Wiki hii Serikali ya Rais Donald Trump imeishangaza ulimwengu kwa kuendelea na sera yake ya kuiandama China kwa kutoa muda wa saa 72 kufungua konseli kuu ya China mjini Houston, kwa kisingizio cha “kulinda taarifa binafsi za wamarekani na kulinda haki za ubinufu za wamarekani”. Wanaofuatilia kwa karibu habari za mvutano kati ya China na Marekani, wanajua kuwa hii sio sababu, bali ni kisingizio kingine cha serikali ya Rais Trump kuendelea na uhasama wake.
Tukiangalia matukio ya hivi karibuni, tunaweza kuona kuwa Marekani ilianza kuleta mvutano wa kibiashara na China kwa kuongeza ushuru kwa upande mmoja. Wakati ule ilionekana kuwa tatizo kati ya Marekani na China ni biashara isiyo na uwiano. Lakini wakati Marekani ikiendelea kutoonyesha udhati kwenye suala hilo, likaibuka suala la kampuni ya Huawei na Marekani ikaanza kuiwekea vikwazo kampuni hiyo na kuzishawishi nchi nyingine kuizuia kampuni hiyo.
Wakati suala hilo likiendelea, likatokea suala la virusi vya Corona na kisingizio cha kukosekana kwa uwiano wa biashara kikapoatea, na Marekani ikaanza kujaribu kulitumia suala la virusi vya Corona kuipaka matope China na kuichonganisha na nchi nyingine. Marekani imekwenda mbali zaidi kwa kufanya vitendo vya uchokozi waziwazi kwa kutuma manowari yake kwenye bahari ya China kusini, kitendo ambacho bila shaka ni uchokozi dhidi ya China.
Marekani na China ni nchi mbili zenye nguvu zaidi kiuchumi duniani. Marekani ndio nchi ambayo kwa muda mrefu imekuwa na nguvu kubwa ya ushawishi duniani, na hasa kuwa na uhuru wa kufanya jambo lolote duniani baada ya kusambaratika kwa Urusi. Lakini sasa hali ya dunia imebadilika, China imekuwa ni nchi inayokua kiuchumi na kuwa mshindani wa Marekani, na kuifanya Marekani iwe na hofu kuwa China inataka kuchukua nafasi yake duniani.
Lakini tukiangalia kwa undani katika hali ya kawaida, nchi yoyote ikifanya juhudi za kujiletea maendeleo na kuboresha maisha ya wananchi wake, matokeo yake yatakuwa ni nchi hiyo itakuwa na maendeleo. Juhudi za China kujiendeleza ndio zimeiletea maendeleo China, na maendeleo ya China sio kama tu yamekuwa na manufaa kwa wachina peke yao, bali pia yamekuwa na manufaa kwa Marekani na kwa nchi nyingine duniani. Kama maendeleo ya nchi nyingine yakichukuliwa kuwa ni hatari kwa nchi nyingine, basi ina maana dunia itakuwa katika hali ya vurugu.
Kwa wanaoangalia suala hili kwa mtazamo wa karibu, tunaweza kusema kuwa vitendo vya uhasama vinavyoonyesha hasa na Rais Trump na waziri wa mambo ya nje wa Marekani Bw. Mike Pompeo, ni janja ya kisasa kutaka kupata uungaji mkono kwa chama cha Republican kwenye uchaguzi mkuu utakaofanyika mwezi Novemba, lakini huu ni mchezo hatari ambao madhara yake ni makubwa.
Kuna wanaoweza kufikiri kuwa mvutano kati ya China na Marekani, ni suala la mafahari wawili na halina uhusiano na nchi za Afrika, lakini tukumbuke kuwa “Mafahari wawili wanapogombana zinazoumia ni nyasi”. China imesema ina uwezo wa kuhimili na kujibu uchokozi wa Marekani. Kwa nchi za Afrika bila shaka kama hali ikiwa mbaya, nchi zetu hazitakuwa kwenye hali nzuri.
China na Marekani ni nchi zenye ushawishi mkubwa kiuchumi duniani. Umuhimu wa uchumi wa China hasa kwa watu wa kawaida barani Afrika iwe ni wafanyabiashara au wateja, umeonekana wazi. Kama mvutano wa China na Marekani ukiongezeka na kutatiza biashara, basi madhara yatakuwa makubwa.