Kwanini maumbo na majina ya kijinsi yalikuwa hivi?

Kwanini maumbo na majina ya kijinsi yalikuwa hivi?

Ni kwanini waliamua kuita hivyo, huyo aliyevipa majina alifikiria nini na alitumia vigezo gani. Na ninani basi mwanzilishi wa majina ya kijinsia na haya maungo ya kijinsia?
Tafuta clip ya erik omondi uone orign ya viumbe kama tilapia na wengine (joke)
 
Mambo mengi au vitu vingi hapo zamani vilikuwa vina sababu au vina maana fulani ya kuwa hivyo vilivyo au kupata jina hilo.

Viumbe wote wenye jinsia ya kike wana kiungo kiitwacho uke, na hicho kiungo ndio kinatofautisha umbo na umbile na majukumu na tofauti nyingi baina ya hizi jinsia.

Kwakuwa jukumu la msingi la jinsia ya kike ni kupokea mbegu, kisha kuzihifadhi na kuzikuza kwa muda fulani, ili kuendeleza kizazi chenye nasaba zao, hivyo akawa na viungo vyenye uwezekano huo.

Pia kwakuwa mbegu zipo kwenye jinsia ya kiume, hivyo jinsia hii ikawa na kiungo chenye uwezekano wa kuziingiza mbegu hizo kunakotakiwa, kiungo hicho kikaitwa uume.


Mwenye uke ikawa mwanauke ambayo ndiye mwanamke.
Mwenye uume ikawa mwanaume.
Yaani ni utambulisho kutokana na ulichobeba hapo kati.
 
Kuhusu mavazi na majina hayo ni mapendekezo tu kutokana na sababu mbalimbali.

MAJINA kazi yake ni utambulisho na kwa ajili ya kutofautisha hiki na kile, mwanzoni yalikuwa yanatolewa kwasababu fulani au tukio, mfano kipindi mtoto anazaliwa, haikuzingatiwa sana jinsia ya mtoto, jina kama vile furaha, mawazo, upendo, zawadi, nk. utakuta jina lipo kwa wanawake na wa kiume.

Sasa ilipotokea kurithisha watoto majina ndipo kukaanza migawanyiko yaani mtoto wa kike aitwe jina la babu yake?
Ndipo ikaanza kutofautishwa kusemwa hili lakike hili la kiume nk.

MAVAZI kazi yake ni kukinga mwili, kutokana na mazingira na majukumu ya watu husika.
Kwa mfano joho, kanzu, panjabi, mavazi ya kinigeria na mavazi fulani hivi ya kichina. Ukitazama vizuri hayana tofauti na magauni.

Wanaume wana purukushani na mbilinge nyingi, hivyo yakaundwa mavazi ambazo ndio haya masuruali, ambazo zina muundo unaowezesha kuruka hata makorongo bila shida.

Kwahiyo mambo ya fasheni, majukumu, mazingira na mtazamo tu ndio unatofautisha mavazi.
 
Hata majina ya wanyama nayo yana sababu zake, majina ya nchi, mikoa na hata jina la kabila zetu zina maana zake na sababu zake.

Kwahiyo kuna majina ya utambulisho wa jumla, wa kundi, mahususi, nk.
kama vile wote tunaitwa viumbe. Kisha kwenye viumbe tunapata mimea, ndege, wadudu, wanyama nk.

Kwenye wanyama kuna watu, mbuzi, tembo nk.

Utu ndio tabia inayotambulisha kuwa sisi ni watu.

Mbuzi wamepata jina hilo kwasababu ya tabia yao ya upuuzi.

Mtiririko unaendelea zaidi hadi kufikia kutambulika kiumbe kwa ubinafsi wake.

Mtu mwenye uke atatambulika kuwa ni mwanamke, mwenye uume ataitwa mwanaume.

Hayo yote ni mgawanyo wa majina na sababu zake, lakini malengo ya jina ni utambulisho tu katika jamii.
 
Back
Top Bottom