Kwanini maonyesho mazingaombwe yaliacha kuonyeshwa shuleni na nchini?

Kuna Mwl alikuwa mke wa kigogo alitaga mayai hadharani toka hapo yalipigwa marufuku mjini kwetu yasionyeshwe tena
Nilikuwa sijanywa chai mkuu asante sana.

Ila hawa jamaa walikuwa wana burudani yake basi tu, walikuwa wanafunga mtaa kabisa
 
Ni burudani kweli na fursa ya kushangaa-shangaa esp. kwa watoto huko mashuleni. Lakini kiuhalisia mazingaombwe ni aina fulani ya wizi (Ujanja)na huwajengea watoto fikra za Imani potofu ya Ushirikina kwa sababu:-
1. Magic au Mazingaombwe ni Utaalam mtu yeyote unaweza kujifunza wa namna ya kuficha, kuhadaa, kulaghai na kuteka akili ya mtazamaji/watazamaji.
Kwa bahati mbaya sana, Mwisho wa maonyesho hayo, Watoto waliotazama mwanzo-mwisho hawapati nafasi ya kuuliza maswali ni nini kilifanyika na kupata maelezo. Badala yake Watoto wanaachwa wajitafutie majawabu wao wenyewe. Hapo ujue wapo watoto ambao wataona ni uchawi, wapo watoto wataamini yale maneno ya mwoneshaji i.e. Abra-ca-dabra na wapo watakaoendelea kudadisi kilichojiri n.k. Wanayumbishwa Kiimani na hapo Sayansi inadhalilika - mfano inakuwaje mchanga uliochotwa hapo nje ya darasa unageuzwa kuwa sukari halisi? Inawezekanaje makaratasi /magazeti kugeuzwa kuwa fedha halisi noti za elfu tano tano tena nyingi? Inakuwaje mtu anawasha moto bila kiberiti au moto kutoka sehemu nyingine? Inakuwaje mtu anachomwa kisu hadi kinatokezea upande wa pili au kukatwa panga kichwani hadi likazama ndani lakini bado mtu huyo yupo hai na anaongea kwa mbwembwe?
2. Kwa kuzingatia nguvu ya soko; Mazingaombwe hayana tena mvuto wa soko (Demand)na hivyo biashara ya mazingaombwe imepitwa na wakati.e.g. Hakuna Taasisi au mahali utakuta ajira ya mwanamazingaombwe.
Lakini pia Utaratibu wa kuonesha mazingaombwe kwenye Halaiki au Kadamnasi ya watu (Public magic shows i.e. Public Conjurements) una mlolongo mrefu na usumbufu mkubwa usio wa lazima e.g. 1.mwoneshaji awe amejihakikishia uweza wa kuteka fikra na maono ya Jamii husika
2. Kupata kibali na kutoa matangazo ili wateja wafike kwa wingi.
3. Mwoneshaji atalipia gharama za eneo /ukumbi wa kuoneshea hayo mazingaombwe.
4. Mwoneshaji anatakiwa ajihakikishie Usalama kwa watazamaji na yeye mwenyewe.
5. Mwoneshaji mazingaombwe atanunua kwa gharama vifaa au mahitaji kwa ajili ya maonesho.
Hayo 1-5 ni baadhi ya changamoto katika kuwezesha Maonesho ya Mazingaombwe hadharani. Je, mwoneshaji anajihakikishia vp kwamba gharama zake binafsi zote hizo zitarudi?
Kwa mashuleni zama hizo ilikuwa ni rahisi tu kwani mhusika alikuwa ni mwalimu mkuu wa shule. Tofauti na Siku hizi yupo mwl.Mkuu, Elimu Kata, Kamati ya Shule, Elimu Taaluma(W), Afisa Utamaduni (W) n.k. na wote hao inabidi uwaone na waridhie jambo hilo.
 
Kupotea Kwa raia wema ni sehemu ya mchezo huo.
 
Sisi shuleni kiingilio kilikuwa kinakusanywa wiki moja kabla, wajanja na wenye pesa wanawahi kulipia mapema wapate siti za mbele maana ilikuwa unaingia kwa kuitwa jina, mara ya mwisho kiingilio kilikuwa shillingi mia mbili hivi.
Mbona kama tumelipa kiingilio sawa kwa ajili ya mazingaombwe? Ndiyo kusema tulikua level sawa ya shule around same time
 
Sasa ulitaka akalie msumari kavu kavu..
We mchawi ety
 
Uwepo wa walokole shuleni! Palipo mlokole mazingaombwe ya kichawi/uganga/mazingaombwe kwishney!
 
Unasomema hayapo kwani bado upo huko shule ya msingi?!
 
Kwamba dogo alifariki!!πŸ€’πŸ€’πŸ€’
 
Kwamba dogo alifariki!!πŸ€’πŸ€’πŸ€’
hakufa ila hakuja shule kama wiki na siku kadhaa, nakumbuka stori ni alikuwa amelazwa alikutwa na matatizo ya kiafya.

Ila kilikuwa kipindi kirefu kweli maana kuna masela walikuwa wanatutishia eti sisi ndio tumemuua wanaenda kusema tukamatwe na polisi....utoto raha sana !
 
Basi hapo matumbo yakawa joto wenyeweee!!πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Sisi shuleni kiingilio kilikuwa kinakusanywa wiki moja kabla, wajanja na wenye pesa wanawahi kulipia mapema wapate siti za mbele maana ilikuwa unaingia kwa kuitwa jina, mara ya mwisho kiingilio kilikuwa shillingi mia mbili hivi.
Mkuu noma sana mimi kipindi kile tulikuwa tunachanga shilingi hamsini mpaka shilingi mia moja maisha yamebadilika sana jamani acheni tu
 
Waliacha baada ya mwana mazingaombwe mmoja kumuweka mtalimbo mwalimu mmoja wa kike kwenye paji la uso 🀣🀣🀣🀣🀣
 
Wazungu wana maonyesho mengi makubwa sana ya magic hadi kwenye media kubwa, ni biashara ya mabilioni ya dola.

Tatizo watz ulimbukeni umewajaa. Wazungu wanayafanya sana haya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…