Kwanini Mazoezi hayanisaidii?

Kwanini Mazoezi hayanisaidii?

Kwa kifupi ni kwamba hufanyi mazoezi yoyote wewe!!.....Mazoezi ya kupunguza mwili siyo kitu kirahisi kama kula pilau la xmas!!......Wewe unaenda kucheza cheza then unasema kuwa unafanya mazoezi???[emoji32][emoji32][emoji32]
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] nimecheka sana aisee
 
Usikate tamaa mkuu.
Mtafute Dr. Boaz Mkumbo MD atakusaidia
Utampata Facebook pia Youtube ana channel yake, vilevile anavitabu vyenye maelekezo ya kupungua, chukua namba kwenye page yake mtafute atakuelekeza ofisini kwake mwananyamala.
Jamaa amesaidia wengi kupunguza uzito wa mwili pamoja na kuondokana na magonjwa ya kisukari, pressure, ngozi etc kwa kutumia mwongozo wake wa "HEALTHY EATING ACADEMY (HEA)"
Kwa kifupi unatakiwa kukwepa kabisa vyakula vya sukari & wanga.
Utapungua hata bila ya mazoezi
Lakini ukifuata lishe pamoja na mazoezi utapungua kwa speed.
Kasi ya kupungua & kupona figisu za mwili inatofautiana kati ya mtu na mtu, kuna mtu ndani ya wiki 2 anaona matokeo, mwengine hadi baada ya miezi kadhaa ndipo ataona matokeo.
Pia kua makini matapeli ni wengi, wengine tulikua wanafunzi wake na tunajidai kukomboa watu kwa mgongo wa jamaa.
YOTE KWA YOTE UNATAKIWA UKAZE UZI KWELIKWELI ILI KUFIKIA MALENGO, SIO KITU RAHISI
Binafsi nilipunguza kilo 11 ndani ya siku 100
ulipunguaje? nataka kupungua sana tumbo
 
Kwa kifupi ni kwamba hufanyi mazoezi yoyote wewe!!.....Mazoezi ya kupunguza mwili siyo kitu kirahisi kama kula pilau la xmas!!......Wewe unaenda kucheza cheza then unasema kuwa unafanya mazoezi???[emoji32][emoji32][emoji32]
Hahahahaha Wewe una kilogiramu ngapi rafiki??


Cc Smart911
 
Hakuna dkt wa kupunguza mwili mjomba. Kikubwa cha kufanya ni zoezi, zingatia chakula bora, muda wa kupumzika na kiwango cha maji unachokunywa. Na kutoa nafasi kati ya maji na chakula.
 
Hakuna dkt wa kupunguza mwili mjomba. Kikubwa cha kufanya ni zoezi, zingatia chakula bora, muda wa kupumzika na kiwango cha maji unachokunywa. Na kutoa nafasi kati ya maji na chakula.
kwahiyo akitoka tizi ashushie na sprite au pepsi baridi? huku sahani la ubwabwa likimngojea.
pia sio kila mazoezi ni yakupunguza uzito, mengine unaongeza uzito.
yote kwa yote ni kuzingatia eating discipline (na hapa ndipo kwenye mtihani).
 
Mazoezi ni taaluma!

Kama kwenye Mazoezi yako unachoma Calories 120 Halafu unatupia msosi Wenye calories 130 utapunguaje?
Mtu anachoma calories 160 ila menu kwa siku ukijumlisha na monde inagonga calories 2,800. Hapo kitambi na unene utabakia kusema ni "wa asili"
 
pole lkn katika kupunguza mwili ,,, asilimia 70 ya kupunguza inahusiana na diet asilimia 20 mazoezi na 10 ni vingine kama muda wa kula, muda wa kulala, mambo ya stress maana ukipunguza uzitobwakati una mistress hupungui labda mawazo ndo unapungua. chakukuchauri acha kabisa kula vyakula vya wanga na sukari vyote kwa aina zake, kula samaki nyama ,matunda mboga za majani, nuts kama almonds, korosho,flaxseeds, chiaseed afu usile mara kwa mara kula tu pale unaposikia njaa, afu jua kutofautisha kati ya hamu ya kula na njaa, usile chakula unapokuwa na hamu
 
ukifanya diet hiyo utapungua kwa mazoezi hayohayo unayofanya, kula kwa afya usishinde njaa kula unaposikia njaa usile kwa hamu. na kama unene unauchukia anza kuchukia pia chakula, mimi nimetoka 115- 78kg
 
