Kuhusu mavazi na majina hayo ni mapendekezo tu kutokana na sababu mbalimbali.
MAJINA kazi yake ni utambulisho na kwa ajili ya kutofautisha hiki na kile, mwanzoni yalikuwa yanatolewa kwasababu fulani au tukio, mfano kipindi mtoto anazaliwa, haikuzingatiwa sana jinsia ya mtoto, jina kama vile furaha, mawazo, upendo, zawadi, nk. utakuta jina lipo kwa wanawake na wa kiume.
Sasa ilipotokea kurithisha watoto majina ndipo kukaanza migawanyiko yaani mtoto wa kike aitwe jina la babu yake?
Ndipo ikaanza kutofautishwa kusemwa hili lakike hili la kiume nk.
MAVAZI kazi yake ni kukinga mwili, kutokana na mazingira na majukumu ya watu husika.
Kwa mfano joho, kanzu, panjabi, mavazi ya kinigeria na mavazi fulani hivi ya kichina. Ukitazama vizuri hayana tofauti na magauni.
Wanaume wana purukushani na mbilinge nyingi, hivyo yakaundwa mavazi ambazo ndio haya masuruali, ambazo zina muundo unaowezesha kuruka hata makorongo bila shida.
Kwahiyo mambo ya fasheni, majukumu, mazingira na mtazamo tu ndio unatofautisha mavazi.