Teamanaconda
JF-Expert Member
- Jun 21, 2013
- 602
- 564
Hii kitu hata ofisini kwa jirani yangu imetokea miezi miwili iliyopita, ilianza kugoma kupeleka akaambiwa imejaa so amenunua nyingine, hii iliyojaa amekaa nayo miaka 5,ni hizi incotex.Hebu tuwekee wazi mashine yako ni kampuni gani huenda tukafaidika kujua nani ni bomu zaidi,.Lakini pia hii ni miaka mitano tu,Jee kama ikiharibika leo umeridhia kulipa tena takriban laki 7 mpaka 8 kununua nyengine au ungependa idumu zaidi na hizo pesa ukala na wanao.
Hujui mambo ya TRA wewe sio mlipa kodi period. Maana unachobisha Ni kitu kipo.Yawezekana wewe uko huko huko ndio maana unajua njia za kupitia kwa sisi wengine urasimu unakufanya usamehe tu.Na ukikazia kudai ndio unawakaribisha wakufanyie visa vya kukudai zaidi na kufukua mahesabu ya zamani.
Tujaalie unarudishiwa kweli.Sasa hizi unazorudishiwa si ni pesa vile vile zimetoka serikalini umerudishiwa wewe.Faida iko wapi.Afadhali kuwe na mfumo bora wa kupata kodi bila kumnyonya mfanyabiashara na serikali inachopata kibaki na kutumika vizuri. Isiwe kuna kugawana baina ya TRA,watengenezaji na wasambazaji kwa jasho la mfanyabiashara,
Huwa wanafanya hivo rrondo .Kama hukukatwa hela yako ya mashine basi ukadai.nenda na risiti andika baruaUshawahi kwenda TRA kulipa kodi ukawaambia nalipa pungufu kwasababu nimenunua EFD ? Mfano unadaiwa 2m ukawaambia nalipa 1.3m kwasababu 700,000 nimenunua EFD?
Well, mimi nimeiweka kwenye expenses.Huwa wanafanya hivo rrondo .Kama hukukatwa hela yako ya mashine basi ukadai.nenda na risiti andika barua
Nimejikuta nacheka tuKwa kweli kwenye hizi mashine ni majanga matupu ni utapeli wa hali ya juu
Jana nilipeleka mashine kwa wakala ili kubadilisha battery akanichaji shilingi 40 elf ki battery chenyewe kidogo kama cha saa
Baadae nikaingia mtandaoni kuona bei zake hizo battery zinauzwa kwa pakiti moja yenye battery 12 USD 1.5 ambayo ni sawa na shilling 3500
Ambayo ukichukua 3500÷12= 291.66 kwa pc moja lakini tunaiziwa elfu 40
Hata kama bei hii ni imported inje China bado Bei ni kubwa mno
Waruhusu tuagize wenyewe wao walinde mfumo wao
Kama kweli hizi mashine zinasaidia kuongeza mapato ya serikali itakuwa ni uzembe mkubwa wa TRA kuruhusu maslahi ya kampuni binafsi kuwa mbele kuliko maslahi ya taifa.Inakuwaje mashine ijae na iache kufanya kazi kwa kuwa tu kampuni inataka tsh.150,000 na hawajapewa na wao wanafungia mashine.Msambazaji wangu ndio muhuni zaidi. Yeye kila mwaka analazimisha ukaifanyie service kwa 150,000/- mimi nikawa siendi sasa hivi wameiwekea code ikifika mwaka inadai service usipoenda haifanyi kazi. Hio service ni wizi tu maana hamna jipya.
Ndiyo maana Tundu Lissu kasema atapeleka Muswaada wa Taxpayers bill of right.Wananchi wale nyasi lkn raisi anunue ndege ya kutembelea, chanzo kikubwa ni selikali kutaka kodi haijalishi mlipa kodi anamtaji gani anapataje faida nk,mfano hiki Kitambulisho cha machinga wapo wenye maduka ambayo kwa kuyatazama tu unakuta mtaji wake haufiki million 2 wakaamua kukata Kitambulisho kwa sababu ndio mkuu WA nchi alivyosema wakija hata tra wanasema hiyo hawaitambui
Sent from my itel S11 using JamiiForums mobile app
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Mimi TRA wanachonikera tu kila wakija kwako hawakosi kosa Mara mashine imefyokofyoko sijui nini
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] Dah we jamaa hadi nimetamani nikujue.... [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]Mimi TRA wanachonikera tu kila wakija kwako hawakosi kosa Mara mashine imefyokofyoko sijui nini
Serikali inaendeshwa na watu primitive ndio tatizo....Kama mliyoyaandika humu ni ya kweli basi tunaweza kusema serikali yenu iko enzi za zama za mawe za mwanzo
Sijui kwa nini serikali ya maccm wamekuwa wazito sana kuimalisha mifumo ya TEHAMA ya nchi hii
Nafuatilia huko Rwanda serikali iko inahamasisha watu kutumia cashless payment system ili waweze kupunguza gharama za kuchapisha pesa ila huku kwetu ndio kwanza wanazuia hata kupokea hela kwa PayPal nk.
Inajaa vipi? Kwamba unalipa sana kodi ndio inajaa(bilioni ngapi inajaa)?
Ukiniona hutaamini[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] Dah we jamaa hadi nimetamani nikujue.... [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Sent using Jamii Forums mobile app
Asikuombe namba tu bado tunakupenda maana kwasasa serikali yetu haitaki ukweli ukiwa mkweli hadharani umepoteaUkiniona hutaamini
Usihofu chiefAsikuombe namba tu bado tunakupenda maana kwasasa serikali yetu haitaki ukweli ukiwa mkweli hadharani umepotea
Sio kweli.Sasa niemeelewa vizuri. Hizi mashine zimewekewa kiwango cha siku za matumizi ndio maana kila siku inakulazimisha utoe z-repot.Zikifika 2000 sawa na miaka 5 na miezi 4 lazima isite kufanya kazi na ununue nyengine hata kama kila kitu kiko sawa.Hiyo mashine Ina memory chip kama ya computer au simu.
Ikijaa data ndiyo inabidi ununue mashine nyingine.