Ukarimu ni utamaduni wetu watanzania na afrika kwa ujumla ambapo ni tofauti na watu was mabara mengine..kikubwa anazingatiwa ulinzi na usalama wake inatosha.
Wasomi wa kiafrika ni wababaishaji na hawafikiri nje ya kile walichokisoma kwenye vitabu vilivyoasisiwa na wazungu ndio maana hatuendelei.
Hakuna tofauti kati ya mzungu na mwafrika unapozungumzia suala la asili.
Tofauti ni mila za sasa na za zamani.
Binadamu wote kwa asili yao wanafanana kimifumo waliyopitia ya maisha.
Waafrika wanaelekea kule kule walipowazungu au waarabu.
Kwa sasa kwa mfano watu wanaoishi Dar es salaam na wale wa Vijijini kule usukumani, Singida ,umasaidi wanautofauti mkubwa sana kwenye suala la Ukarimu japo wote ni waafrika tena wa kizazi cha leo.
Ukifika maeneo hayo ya vijijini utakaribishwa kwa shamrashamra kubwa sana na ukarimu wa hali ya juu. Lakini ukienda Huko mijini hasa jiji lenye watu mabilionea kama akina Mo ,Bakheresa, Rugemalila,Manji na mzunguko mkubwa wa fedha utakuta ukarimu ni ziro. Hawana muda wa kupoteza. Wanaangalia mambo yao ,biashara zao, kazi zao, bize na simu ,mitandao ,kufanya mahesabu yao,vikao vya makazini ,harusi,michango n.k.
Hii ni miaka kama 150 tangu hayo maendeleo ya kisasa yaingie huku kwetu.
Fikiri miaka 50 ijayo mbele ili tukaribie miaka zaidi ya 2000 ya ustarabu na sayansi ya Mgiriki na Mrumi na 1000 ya Mwingereza.
Je, patakua na kitu kinachoitwa Mila na ukarimu wa Mwafrika??
Mimi nimebahatika kupata simuliza nyingi toka kwa bibi yangu ambaye aliishi zaidi ya miaka 110 , Bibi ambaye aliwaona Wajerumani wakiwa bado wanamizizi Tanganyika hasa wamisionari wa kijerumani. Walikua wanawambia Watanganyika wakati huo kuwa nyakati zikifika watu wote wataishi maisha yanayofanana na wale wa kule kwao ulaya. Wazee wengi wakawa wanabisha sana lakini wale wamisionari walikua wakiwapa Tahadhari kuwa wakati utafika kila kilichopo na kinachofanyika ulaya kitafanyika na Afrika kwa wakati kwa kwa sababu ya maendeleo. Walati huo mzungu peke yake alikua anaishi kwenye nyumba nzuri yenye umeme wa jenereta na kanisani palikua na Karabai na taa za Chemli. Waafrika walikua wanaishi kwenye nyumba za nyasi na moto wa kuni tu. Mkoloni akawaletea vibatari na mafuta ya taa ,tochi za betri n.k.
Lakini yote kwa yote kila binadamu alipitia kwenye kwenye teknolojia duni na hapakua na namna ya kuishi bila kuwa wajamaa na wakarimu kwa sababu dunia ilikua ni kubwa na wanafamilia walikua wanakaa pamoja kama ilivyo kwa wamasai wasiosoma.
Elimu ni Ufunguo wa ubinafsi na uovu wote duniani. Ukitaka Afrika ibaki ile ya watu wakarimu basi futa mitaala yote ya kizungu na teknolojia isiwe kigezo cha maendeleo endelevu bali maendeleo yawe ni utu ,haki na amani.
Waarabu ambao wamejitahidi kulinda asili kwa kiwango kikubwa ndio wanaojaribu kidogo kuonyesha ukarimu wa binadamu wa asili hasa wakati wa Mfungo wa Ramadhani japo wanaharibiwa na makundi ya wanasiasa wanaopenda kutawala kupitia Ugaidi( Ubinafsi)
Sent from my TECNO L8 Lite using
JamiiForums mobile app