza!
Wakimbizi waliokulia usukumani wana lafudhi hiyo hiyo.
 
Back
Top Bottom