Ndugu cha kwanza lazima utambuwe sababu iliyokufanya kunene ni ipi, punguza hiyo sababu punguza kula vyakula sukari, ugali wali na kwa ujumla wanga.
Mtu anayefanya mazoez ni ngumu kupunguza uzito kwa sababu unafanya mazoez half ukirudi kwenye unaendelea kula vyakula vile vile
 
Habari wakuu wa humu JF,Mimi ni mnene sana Nina 105 kg nimepima Juzi.

Najitahidi sana kufanya Mazoezi lakini sipungui,Kwa kweli nauchukia unene kuliko kitu chochote na mbaya zaidi Nina kisukari nashangaa wagonjwa wenzangu wakipungua na wako na mwili mzuri.

Je Kwanini Mimi Mazoezi hayanisaidii?
Fanya diet,...
 
Habari wakuu wa humu JF,Mimi ni mnene sana Nina 105 kg nimepima Juzi.

Najitahidi sana kufanya Mazoezi lakini sipungui,Kwa kweli nauchukia unene kuliko kitu chochote na mbaya zaidi Nina kisukari nashangaa wagonjwa wenzangu wakipungua na wako na mwili mzuri.

Je Kwanini Mimi Mazoezi hayanisaidii?
PUNGUZA KG 5 KWA SIKU 7.

Ni watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha maradhi mbalimbali bali pia mwonekano wako unakuwa si mzuri. Makala haya yanaeleza namna ya kupunguza unene ndani ya siku saba.

Siku ya 1: Asubuhi kula matunda (lakini usile ndizi). Mchana chemsha kabichi, weka chumvi kidogo na nyanya, chemsha na upate supu. Kula mchanganyiko huo na utajiona umeshiba. Jioni kula tikiti maji na mbogamboga au kabichi uliyotengeneza mchana.

Siku ya 2: Kula mboga za majani asubuhi (usile mboga za majani zenye wanga kama karoti). Mchana kula kabichi iliyochemshwa, tengeneza na kachumbari. Katika kabichi weka chumvi, pilipili na mafuta ya olive. Jioni unaweza kula mlo kama wa mchana lakini unaweza kukaanga mboga nyingine za majani.

Siku ya 3: Kula mboga za majani na matunda, unaweza kuongeza kiazi kitamu kimoja.

Siku ya 4: Kula ndizi moja na unywe na maziwa ya mtindi wakati wa asubuhi. Mchana kula kabichi kama ulivyoitengeneza kwenye siku ya kwanza, usiku rudia mlo wa mchana.

Siku ya 5: Kula nyanya nne pamoja na samaki au kipande cha kuku asubuhi. Mchana unaweza kula samaki wa kuchemsha kiasi ambaye amechanganywa na nyanya. Wakati wa jioni unaweza kula chakula kama cha mchana.

Siku ya 6: Unaweza kula chakula cha protini na mboga za majani. Anza kwa kula kachumbari asubuhi. Mchana kula tambi kiasi na kipande kidogo cha samaki. Usiku tengeneza supu ya kabichi.

Siku ya 7: Anza kwa matunda na juisi. Mchana kula mboga za majani na usiku kula supu ya kabichi na kiazi kimoja.

Kumbuka: Unatakiwa kunywa maji angalau glasi nne kila siku. Usiendelee kwa muda mrefu, kumbuka dayati hii ni ni kwa siku saba pekee.

Source: Muungwana blog.
 
Carbs, carbs, carbs....
Refined sugar, sugar, sugar....

Google how to avoid/reduce those...

And you are set.
 
Back
Top Bottom