Dah Kukuelewesha Wewe Ni kazi ngumu Sana..
Ngoja Nitumie Lugha Yako Pengine utanielewa...
Mwanafunzi wa Madrassa alienda Chuoni..
Wanaanza Kumfundisha Herufi za Kiarabu ili aweze kusoma Vizuri Quran na Kwa ufasihi..
Kwa mfano:- Ukisema athumani alipelekwa Chuoni (Madrassa) na Mwalimu wake akaanza kumfundisha Aliph, ba ,Ta....
Nahisi Unajua Kuhusu
Noorani Qaida..
Huwezi kuanza Kusoma Qurani Mpaka Ujifunze Kwa ufasaha Kusoma Herufi (Huruf) na Jinsi zinavyotamkwa kwa kina na hiyo ndyo Elimu Inaitwa Nooran Qaida (Kwa waislamu Wote)..
Ukija kibongo Bongo Tunaita alif be te the....
Yesu alienda kwanza kujifunza Hizo herufi Na process Hiyo inaitwa
"לימוד אותיות" (limud otiyot)
Kama Ilivyo
Noorani Qaida Inamfungua Mtoto au Mtu mzima aliyesilimu Kuzijua Herufi vizuri kabla ya kuanza kusoma Qurani..
Pia Vivyo hivyo
Limud Otiyat nayo pia Inaanda mwanafunzi au mtoto kujifunza Herufi na matamshi yake Kabla hajaanza kusoma Torati..
Na hichonndo ulichoona Zakayo akiwa anamfundisha yesu..
TORATI na Qurani Haina tofauti..
Kwani zote zilihifadhiwa Kwenye Njia sawa...
Na Ukumbuke kuwa Hata Qurani Pia ilikuwa kwenye Vifua vya watu mpaka Pale walipoamua Kuiandika Kwenye Maandishi..
Je Hakikufikia Kisa Cha Ezra(Uziel) ambaye Baadhi ya Wayahudi Humuita Mwana w Mungu??
Baada ya Torati Ya Musa Kupotea Ni Nabii pekee Alikuwa amehifadhi Torati yote Bila Kuacha Nucta..
(Hiki kisa Kipo mpaka Kwenye Tarekhe za Visa vya Kiislamu)..
Kama unamkumbuka Nabii aliyelala kwa miaka 100 kama sijasahau..
Na kuwakusanya watu na Kuwasomea Torati...Hapo hapo Mfalme aliamuru Torati hiyo iandikwe na waandishi Wa Kifalme na Ikaguliwe na Ezra na Iweke kwenye Kumbukumbu Na hapo Ndiyo mwanzo wa Kuitwa
Deuteronomy..
Ambayo ni Maneno ya Kigiriki Yanayomaanisha
The second Torah au The second Law au The repeated Torah..
Na ndo maana Waswahili walipotafsiri wakaita Kumbukumbu La torati..
JAPO KWA WAYAHUDI WAO wanaita Simply
Deverim maana Yake
Maneno, Au
Mambo
kwa sababu Sura hiyo imeanza na..." Mambo/ Maneno haya yasitoke.."...
Ushahidi wa Ezra..
View attachment 3049327
Na Ezra 7:21
View attachment 3049328
View attachment 3049332
Kwa kusema Hayo Narudia Swali tena Unajua Torati Iko na Aina Ngapi??
Maana Kuna torati Iliyoandikwa Au The Written Torah (Torah Shebichtav) Hii ndo Mnaiona na Kuisoma kwenye Vitabu kama Mwanzo,Kutoka ,Walawi na Kumbukumbu...
na Kuna Aina ya Pili ya Torati Oral Torah (Torah Shebe'al Peh) Ambapo ili uweze kuijua Hii Ni muhimu au Ni lazma uwe Myahudi au Upitia Mafunzo ya Dini ya Kiyahudi ili kujifunza maana ndo imebeba Tafsiri ya Torati ya kwanza ni kama Mishnah,Talmud,Midrash na Halakha..
ndo maana Mwanzo nikasema Waislamu na Wakristo Wana ile torati ya Kwanza ambayo Ni written ila Torati kubwa Hawana na hawana pia elimu yake..
naendelea kulukaribisha kwenye Mjadala