Kwanini majiji yetu Tanzania hatuwezi kuyafanya yawe masafi kama Kigali?

Traxtion

JF-Expert Member
Joined
Dec 10, 2021
Posts
8,000
Reaction score
16,414
Hivi kwa nini licha ya kuwa jirani na Rwanda bado hatujapata motivation ya kufanya majiji yetu yawe masafi?

Tuna majiji sita tu
1. Dar es Salaam
2. Mwanza
3. Arusha
4. Dodoma
5. Tanga
6. Mbeya

Hivi hatuwezi kuanzisha kampeni kali ya "KEEP OUR CITIES CLEAN" watu walipishwe faini za kutosha wakitupa taka hovyo, kuwe na dustbin mitaani, kuwe na sheria kali kama tu walivyozuia mifuko ya plastiki na ikatoweka. Majiji 6 hayawezi kutushinda kuwa masafi

Shida wala sio umasikini. Rwanda kuna umasikini kushinda Tanzania na bado miji yao kuanzia Kigali, Musanze nk ni misafi na iko civilized.

Shida sio uchumi. Tanzania inazidi Rwanda kuanzia GDP mpaka GDP per capita na bado Rwanda inaonekana civilized

Shida sio watu weusi. Rwanda 99% ya population ni watu weusi, na nchi yao ni safi.

Shida sio population. Because tell me inakuwaje Mbeya, jiji la watu laki 6 ni chafu kuliko Kigali yenye watu milioni 2?

📸 Kigali
photo-1565349479047-d6211d4efc90.jpeg
photo-1585773111351-977313a05e66.jpeg
overview_image_27786643_673824.png
From towers to bustling streets and peaceful walkways_ Kigali moves with a rhythm that_s both...jpeg

FB_IMG_1765556308673.jpg
From towers to bustling streets and peaceful walkways_ Kigali moves with a rhythm that_s both...jpeg
FB_IMG_1765556297976.jpg
FB_IMG_1765556294402.jpg
FB_IMG_1765556223398.jpg
photo-1708772565599-2c4e4b3ed9db (1).jpeg
photo-1668875438994-4388304392ef.jpeg
 
Haya mambo ni psychology, lazima watu wahasishwe kuwa wastaarabu basi hiyo itakuwa kazi nyepesi sana hakuna mtu atatupa taka hovyo watu watazingatia vitu vingi sana ustaarabu ukiimarika ndani yao
 
Inabidi ziwepo sheria kali kwanza na kampeni nyingi za kufanya usafi na upandaji miti.
Sheria zikiwa kali watu watapunguza kutupa taka ovyo na miaka inavyozidi kwenda inakuwa utamaduni wao tayari
 
Sasa mtu toka azaliwe hajawahi kutoka nje ya Tanzania aone watu wastaarabu wanavyoishi; na hata wale walioishi huko hawaleti matokeo yoyote wakirudi unategemea nini? Usafi, mipangilio ya majiji ni elimu, sera, na uongozi ndio vinaweza kuleta hayo tunayoona huko nje.
 
Sehemu zikiwa planned ni rahisi kuwa safi angalia Masaki.
Eneo kama Kigogo,Manzese,Vingunguti nk zinaanzaje kuwa safi ? Sababu nyumba zenyewe zilivyo ni uchafu.

Ogopa jamii ambayo Kila eneo wanataka kuweka cargo, garage,Genge,vibanda vya pesa nk

Nchi ambayo open spaces zinauzwa na mamlaka.
 
Tatizo Tz kila kitu huwa ni kuingiza siasa,mfano sasa hivi serikali ikianzisha sheria kali sana kuhusu usafi kama Rwanda wana siasa wataitumia kama ajenda na mtaji wa kisiasa na watazunguka nchi nzima kuwaelezea wtz jinsi wanavyo nyanyasika kwenye nchi yao kwa kutozwa faini kiholela.

Mpaka sasa serikali imeshindwa kuwadhibiti wamachinga kwa sababu hizo hizo za kisiasa ,kiufupi nchi yeyote siasa ikipewa kipaumbele kuliko matumizi ya akili ni tatizo kubwa sana.
 
Hivi kwa nini licha ya kuwa jirani na Rwanda bado hatujapata motivation ya kufanya majiji yetu yawe masafi?

Tuna majiji sita tu
1. Dar es Salaam
2. Mwanza
3. Arusha
4. Dodoma
5. Tanga
6. Mbeya

Hivi hatuwezi kuanzisha kampeni kali ya "KEEP OUR CITIES CLEAN" watu walipishwe faini za kutosha wakitupa taka hovyo, kuwe na dustbin mitaani, kuwe na sheria kali kama tu walivyozuia mifuko ya plastiki na ikatoweka. Majiji 6 hayawezi kutushinda kuwa masafi

Shida wala sio umasikini. Rwanda kuna umasikini kushinda Tanzania na bado miji yao kuanzia Kigali, Musanze nk ni misafi na iko civilized.

Shida sio uchumi. Tanzania inazidi Rwanda kuanzia GDP mpaka GDP per capita na bado Rwanda inaonekana civilized

Shida sio watu weusi. Rwanda 99% ya population ni watu weusi, na nchi yao ni safi.

