Kwanini Marais wa Kiafrika hawathaminiwi wakienda Nchi za Ulaya?

Vijana waliojifunza siasa ENZI za mwendazake ni shida sana hawajui maana ya UN general meeting
 
mkuu tema mate chini, Umemuona rais wa Brazil? yaani kazuiwa kuingia mgahawani kula kisa hajachanjwa akaona isiwe kesi.. yeye na mawaziri wake wakanunua pizza wakagawana then wanakula pembeni ya barabara.... Just imagine.
View attachment 1948115
 
Hawajaalikwa na marekani bali umoja wa mataifa
NI WAGENI WA KATIBU MKUU

Sent from my TECNO CA7 using JamiiForums mobile app
 
Kwani kuna Rais wa nchi nyingine (tufanye ulaya na kwingineko) amepokelewa ili tuone wetu kadharauliwa? Au ni mawazo finyu kujibana kuwaza kuhusu vinavyokuhusu??

Kupokelewa ni jambo dogo sana. Sijui kwanini umelikuza hivi.
 
Kwani Mheshimiwa Rais kaenda Ziara huko Marekani yani nikimaanisha kaenda kutembelea Marekani au kaenda Marekani kwa Sababu ya Tukio la UN?? Kama kaenda kwa Tukio la UN sa Marekani itahusika vipi na Mapokezi yake.(na huenda hata isijue kama kuna Rais kutoka Tanzania... JOKE😁)

Ila inshort ile safari kaenda kuhudhuria kikao cha UN sio kaenda Ziara Marekani ndio maana unaweza shangaa ukaona baada ya Mkutano wa UN ndio akakutana na Viongozi wa Marekani wa kubwa na kufanya nao Mazungumzo lakini sio saivi.
 

Hao wazungu wanajua fika viongozi wetu ni majizi ya kura. Hivyo hawana muda wa kupokea kwa heshima watu wanaoingia madarakani kwa kunajisi chaguzi za nchi zao.
 
Kama sijakosea ni kwamba, mama hakwenda Marekani kwa issues za Tanzania na USA, amekwenda kuhutubia mkutano wa umoja wa mataifa, issue ya USA inaingia kwasababu makao makuu ya UN yapo USA so yeye ni mgeni wa UN na sio USA
 
Mbona ule mkutano wa viongozi wa SADC kipindi cha dhalimu mpaka Mr. misifa Makonda alituzuia tusiooga tusije mjini?
 
Viongozi wa Afrika ni ma bingwa wa kuhujumu chaguzi, hiyo heshima nzuri ya kupokelewa vzuri kokote hawana, wapokelewe hivyo hivyo inatosha.
 
Kiongozi ni Kiongozi popote Duniani, Ka,a Mungu anawapa Heshima viongozi wewe ni nani hata ushindwe kunyenyekea?
 



JIFUNZE.
 
Marais wote wanaojielewa na kuthamini urais wao mikutano kama hii ya UN unatuma aidha mwakilishi au unarecord video.

JPM alifanya hivyo, Xi Jinping amefanya hivyo na nafikiri ndivyo inavyopaswa kuwa. UN general assembly ni kijiwe tu cha wanasiasa cha kutafuna kodi tu za wananchi wao kupitia gharama za misafara tu na matumizi huko Marekani.
 
Mathalani Rais wetu kipenzi mh. SSH amekwenda MAREKANI kwa ajili ya MKUTANO WA UMOJA WA MATAIFA-UNITED NATIONS GENERAL ASSEMBLY(UNGA) ambao huhudhuriwa na marais wengi sasa ulitaka AKAPOKELEWE NA mh.Rais Joe Biden?!!!Khaaa[emoji44]
Wewe kiaz ni UGA
 
Wao marais wa Africa ndio wanajipendekeza Ulaya
 
mkuu hio ni kawaida sana huko mambele hasa kwa nchi za marekani na ulaya,

yani kwa kifupi, kule kilamtu huwa yupo bize na mishe zake, inavoonesha wale hawajaumbiwa kuduwaa na kushangaa mabarabarani

kuna kipindi ze comedy kina masanja waliendaga huko. Aiseeee cha kushangaza walikuwa wanachekesha mabarabarani kabisa, lakini watu wanapita kama hawawaoni vile.

Yani wale jamaa hawanaga swaga za kushangaa shangaa kama wabongo, kila mtu kule huwa yuko bize na mambo yake.
 
Toka lini baba mwenye watoto masikini mwenye Shamba limetapika raslimali ambazo kashindwa kuzitumia akathaminika.
Watawala wa kiafrica ni zao la malezi mabovu ya waafrika kuhusu dhana ya maendeleo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…