Kwanini mashine za EFD zijae? Si ni unyonyaji mwingine

Kwanini mashine za EFD zijae? Si ni unyonyaji mwingine

Hebu tuwekee wazi mashine yako ni kampuni gani huenda tukafaidika kujua nani ni bomu zaidi,.Lakini pia hii ni miaka mitano tu,Jee kama ikiharibika leo umeridhia kulipa tena takriban laki 7 mpaka 8 kununua nyengine au ungependa idumu zaidi na hizo pesa ukala na wanao.
Hii kitu hata ofisini kwa jirani yangu imetokea miezi miwili iliyopita, ilianza kugoma kupeleka akaambiwa imejaa so amenunua nyingine, hii iliyojaa amekaa nayo miaka 5,ni hizi incotex.
 
Yawezekana wewe uko huko huko ndio maana unajua njia za kupitia kwa sisi wengine urasimu unakufanya usamehe tu.Na ukikazia kudai ndio unawakaribisha wakufanyie visa vya kukudai zaidi na kufukua mahesabu ya zamani.
Tujaalie unarudishiwa kweli.Sasa hizi unazorudishiwa si ni pesa vile vile zimetoka serikalini umerudishiwa wewe.Faida iko wapi.Afadhali kuwe na mfumo bora wa kupata kodi bila kumnyonya mfanyabiashara na serikali inachopata kibaki na kutumika vizuri. Isiwe kuna kugawana baina ya TRA,watengenezaji na wasambazaji kwa jasho la mfanyabiashara,
Hujui mambo ya TRA wewe sio mlipa kodi period. Maana unachobisha Ni kitu kipo.
 
Ushawahi kwenda TRA kulipa kodi ukawaambia nalipa pungufu kwasababu nimenunua EFD ? Mfano unadaiwa 2m ukawaambia nalipa 1.3m kwasababu 700,000 nimenunua EFD?
Huwa wanafanya hivo rrondo .Kama hukukatwa hela yako ya mashine basi ukadai.nenda na risiti andika barua
 
Hapo kuna uhuni mkubwa. Lakini huu ndiyo wakati wa wafanyabiashara na chama chao kusikika.
 
Kwa kweli kwenye hizi mashine ni majanga matupu ni utapeli wa hali ya juu
Jana nilipeleka mashine kwa wakala ili kubadilisha battery akanichaji shilingi 40 elf ki battery chenyewe kidogo kama cha saa
Baadae nikaingia mtandaoni kuona bei zake hizo battery zinauzwa kwa pakiti moja yenye battery 12 USD 1.5 ambayo ni sawa na shilling 3500
Ambayo ukichukua 3500÷12= 291.66 kwa pc moja lakini tunaiziwa elfu 40

Hata kama bei hii ni imported inje China bado Bei ni kubwa mno
Waruhusu tuagize wenyewe wao walinde mfumo wao
Nimejikuta nacheka tu
Yaani hako kabetri 40k ?
 
Msambazaji wangu ndio muhuni zaidi. Yeye kila mwaka analazimisha ukaifanyie service kwa 150,000/- mimi nikawa siendi sasa hivi wameiwekea code ikifika mwaka inadai service usipoenda haifanyi kazi. Hio service ni wizi tu maana hamna jipya.
Kama kweli hizi mashine zinasaidia kuongeza mapato ya serikali itakuwa ni uzembe mkubwa wa TRA kuruhusu maslahi ya kampuni binafsi kuwa mbele kuliko maslahi ya taifa.Inakuwaje mashine ijae na iache kufanya kazi kwa kuwa tu kampuni inataka tsh.150,000 na hawajapewa na wao wanafungia mashine.
 
Wananchi wale nyasi lkn raisi anunue ndege ya kutembelea, chanzo kikubwa ni selikali kutaka kodi haijalishi mlipa kodi anamtaji gani anapataje faida nk,mfano hiki Kitambulisho cha machinga wapo wenye maduka ambayo kwa kuyatazama tu unakuta mtaji wake haufiki million 2 wakaamua kukata Kitambulisho kwa sababu ndio mkuu WA nchi alivyosema wakija hata tra wanasema hiyo hawaitambui

Sent from my itel S11 using JamiiForums mobile app
Ndiyo maana Tundu Lissu kasema atapeleka Muswaada wa Taxpayers bill of right.
 
Kama mliyoyaandika humu ni ya kweli basi tunaweza kusema serikali yenu iko enzi za zama za mawe za mwanzo

Sijui kwa nini serikali ya maccm wamekuwa wazito sana kuimalisha mifumo ya TEHAMA ya nchi hii

Nafuatilia huko Rwanda serikali iko inahamasisha watu kutumia cashless payment system ili waweze kupunguza gharama za kuchapisha pesa ila huku kwetu ndio kwanza wanazuia hata kupokea hela kwa PayPal nk.
 
Mimi TRA wanachonikera tu kila wakija kwako hawakosi kosa Mara mashine imefyokofyoko sijui nini
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] Dah we jamaa hadi nimetamani nikujue.... [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama mliyoyaandika humu ni ya kweli basi tunaweza kusema serikali yenu iko enzi za zama za mawe za mwanzo

Sijui kwa nini serikali ya maccm wamekuwa wazito sana kuimalisha mifumo ya TEHAMA ya nchi hii

Nafuatilia huko Rwanda serikali iko inahamasisha watu kutumia cashless payment system ili waweze kupunguza gharama za kuchapisha pesa ila huku kwetu ndio kwanza wanazuia hata kupokea hela kwa PayPal nk.
Serikali inaendeshwa na watu primitive ndio tatizo....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Imebidi niandike tuu kwa nn TRA wasiruhusu kama ukishindwa kufanya biashara ile mashine uweze kuuza kwa wenye uwezo wa kufanya biashara wapo wengi wenye nazo ndani zimekuwa ni toy's kwa ajili ya kuchezea watoto
Ilhali wamezinunua zaidi ya laki saba kwao
 
We have good comments from contributors here, I hope TRA is listening to these comments or they tried these gadgets before in the market before coming to finalize the design. If not they are not very late they can still modify and waive these problems to taxpayers.
 
Hiyo mashine Ina memory chip kama ya computer au simu.
Ikijaa data ndiyo inabidi ununue mashine nyingine.
Sio kweli.Sasa niemeelewa vizuri. Hizi mashine zimewekewa kiwango cha siku za matumizi ndio maana kila siku inakulazimisha utoe z-repot.Zikifika 2000 sawa na miaka 5 na miezi 4 lazima isite kufanya kazi na ununue nyengine hata kama kila kitu kiko sawa.
Zipo sababu kadhaa hapo katikati zitakazokufanya uipeleke kwa kampuni iliyokuuzia ili kurekebisha baadhi ya vitu kama kuganda kwa vifungo na kadhalika na tena kwa gharama kubwa.Anaweza akatoa zreport kadhaa katika majaribio na zote zinahesabiwa.Hata kazini kwako unaweza kulazimika kutoa zreport kimakosa na zote ziko kwenye hesabu.Hatimae umri wa mashine unazidi kushuka ndio maana ya kwangu imisha muda wake mapema na hata sijajipanga kununua nyengine.
 
Hivi vile vitambulisho vya 20000 bado vipo ? ,,je kama vipo nikihitaji naenda TRA au halimashauri.?
 
Back
Top Bottom