Kenya ukilinganisha
Kenya hawana demokrasia komavu kama Marekani.
Ni kweli mfumo wao wa sasa Jaji mkuu anaomba kazi na kupitia katika mikono ya usaili toka kwa manguli wa sheria. Pamoja na hayo, bado mfumo huo una mapungufu mengi hasa ukikuta Jaji Mkuu ana msimamo mkali ambao hauzingatii matakwa ya maslahi mapana ya Taifa.
Fikiria kitendo cha mahakama kufuta uchaguzi mkuu wa Kenya mwaka jana. Hakuna anaepinga gharama za demokrasia na utawala wa sheria. Mwisho wa siku uchaguzi umerudiwa na fedha nyingi zimetumika, na alieshinda ni yule yule Uhuru Kenyatta.
Fedha zile zingeweza kufanya miradi ya kugusa wananchi moja kwa moja kama vile maji, huduma ya afya, mikopo inayoibua ajira endelevu kwa vijana na mambo kama hayo