Kwanini mahusiano mengi ya kimapenzi sasa hivi yanadumu wiki mbili tu, au siku nne tu?

Ni kwasababu wengi wao hawajui maana nzima ya mapenzi!
Mapenzi yanamaana kubwa sana tofauti na yanavyochukuliwa.. mapenzi yamechanganywa na tamaa,uhuni,ubinafsi na uthamini wake umepungua!.. Nani atadumu kama tamaa ikitamalaki..?
Uhuni he..?
Vipi kuhusu ubinafsi..?

Ulichokiandika hapo mi sikiiti mapenzi bali makutano ya kitamanio ya watu mbalimbali..!

Mapenzi ni kuishi nusu maisha yako na nusu maisha ya mwenzio, mapenzi ni maelewano yenye msingi wa pamoja, mapenzi ni upendo wenye kiutendaji.. hivyo basi misingi ya mapenzi na tafsiri zake zisipokuwa bayana kwa hayo makutano ya watu mbalimbali sahau kuishi milele kwa watu hao.
Ndo maana nakupendaga
 
Nimeona kwa washkaji zangu wengi walionizunguka, utakuta amepata namba ya mdada leo, lakini baada ya siku chache au baada ya wiki mbili washaachana, wengine wakiachana hata wakikutana barabarani, salamu hawapeani, tatizo ni nini?
Alpha kuna Jambo la ajabu Sana limeikumba dunia. Vijana wengi Wana owa kurusha watu na wanaolewa kurusha watu nadhan jibu umelipata.
 
Kuna kademu nilikutana nako instagram. Nikaweka mambo sawa tukaanza. Huku na kule baada ya mitoko, na mieleka kadhaa kuna siku kakanitumia ujumbe kuwa kanashida ya kodi na mimi muda huo siko vema yaani gari yenyewe naendesha kwa route za hela tu route za kipuuzi napaki gari nakanyaga na kupanda daladala.

Sasa nikakaambia kasubirie nitakacheki kakawa kanalazimisha kuwa nikaombee hata kwa rafikk yangu. Mmmmmmhmn me nakakauliza kwani kwann imekuwa ghafla hivyo, kakanambia mwenye nyumba amecharuka.

Nikakaambia kama ni hivyo nipe namba ya mwenye nyumba nitamalizana nae asikusumbue wewe kademu kakakomaa nakwambia hakataki kuelewa kwamba nikatumie hata kidogo (90,000).

Basi nikamwambia kwasasa sina ngoja. Kananambia yaani umeshindwa kunipa 90,000 na unaendesha gari kila siku. Nikaona hii takataka sijui hata kwann najibizana nayo. Nikakaa kimya. Weee alinitumia gazeti hilo. Nikaona hapa hamna kitu hapa. Huyu ni mdangaji tu kama wengine nikamzimia umeme.
Hahaa
 
Ni kwasababu wengi watakuwa nje ya matarajio, yaani walichotegemea baada ya kuanza uhusiano kinakuwa ni tofauti na kupelekea Kila mtu kupita njia yake,
 
-Tatizo ni nafsi mbili zisizokua na nia moja!
-Hamuendani mmetakana tu kwasababu fulani pengine kila mmoja hajapata/amepata anachokitaka kwa muda aliojipangia sasa mnaendelea muende wapi? Guantanamo au[emoji174]
pia kuna vile vijambo vidogo dogo vinavunja mahusiano ambavyo vinaingia kwenye category ya kutoendana (Unapata mtu mnachat anakuandikia mwandiko wa ajabu Xaxa/Oi/nipange/Mamb/[emoji2],Story zake za ajabu ajabu wakati ww uko serious unajikuta waswahili wanasema sio pigo zako) kwakua hamna mtu aliekula cha mtu basi kila mtu anashika hamsini zake
Na wale ambao muda wote wanataka mchat, wanaingia kwenye kundi lipi ?
 
Kuna kademu nilikutana nako instagram. Nikaweka mambo sawa tukaanza. Huku na kule baada ya mitoko, na mieleka kadhaa kuna siku kakanitumia ujumbe kuwa kanashida ya kodi na mimi muda huo siko vema yaani gari yenyewe naendesha kwa route za hela tu route za kipuuzi napaki gari nakanyaga na kupanda daladala.

Sasa nikakaambia kasubirie nitakacheki kakawa kanalazimisha kuwa nikaombee hata kwa rafikk yangu. Mmmmmmhmn me nakakauliza kwani kwann imekuwa ghafla hivyo, kakanambia mwenye nyumba amecharuka.

Nikakaambia kama ni hivyo nipe namba ya mwenye nyumba nitamalizana nae asikusumbue wewe kademu kakakomaa nakwambia hakataki kuelewa kwamba nikatumie hata kidogo (90,000).

Basi nikamwambia kwasasa sina ngoja. Kananambia yaani umeshindwa kunipa 90,000 na unaendesha gari kila siku. Nikaona hii takataka sijui hata kwann najibizana nayo. Nikakaa kimya. Weee alinitumia gazeti hilo. Nikaona hapa hamna kitu hapa. Huyu ni mdangaji tu kama wengine nikamzimia umeme.
Bwana Sam umepotea sana whatsapp
 
kwa sababu naomba ela ni nyingi sana ukikaa kidogo utasikia baby nikwambie kitu ujue mzinga uo sasa unategemea mapenzi yatadumu kwa staili iyo
 
Kutoendana
Na wale ambao muda wote wanataka mchat, wanaingia kwenye kundi lipi ?
Maana yeye anataka mchati muda wote ,wewe hutaki
-ila hii inarekebishika unamwambia nakua busy kama bado haelewi mtafutie kazi impe ubusy kama wako mfanane
 
Watu kila rangi tumeziona kila uongo tunaujua kila trick tushafanya/fanyiwa kwa hiyo haichukui muda. Mtu mbabaishaji mm namjua baada ya first date tu. Wiki nyingi.

Hahaa unajuaje kuwa mwanaume ni mbabaishaji kwenye date ya kwanza tu? Umdhaniaye ndie mbabaishaji kumbe sie Tuttyfruity
 
Kuna kademu nilikutana nako instagram. Nikaweka mambo sawa tukaanza. Huku na kule baada ya mitoko, na mieleka kadhaa kuna siku kakanitumia ujumbe kuwa kanashida ya kodi na mimi muda huo siko vema yaani gari yenyewe naendesha kwa route za hela tu route za kipuuzi napaki gari nakanyaga na kupanda daladala.

Sasa nikakaambia kasubirie nitakacheki kakawa kanalazimisha kuwa nikaombee hata kwa rafikk yangu. Mmmmmmhmn me nakakauliza kwani kwann imekuwa ghafla hivyo, kakanambia mwenye nyumba amecharuka.

Nikakaambia kama ni hivyo nipe namba ya mwenye nyumba nitamalizana nae asikusumbue wewe kademu kakakomaa nakwambia hakataki kuelewa kwamba nikatumie hata kidogo (90,000).

Basi nikamwambia kwasasa sina ngoja. Kananambia yaani umeshindwa kunipa 90,000 na unaendesha gari kila siku. Nikaona hii takataka sijui hata kwann najibizana nayo. Nikakaa kimya. Weee alinitumia gazeti hilo. Nikaona hapa hamna kitu hapa. Huyu ni mdangaji tu kama wengine nikamzimia umeme.
Ukampa nyekundu
JamiiForums-1758283439.jpg

One love
 
Ubinafsi
Tamaa
Kukosa uvumilivu
 
Back
Top Bottom