Shida sio population. Because tell me inakuwaje Mbeya, jiji la watu laki 6 ni chafu kuliko Kigali yenye watu milioni 2?

📸 Kigali
View attachment 3593610View attachment 3593611View attachment 3593612View attachment 3593613View attachment 3593614View attachment 3593615View attachment 3593616View attachment 3593617View attachment 3593618View attachment 3593619View attachment 3593620View attachment 3593621View attachment 3593622View attachment 3593623
Mbona mji wenyewe hauna watu?
au umepiga picha masaki ukafikiri na kariakoo kupo hivyo hivyo?
 
Mbeya haiwezi kufikia Kigali. Ni pachafu mno, barabara zimechoka mbaya, na vumbi ndio usiseme. Haifikii hata robo ya Kigali
Walipoanzisha ile program yao ya kila mwezi,waliita(umuganda)
Kila raia awe anafanya usafi
Kwenye eneo lake,ilifanikiwa sana
Na sheria walizotunga na kuweka kwenye mambo ya
Usafi na mazingira wamefanikiwa,raia imewaingia kisawawasawa

Ova
 
Wabongo ustaarabu na usafi ni sifuri (zero) .

Tuwezacho sisi ni fitina, umbea, majungu, chuki, siasa za kipumbavu na kukata mauno ya singeli na vibao kata vya Bi Halima Kindamba.

Mtu akimaliza kula au kunywa chochote hata akiwa mjini kati kwenye gari, atafungua kioo cha gari, atupe uchafu nje bila kujali.

Ukipita mitaa ya Buguruni, unakuta uchafu umerundikwa barabarani kabisa. Hii barabara ya Nelson Mandela.

Ndio maana mitaro ya maji barabarani inaziba haraka sana kutokana na uchafu.

Waafrika hasa watanzania tuna uchafu na upumbavu wa milele.

Hapo Rwanda 🇷🇼, Ukipanda bodaboda ni LAZIMA na AMRI uvae Helmet 🪖 wewe na dereva. SIO OMBI. Ukikiuka hiyo faini utakayopigwa utasimulia.

Na hakuna ujinga wa kupakizana mishikaki.

Sisi watanzania bado tuna upumbavu ambao unahitaji kuondolewa kwa nguvu kubwa na sheria kali kabisa.
 
Mbeya haiwezi kufikia Kigali. Ni pachafu mno, barabara zimechoka mbaya, na vumbi ndio usiseme. Haifikii hata robo ya Kigali
Jamaa wako well organized sana kwenye mambo yao

Nje ya mada,niko naangalia hapa BAL basketball mashindano yao waliyoyaanda,ona walivyojopanga 😄

Ova
 
Serikali ikitilia mkazo unadhani itashindikana?

Halafu pia watu wenyewe usitarabu mdogo yaan unaenda kwa mtu alivyo jitupa tupa hovyo mavitu yapo hovyo hovyo huyu nyumbani kwake kuna mshinda ataweza huko njee bila kushikiwa bakora?
 
Wabongo ustaarabu na usafi ni sifuri (zero) .

Tuwezacho sisi ni fitina, umbea, majungu, chuki, siasa za kipumbavu na kukata mauno ya singeli na vibao kata vya Bi Halima Kindamba.

Mtu akimaliza kula au kunywa chochote hata akiwa mjini kati kwenye gari, atafungua kioo cha gari, atupe uchafu nje bila kujali.

Ukipita mitaa ya Buguruni, unakuta uchafu umerundikwa barabarani kabisa. Hii barabara ya Nelson Mandela.

Ndio maana mitaro ya maji barabarani inaziba haraka sana kutokana na uchafu.

Waafrika hasa watanzania tuna uchafu na upumbavu wa milele.

Hapo Rwanda 🇷🇼, Ukipanda bodaboda ni LAZIMA na AMRI uvae Helmet 🪖 wewe na dereva. SIO OMBI. Ukikiuka hiyo faini utakayopigwa utasimulia.

Na hakuna ujinga wa kupakizana mishikaki.

Sisi watanzania bado tuna upumbavu ambao unahitaji kuondolewa kwa nguvu kubwa na sheria kali kabisa.
Hivi dar mitaa ya upanga ile junction ya kwenda muhimbili bado chemba ya maji machafu inatema

Ova
 
Serikali ikitilia mkazo unadhani itashindikana?

Halafu pia watu wenyewe usitarabu mdogo yaan unaenda kwa mtu alivyo jitupa tupa hovyo mavitu yapo hovyo hovyo huyu nyumbani kwake kuna mshinda ataweza huko njee bila kushikiwa bakora?
Watu wachafu sana bila mkazo mambo hayawezi kwenda

Ova
 
Mbona mji wenyewe hauna watu?
au umepiga picha masaki ukafikiri na kariakoo kupo hivyo hivyo?
Hizo ni picha za Kigali. The cleanest city in East Africa so whatever point you want to make, is not valid. Kigali ni jiji safi asilimia kubwa, everyone knows that coz it's a fact
 
Back
Top Bottom