secretarybird
JF-Expert Member
- Aug 22, 2024
- 23,984
- 51,055
Kwanini mara nyingi watu wanashangaa ukijiita Mtanganyika, lakini ukijiita Mzanzibari wanaona kawaida?
Kivipi? Kiuchumi au 🤔.Zanzibar is another level.
Keep my word.
Wewe umeona uchumi tu?Kivipi? Kiuchumi au 🤔.
Noma sana mkuu.Wewe umeona uchumi tu?
Funguo jicho la tatu utajua kivipi.
Dah!Ushaambiwa zanzibar haikupoteza utaifa wake, taifa la tanganyika liko wapi mjuba?
Vipi kuhusu Zanzibar.Wanakushangaa kwa sababu ni kama kujiita mzimu wakati unatembea
Tanganyika ilishakufa kitambo kilichopo ni kivuli tu tena kwenye watu zaidi ya 70m+waliopo sasa waliozaliwa kipindi Tanganyika ina exist labda wamebaki laki mbili na ushee tu
Watu wa bara walikuzwa/wamekuzwa kutojibagua na kujitenga.Ndiyo(kinyume chake)maana anayetoka Zanzibar akijiita Mzanzibari hawatamshangaa.Kwa nini mara nyingi watu wanashangaa ukijiita Mtanganyika, lakini ukijiita Mzanzibari wanaona kawaida?
Ukijiita mtanganyika wanaanza kusema unataka kuvunja muungano.Watu wa bara walikuzwa/wamekuzwa kutojibagua na kujitenga.Ndiyo(kinyume chake)maana anayetoka Zanzibar akijiita Mzanzibari hawatamshangaa.
Katika kuidai Tanganyika hapo tupo wote.Kwa wazawa kiujumla,watu wa bara kujiita Watanganyika haijazoeleka vinywani na vichwani mwao.Ni rahisi sana mtu wa bara kujitambulisha kwa kabila lake au eneo/mkoa wa asili yake kuliko kuutamka Utanganyika.Utanganyika hujumuishwa ndani kwa ndani kwenye makabila na maeneo watokayo.Ukijiita mtanganyika wanaanza kusema unataka kuvunja muungano.
Huu ni ujinga bhana.
Ni kweli kabisa unayoyasema lakini Leo hii ukijitambulisha mbele ya watu fulani kama mtanganyika hawatafurahi. Watakufiria kama mtu anayetaka kuigawa nchi, wakati ukijitambulisha kama mzanzibari mbele ya hao hao watu itaonekena jambo la kawaida.Katika kuidai Tanganyika hapo tupo wote.Kwa mazawa kiujumla,watu wa bara kujiita Watanganyika haijazoeleka vinywani na vichwani mwao.Ni rahisi sana mtu wa bara kujitambulisha kwa kabila lake au eneo/mkoa wa asili yake kuliko kuutamka Utanganyika.Utanganyika hujumuishwa ndani kwa ndani kwenye makabila na maeneo watokayo.
Uangalie umri wa unaowaambia au mrengo wao kisiasa kwanza.Ni kweli kabisa unayoyasema lakini Leo hii ukijitambulisha mbele ya watu fulani kama mtanganyika hawatafurahi. Watakufiria kama mtu anayetaka kuigawa nchi, wakati ukijitambulisha kama mzanzibari mbele ya hao hao watu itaonekena jambo la kawaida.
Huu muungano ipo siku utavunjika tu! Sijui itakuwa lini.Uangalie umri wa unaowaambia au mrengo wao kisiasa kwanza.
Siku si nyingi.Kuna watu huwa wanajidai kuapa kuulinda lakini machoni tu unaona si kweli wanachokisema.Muda utaongea si muda sana.Muda upewe muda.Huu muungano ipo siku utavunjika tu! Sijui itakuwa lini.
Sahihi kabisa. Nataka hilo litokee ningali na uhai. Nishuhudia.Siku si nyingi.Kuna watu huwa wanajidai kuapa kuulinda lakini machoni tu unaona si kweli wanachokisema.Muda utaongea si muda sana.Muda upewe muda.
Ni upumbavu tu unao endekezwa na wapumbavu wanaolazimisha kuifuta Tanganyika kwenye historia ya dunia. Ni kawaida kwao kuwasikia wakkpotosha hadharani kwa kusema eti muungano ni kati ya Tanzania bara na Zanzibar! Mara Tanganyika ilifutwa mwaka 1964!!! Mara Tanganyika ni jina la Kikoloni!Kwa nini mara nyingi watu wanashangaa ukijiita Mtanganyika, lakini ukijiita Mzanzibari wanaona kawaida?
Eti mtu (tena wa serikalini) anakuambia tarehe 9/12/1961 Tanzania bara ilipata uhuru.Ni upumbavu tu unao endekezwa na wapumbavu wanaolazimisha kuifuta Tanganyika kwenye historia ya dunia. Ni kawaida kwao kuwasikia wakkpotosha hadharani kwa kusema eti muungano ni kati ya Tanzania bara na Zanzibar! Mara Tanganyika ilifutwa mwaka 1964!!!
Huu ni upotoshaji wa wazi kabisa. Ninashauri Watanganyika wenzangu wazalendo tuipiganie nchi yetu kabla wahuni hawajaipiga mnada yote kwa wageni. Na huu muungano wao wa kinyonyaji tuukatae kwa nguvu zote.
Kwa nini kuna mambo ya muungano na mambo yasiyo ya muungano?Ushaambiwa zanzibar haikupoteza utaifa wake, taifa la tanganyika liko wapi mjuba?