Kwanini mahusiano mengi ya kimapenzi sasa hivi yanadumu wiki mbili tu, au siku nne tu?

Kwanini mahusiano mengi ya kimapenzi sasa hivi yanadumu wiki mbili tu, au siku nne tu?

AlphaMale

JF-Expert Member
Joined
Oct 26, 2019
Posts
613
Reaction score
1,425
Nimeona kwa washkaji zangu wengi walionizunguka, utakuta amepata namba ya mdada leo, lakini baada ya siku chache au baada ya wiki mbili washaachana. Wengine wakiachana hata wakikutana barabarani, salamu hawapeani. Tatizo ni nini?
 
Ukikua utajua kwa nn hatudumu nao mda mrefu, ila pamoja na kupunguza gharama maana utalipa kodi, utanunua dstv na kulipia kifurushi lak kila mwezi n.k
 
Ni kwasababu wengi wao hawajui maana nzima ya mapenzi!
Mapenzi yanamaana kubwa sana tofauti na yanavyochukuliwa.. mapenzi yamechanganywa na tamaa,uhuni,ubinafsi na uthamini wake umepungua!.. Nani atadumu kama tamaa ikitamalaki..?
Uhuni he..?
Vipi kuhusu ubinafsi..?

Ulichokiandika hapo mi sikiiti mapenzi bali makutano ya kitamanio ya watu mbalimbali..!

Mapenzi ni kuishi nusu maisha yako na nusu maisha ya mwenzio, mapenzi ni maelewano yenye msingi wa pamoja, mapenzi ni upendo wenye kiutendaji.. hivyo basi misingi ya mapenzi na tafsiri zake zisipokuwa bayana kwa hayo makutano ya watu mbalimbali sahau kuishi milele kwa watu hao.
 
Hao wanaokutana then after two week wanaachana inamaana walikubaliana ndani ya week mbili, wakalana ndani ya week hzo hzo mbili ,wakasalitiana (pengine) ndani ya week hzo hzo mbili , + mizinga, Sasa kwenye kipindi kifupi km hicho matukio yote yameshafanyika ...unafikiri Nani atakua na hamu ya kuiendeleza safari iliyofikia ukomo
Na hao sio wapenzi ...Ni wahuni wawili waliobobea wamekutana

One love
 
Siku hizi watu wamekuwa wabinafsi sana sana. Mapenzi yanahitaji watu wawili wawe kwenye barabara moja. Sasa kila mtu anapigia msuli tu mambo yake mapenzi yatadumu? Unakuta kila mtu anakuwa mzigo kwa mwenzake. Enzi za zamani mapenzi ilikuwa uchumba serious kisha ndoa serious. Siku hizi ni kugusana gusana tu siku ziende huku kila mtu anapambania matakwa au mahitaji binafsi
 
Mwanamke unayempata ndani ya muda gani ndio utadumu nae?
Muda unaotosha kusoma tabia zake naye asome zako huku ukiwa unalialia bila kukubaliwa. Msichana ambaye mpaka unampata hata wazazi wake na wako wanajua unamhangaikia. Hao wa vodafasta huisha hata kabla hujamaliza maongezi. Utasikia "hauna salio la kutosha, kuendelea na maongezi tafadhali ongeza salio."
 
-Tatizo ni nafsi mbili zisizokua na nia moja!
-Hamuendani mmetakana tu kwasababu fulani pengine kila mmoja hajapata/amepata anachokitaka kwa muda aliojipangia sasa mnaendelea muende wapi? Guantanamo au[emoji174]
pia kuna vile vijambo vidogo dogo vinavunja mahusiano ambavyo vinaingia kwenye category ya kutoendana (Unapata mtu mnachat anakuandikia mwandiko wa ajabu Xaxa/Oi/nipange/Mamb/[emoji2],Story zake za ajabu ajabu wakati ww uko serious unajikuta waswahili wanasema sio pigo zako) kwakua hamna mtu aliekula cha mtu basi kila mtu anashika hamsini zake
 
Kuna kademu nilikutana nako instagram. Nikaweka mambo sawa tukaanza. Huku na kule baada ya mitoko, na mieleka kadhaa kuna siku kakanitumia ujumbe kuwa kanashida ya kodi na mimi muda huo siko vema yaani gari yenyewe naendesha kwa route za hela tu route za kipuuzi napaki gari nakanyaga na kupanda daladala.

Sasa nikakaambia kasubirie nitakacheki kakawa kanalazimisha kuwa nikaombee hata kwa rafikk yangu. Mmmmmmhmn me nakakauliza kwani kwann imekuwa ghafla hivyo, kakanambia mwenye nyumba amecharuka.

Nikakaambia kama ni hivyo nipe namba ya mwenye nyumba nitamalizana nae asikusumbue wewe kademu kakakomaa nakwambia hakataki kuelewa kwamba nikatumie hata kidogo (90,000).

Basi nikamwambia kwasasa sina ngoja. Kananambia yaani umeshindwa kunipa 90,000 na unaendesha gari kila siku. Nikaona hii takataka sijui hata kwann najibizana nayo. Nikakaa kimya. Weee alinitumia gazeti hilo. Nikaona hapa hamna kitu hapa. Huyu ni mdangaji tu kama wengine nikamzimia umeme.
 
Back
Top Bottom