Wakati nasoma shule ya msingi kulikuwa na watu mbalimbali wanakuja shuleni kufanya maonyesho ya mazingaombwe, yale maonyesho yalikuwa na buradani ya aina yake, wanafunzi wengi walikuwa wanalipia pesa ya kiingilio cha kuingia kutazama na wanafanya juu chini kupata siti za mbele katika ukumbi mdogo wa shule uliokuwepo.
Miaka mili ya kumalizia shule ya msingi haya maonyesho ya mazingaombwe yalikuja kupotea kabisa na siku hizi sidhani kama bado yapo kokote nchini, sijui kitu gani kilitokea kikaipoteza hii burudani.
Ni burudani kweli na fursa ya kushangaa-shangaa esp. kwa watoto huko mashuleni. Lakini kiuhalisia mazingaombwe ni aina fulani ya wizi (Ujanja)na huwajengea watoto fikra za Imani potofu ya Ushirikina kwa sababu:-
1. Magic au Mazingaombwe ni Utaalam mtu yeyote unaweza kujifunza wa namna ya kuficha, kuhadaa, kulaghai na kuteka akili ya mtazamaji/watazamaji.
Kwa bahati mbaya sana, Mwisho wa maonyesho hayo, Watoto waliotazama mwanzo-mwisho hawapati nafasi ya kuuliza maswali ni nini kilifanyika na kupata maelezo. Badala yake Watoto wanaachwa wajitafutie majawabu wao wenyewe. Hapo ujue wapo watoto ambao wataona ni uchawi, wapo watoto wataamini yale maneno ya mwoneshaji i.e. Abra-ca-dabra na wapo watakaoendelea kudadisi kilichojiri n.k. Wanayumbishwa Kiimani na hapo Sayansi inadhalilika - mfano inakuwaje mchanga uliochotwa hapo nje ya darasa unageuzwa kuwa sukari halisi? Inawezekanaje makaratasi /magazeti kugeuzwa kuwa fedha halisi noti za elfu tano tano tena nyingi? Inakuwaje mtu anawasha moto bila kiberiti au moto kutoka sehemu nyingine? Inakuwaje mtu anachomwa kisu hadi kinatokezea upande wa pili au kukatwa panga kichwani hadi likazama ndani lakini bado mtu huyo yupo hai na anaongea kwa mbwembwe?
2. Kwa kuzingatia nguvu ya soko; Mazingaombwe hayana tena mvuto wa soko (
Demand)na hivyo biashara ya mazingaombwe imepitwa na wakati.e.g. Hakuna Taasisi au mahali utakuta ajira ya mwanamazingaombwe.
Lakini pia Utaratibu wa kuonesha mazingaombwe kwenye Halaiki au Kadamnasi ya watu (
Public magic shows i.e. Public Conjurements) una mlolongo mrefu na usumbufu mkubwa usio wa lazima e.g. 1.mwoneshaji awe amejihakikishia uweza wa kuteka fikra na maono ya Jamii husika
2. Kupata kibali na kutoa matangazo ili wateja wafike kwa wingi.
3. Mwoneshaji atalipia gharama za eneo /ukumbi wa kuoneshea hayo mazingaombwe.
4. Mwoneshaji anatakiwa ajihakikishie Usalama kwa watazamaji na yeye mwenyewe.
5. Mwoneshaji mazingaombwe atanunua kwa gharama vifaa au mahitaji kwa ajili ya maonesho.
Hayo 1-5 ni baadhi ya changamoto katika kuwezesha Maonesho ya Mazingaombwe hadharani. Je, mwoneshaji anajihakikishia vp kwamba gharama zake binafsi zote hizo zitarudi?
Kwa mashuleni zama hizo ilikuwa ni rahisi tu kwani mhusika alikuwa ni mwalimu mkuu wa shule. Tofauti na Siku hizi yupo mwl.Mkuu, Elimu Kata, Kamati ya Shule, Elimu Taaluma(W), Afisa Utamaduni (W) n.k. na wote hao inabidi uwaone na waridhie jambo hilo.