Hawa wenzetu wameshapita kipindi cha "UJUHA" cha kuteketeza resources zao kwa ajili ya mtu, wao wapo ktk maendeleo zaidi na hawana kabisa muda wa kujipanga barabarani kwa masaa mawili kumsubiri mtu.
Nchi nyingi za Africa, bado tuna huo Ujuha au kwa lugha ya mtaani Ushamba. Hatujipi kazi ya kufanya uchunguzi kuwa tunapoteza muda kiasi gani kwa matendo kama hayo, au tunapoteza rasilimali kiasi gani kwa mambo kama hayo? Je vipaumbele vyetu ni nini? Tungekuwa tunafikiri kwa mtazamo huo, nadhani haya yanayotokea huko US, yasingetushangaza. Angalia mfano mmoja tu, Ukiona msafara wa Waziri Mkuu wa Uingereza, hauna gari zaidi ya 3, lakini ukiona msafari wa Maraisi wetu utaona kuna magari yasiyopungua 20. Hayo yote ni matumizi ya mtu mmoja, na ukiangalia kwa mwaka ni pesa nyingi sana. Wenzetu tayari wanavipaumbele vyao vya maendeleo, na si ujio wa Rais watu mpaka washone sare au uniform nk. Angalia mfano wakati wa kukimbiza Mwenge, ukiangalia Mwenge unapita eneo fulani si zaidi ya dk 30, lakini utaona watu wameshona vitenge au wamenunua T-shirt, hizo zote ni pesa za Umma.
Mifano ipo mingi, nadhani hy michache inatupa kujifanyia tathmini juu ya UJUHA wetu. Kiongozi analindwa utadhani tunaishi na Magaidi? Kiongozi anakuwa kama si binadamu sijui kiumbe gani? Tubadilike, hao viongozi ni watu kama sisi tu, tunahitahi mpango kazi wa maendeleo sio kuwashangilia watu barabani.
Hayo ya US na Nchi nyingine yasitushangaze, watu wako busy na kazi zao, wengine wanafanya kazi hata 3 kwa siku, huo muda wa kushangilia Viongozi haupo.