Kwanini mali za umma zinachezewa namna hii?

Kwanini mali za umma zinachezewa namna hii?

Leverage

JF-Expert Member
Joined
Jan 25, 2021
Posts
2,125
Reaction score
3,150
Mkurugenzi mkuu wa shirika la reli (TRC) alisema moja kati ya changamoto za shirika ni watu kuchukua maeneo ya shirika. Mfano:
Akasema kuna eneo la reli ambapo reli ilitakiwa kupita kutoka Mwenge via Mbezi beach hadi kiwanda cha cement Wazo hill. Lakini hilo eneo sasa hivi limejaa maghorofa. Naamini masikini hana ubavu wa kuchukua eneo la serikali wala kubadili hati ya ardhi. Kwanini serikali muda wote imekaa kimya inamuogopa nani? Au ndio shamba la bwana heri, ng'ombe wa bwana heri basi yote heri?
Huu ni mfano mmoja tu ila yako maeneo mengi ya serikali watu waliyojimilikisha kama wamerithi.
 
... ni muda sahihi na rahisi zaidi kuhamisha kiwanda cha saruji kuliko raia. By the way kiwanda kilipo kwa sasa sio mahali sahihi. Kipelekwe maporini huko same to TBL na hata kambi za jeshi maeneo ya Mwenge to Kawe zihamishwe maeneo yale yabaki kwa matumizi mengine ya serikali.

Sehemu kubwa ya jiji inaweza kuhamishiwa maeneo yale kwa executive order itakayopangua order ya awali kwamba jiji la Dar ni Ilala.
 
Nafikiri lengo halikuwa kubeba cement tu na abiria pia wa ukanda huo
 
Nafikiri lengo halikuwa kubeba cement tu na abiria pia wa ukanda huo
... japo ripoti inasema lengo ni kuifikisha reli kiwandani Wazo; ripoti iko very specific.
 
Back
Top Bottom