Kwanini mara kadhaa alipo Rais Samia huambatana na Rostam Aziz?




Rostam ndiye Mkuu wa Kikosi binafsi cha rais cha mambo ya Ulinzi wa Kiuchumi, Biashara, Uwekezaji na Mahusiano ya Kimataifa.
 
Kipaumbile cha diplomasia na mahusiano na nchi za nje ni UCHUMI na sio siasa zisizo na tija.
Kwa hiyo ikitokea fursa ya rais au waziri kwenda nje inakuwa ni fursa ya wafanya biashara na wawekezaji wakuu nchini kukutana na wenzao huko
 
Kuna wakati akili ndogo zinafanana kabisa na Akili za Wachawi!
Watu wenye Husda na Roho Mbaya.

Bwn Rostam Azizi walau ni Mtanzania Kuna shida gani?

Mtu Huyu ni Mfanyabiashara mwenye uwezo Mkubwa wa Kuiwakilisha Sekta Binafsi kwenye Mpango wa Maendeleo wa Serikali.

Ebu fikiri
TAIFA gas ni Biashara inayoendeshwa na Bwn Rostam pamoja na Serikali.

Ni Mtanzania gani mwingine anayeweza kwenda pale Norway akaongeq Science ya Gas lets say LPNG na akatafsiri hapo Biashara?

Norway ni Mabingwa wa kuchimba Gas na Mafuta.

Lugha tu ya Upstream na Downstream ya Mafuta na Gas kwa wafanyabiashara wa kawaida ni misamiati mwanzo mwisho!

Tujengeane uwezo na tupendane mtu akipata fursa ya kukua tuache kuwanga!

Sent from my SM-A307FN using JamiiForums mobile app
 
Ukipata jibu uje nikupe posho ya mbunge siku moja, Ila CCM bhana ndio maana unashangaa makonda kutembea na msafara huyo naye bado nyuma take kuna watu pia, yaani kazi juu ya kazi
 
Hujaelewa shwari jamaa kauliza kwa nini kila anapokuwa rais naye yupo,majukumu yake ni nini?
 
Makubwa Rostan Rome kaenda kufanya nini?
huyu ndugu ni mfanyabiashara wa gesi.Ziara hii iliwapeleka hadi Norway nchi yenyè uzoefu wa kuchimba mafuta na gesi.
Serikali mara nyingi ni muwezeshaji wa wafanyabiashara katika kuwarahisishia shughuli zao na mataifa mengine.
 
Huyo ndio Mfanyabiashara Nguli na mshauri wa kimataifa. Huyu ni rafiki ya viongozi wote wa Afrika Mashariki- Uhuru Kenyatta, Samia, Kikwete , Mwinyi na wengine wengi. Tunatakiwa kujifunza toka kwake, uadui na viongozi wakuu hauna faida kwa biashara yako. Tenda kama kila kiongozi mkuu anavyotaka na wewe utafanikiwa. Tuache wivu na tujifunze mazuri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…